Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameiagiza Wizara ya Nishati kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuandaa mpango mkakati wa kuwajengea uwezo vijana na kampuni za Kitanzania ili washiriki kikamilifu katika miradi ya mafuta na gesi asilia.



Ametoa maelekezo hayo leo, Oktoba 28, 2026, jijini Dar es Salaam, katika hafla ya utiaji saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi.


Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais alimwita mbele kijana Mwizegwa Rusibamanyila, aliyeacha kazi nje ya nchi na kurudi nyumbani kuanzisha kampuni yake inayofanya kazi katika kitalu cha gesi cha Mnazi Bay, mkoani Mtwara. Kampuni hiyo imeajiri zaidi ya Watanzania 50, na asilimia 80 kati yao wanatoka katika kijiji kinachozunguka mradi huo. Miongoni mwao ni binti aliyeajiriwa akiwa bado mwanafunzi, akaendelezwa kielimu, na sasa ni mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.


“Kitengo cha local content tukikisimamia vizuri, tuna uwezo wa kuzalisha akina Rusibamanyila wengi zaidi ambao watakuja kuajiri Watanzania wenzao katika miradi ya mafuta na gesi,” amesema Mhe. Ndejembi.


Amesisitiza kuwa maandalizi ya vijana hao yaanze sasa, kabla miradi mikubwa ikiwemo mradi wa LNG mkoani Lindi haijakamilika, ili Watanzania wawe tayari kushiriki kama wataalamu, watoa huduma na wasambazaji wa bidhaa.


Aidha, amemshauri Waziri wa Nishati kuandaa tuzo maalum kwa kijana huyo kutokana na kazi kubwa anayoifanya.

 



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii  Nkoba Mabula ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa uboreshaji wa miundombinu ya barabara, maji, umeme, mawasiliano, vitendea kazi pamoja na utoaji elimu kwa watumishi na wadau mbalimbali kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na Mvua za El-nino zinazotarajiwa 



Akiwa katika ukaguzi wa miundombinu Ngorongoro Mabula ameelekeza spidi  kuongezeka kuboresha miundombinu ya maeneo hatarishi, mitambo, huduma za afya na kutoa Mafunzo ya vitendo kwa timu za uokoaji zinazohusisha maafisa na Askari wa jeshi la uhifadhi 



“Kama Elnino itakuja itukute tumeshajiandaa, mitambo, magari ya huduma, mafuta, na vipuri viwepo mda wote ili kuhakikisha usalama wa watalii, wananchi na rasilimali za Wanyamapori na malikale zilizopo pamoja na kuweka alama kwenye maeneo ambayo ni hatarishi ili kuongeza tahadhari kwa watumiaji” aliongeza Mabula. 




Akizungumza kwa Niaba ya Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro,  SACC Gloria Bideberi ameeleza kuwa katika kukabiliana na janga hilo hadi sasa imetoa elimu kwa Watumishi 200, Viongozi wa Vijiji na Kata 275,  wanafunzi wa shule zaidi ya 1550, Wananchi 4,965 kwenye  kata 10 zilizopo ndani ya hifadhi,maeneo ya huduma za malazi 80 na kuandaa magari ya magonjwa matatu na vifaa tiba.



Mratibu wa shughuli za Miundombinu Eng. Shaban Felician amebainisha kuwa mitambo zaidi 11 imeandaliwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara na uokozi wa magari ya wageni sambamba na kuhakikisha mtandao wa barabara ndani ya hifadhi wenye zaidi ya kilomita 600 zinapitika katika msimu wote wa mvua.

 


Aelekeza Viwanja vya Mizengo Pinda Kabungu kuwa eneo rasmi la Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi

TANGANYIKA, KATAVI — Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi katika Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi ili kujifunza fursa za kiuchumi na kuzitumia kuboresha maisha yao.



Prof. Shemdoe ametoa wito huo Oktoba 25, 2026, wakati akizindua rasmi maonesho hayo yanayofanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 31, 2026, katika Viwanja vya Mizengo Pinda Kabungu, Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi.



Amesema maonesho hayo ni fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za uzalishaji katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, viwanda na biashara, pamoja na kupata elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.



“Wananchi wa Katavi, jitokezeni kwa wingi katika viwanja hivi ili kujifunza namna ya kutumia fursa za kiuchumi katika kilimo, mifugo na uvuvi, viwanda na biashara, pamoja na mikopo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, na kutumia elimu hiyo kuendesha shughuli zenu za uzalishaji na biashara,” amesema Prof. Shemdoe.



Akizungumzia umuhimu wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, Prof. Shemdoe amesema maonesho hayo yanatoa fursa ya kujifunza kutoka kwa vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo na kutumia mitaji waliyoipata kuanzisha au kuendeleza shughuli za uzalishaji.



Ametolea mfano kikundi cha wanawake kilichopata mkopo wa Sh milioni 15 kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, ambacho kimefanikiwa kuanzisha uzalishaji wa mafuta ya mawese na sabuni na hivyo kupata kipato.

“Akina mama na vijana mliopo hapa, nendeni mkajifunze namna kikundi hicho kilivyoweza kurejesha mkopo na kupata faida iliyowawezesha kununua sare za shule na madaftari kwa watoto wao wanaonufaika na elimu bila ada, huku wengine wakimudu gharama za kuwasomesha watoto wao katika shule binafsi,” amesisitiza.

Prof. Shemdoe amesema ushuhuda huo unapaswa kuwa chachu kwa wanawake na vijana kujifunza namna ya kutumia mikopo kwa tija, kuendeleza shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato cha familia zao.

Katika hatua nyingine, ameelekeza Viwanja vya Mizengo Pinda Kabungu kuwa eneo rasmi la kufanyia Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi kila mwaka, hatua inayolenga kuweka utaratibu wa kudumu wa kuandaa maonesho hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amesema maadhimisho hayo yanalenga kuwaunganisha wananchi, wakulima, wafugaji, wachakataji, wazalishaji wa bidhaa mbalimbali, taasisi za umma na binafsi pamoja na taasisi za kifedha.

Amesema kupitia maonesho hayo, washiriki wanapata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi ya teknolojia mpya na za kisasa katika uzalishaji na uchakataji wa bidhaa, pamoja na kupata fursa za kuunganishwa na masoko.

Maonesho ya Wiki ya Mwanakatavi yalianza mwaka 2022 kufuatia tamko la kimkakati la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliyeelekeza kila mkoa kuandaa maonesho ya wiki baada ya Maonesho ya Nane Nane.

Lengo la mpango huo ni kuwawezesha wananchi kupata mrejesho kuhusu mafunzo na uzoefu uliopatikana kupitia Maonesho ya Nane Nane, pamoja na kuendeleza matumizi ya maarifa hayo katika shughuli za kiuchumi na uzalishaji.

 


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameeleza kuwa jitihada za Ngorongoro kuboresha miundombinu ya Utalii eneo la maporomoko ya maji na mapango ya Tembo Endoro ni silaha muhimu kutekeleza ilani ya CCM ya kufikisha Watalii milioni nane mwaka 2030 na kuitaka menejimenti kuendelea kusimamia ujenzi huo kwa kasi na viwango.



Akielezea  kufurahishwa kwake kutokana na kasi ya ujenzi katika eneo hilo, waziri Dkt. Kijaji amesema fedha za utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya utalii (TDL) zipo na hivyo ni jukumu la mamlaka kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.



Ameeleza kuwa  hadi sasa Ngorongoro imetengewa shilingi bilioni 10 kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara ambapo wakandarasi wameendelea kulipwa kwa kila hatua na fedha ipo.



 Kijaji amebainisha  kuwa kati ya fedha hizo shilingi 1,674,783,089.00  zitatumika kwa ajili ya miradi ya kivutio cha utalii Endoro na Ngoitoktok

vilivyopo eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 68 na mradi utakamilika mwezi Desemba, 2026.



Msimamizi wa Mradi huo SACC Mariam Kobelo ameeleza kuwa mradi wa Endoro unahusisha majengo ya Ofisi, geti, walking trails zenye urefu wa mita 2,200, boardwalk, alama za maelekezo, vyoo na maeneo ya kupumzikia wageni wakati katika eneo la Ngoitoktok mradi unalenga kuboresha mazingira eneo la picnic kwa kuongeza miundombinu ya kukaa na kupumzika kwa wageni.

 


Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa barabara ya tabaka gumu kutoka Loduare hadi geti la Seneto km 29.5 Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa mradi huo unaotekelezwa kwa miaka miwili kwa thamani ya shilingi Bilioni 80.36 unaendelea vizuri ambapo hadi sasa umefikia asimilia 8 ambapo nguvu kazi na usimamizi unaendelea kuimarisha ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati.



 

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewataka watumishi wake waliohudhuria mafunzo ya kiutumishi kwa siku tano mjini Dodoma kuyafanyia kazi mafunzo yao ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji.



Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo anayeshughulikia huduma za shirika Aidan Makalla ametoa rai hiyo kwa watumishi wakati akifunga mafunzo ya wiki moja yenye lengo la kuwajengea watumishi uelewa kuhusu utawala bora, usimamizi wa rasilimali watu, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uhifadhi, Utoaji wa huduma bora kwa wateja na nidhamu mahala pa kazi




Makalla amesema mamlaka imewekeza mtaji kwa watumishi hao kwa kuwapa elimu hiyo ya utumishi, maadili, uwekezaji,afya ya akili na itifaki ikiamini kwamba mafunzo ndiyo nyenzo muhimu katika uwajibikaji.



“Sisi viongozi wa mamlaka ni kama wazazi tuna wajibu wa kuwapa mafunzo ili msiharibikiwe na baadaye mamlaka ikaja kulaumiwa, yatumieni mafunzo haya kuyajenga katika kazi zenu,”alisema Makalla.



Hii ni awamu ya Pili kwa mwaka huu wa fedha kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoa mafunzo kwa watumishi wake ikiamini kwamba asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu.



 


Tanzania imeweka wazi mikakati yake mikubwa ya muda mrefu ambapo inalenga kuwa mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika na kuingia kwenye orodha ya nchi 10 bora duniani kwa uzalishaji wa chakula ifikapo mwaka 2050.


Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati akitoa mada kuu kwenye mjadala kuhusu Mustakabali wa Kilimo barani Afrika katika Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue) unaoendelea jijini Des Moines, Marekani.


Mambo Makuu Yaliyobainishwa na Waziri Mkuu:
  • Ongezeko la Bajeti: Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kwa kasi kubwa kutoka shilingi bilioni 294 (2021/2022) hadi kufikia shilingi trilioni 1.241 katika mwaka wa fedha wa 2025/2026.
  • Utoshelevu wa Chakula: Kutokana na uwekezaji huo, Tanzania imefikia utoshelevu wa chakula kwa asilimia 130, jambo linaloifanya nchi kuwa na ziada kwa ajili ya soko la kikanda na kimataifa.

  • Kukua kwa Mauzo ya Nje: Mauzo ya nje ya mazao ya kilimo yameongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 2.1 (2021/2022) hadi kufikia dola bilioni 3.7 (2024/2025).
  • Mhimili wa Uchumi: Kilimo kinachangia asilimia 24.6 ya Pato la Taifa (GDP), kinaajiri asilimia 65 ya nguvu kazi nchini, na kinazalisha takriban asilimia 30 ya mapato ya mauzo ya nje.


Katika mjadala huo, wadau mbalimbali akiwemo Mwanzilishi na Mhariri Mkuu wa Jarida la Chakula la Afrika, Prof. Ruth Oniang’o, wameipongeza Tanzania kwa hatua kubwa inayopiga, hususan kupitia programu bunifu kama 'Jenga Kesho Bora' (BBT), uboreshaji wa miundombinu, na ufanisi wa maafisa ugani.




Waziri Mkuu ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuwekeza kwa wakulima, vijana, wanawake, na kwenye sayansi ili kujenga mifumo thabiti ya chakula kabla njaa haijatushinda.

 




DAR ES SALAAM, Tanzania — Regional industry leaders and policymakers have called for predictable trade policies, affordable industrial finance, and urgent structural reforms to strengthen manufacturing and value addition across the East African Community (EAC).
The call was made during a two-day Public–Private Dialogue (PPD) co-hosted by the East African Business Council (EABC) and the African Development Bank (AfDB). The forum brought together 65 representatives from regional governments, the EAC Secretariat, manufacturers, and development partners to address systemic constraints affecting industrial competitiveness in the leather, textiles, and edible oils sectors.
The Resource-Manufacturing Deficit




Opening remarks delivered on behalf of EABC Executive Director, Ahmed Farah, highlighted a severe mismatch between East Africa's abundant natural resources and its actual industrial performance. According to trade data from 2025, the region remains heavily reliant on costly foreign imports to meet local demand:
  • The Leather Sector: Despite producing approximately 370,000 tonnes of hides and skins annually, the EAC imported US$566 million in footwear and leather goods in 2025. Conversely, regional exports of raw and semi-processed leather stood at just US$46 million.
  • The Textile Sector: Only 37% of the region’s 119,000 tonnes of cotton lint is spun locally. This drove textile and apparel imports to US$3.24 billion in 2025, vastly overshadowing the US$970 million generated from exports.
  • The Edible Oils Sector: Local production covers a mere 37% of regional consumption. As a result, the EAC spent US$3.1 billion on edible oil imports in 2025, while exports stood at US$1.2 billion.
Pervasive Capacity Underutilization
A Growth Diagnostic and Competitiveness Study presented by Dr. Onesmos Shuma of the Excellon Group revealed that policy inconsistencies and structural barriers are crippling factory output. The study found that 79% of surveyed firms operate below 75% of their production capacity, while 67% have been forced to delay or cancel investments. Furthermore, 78% of businesses face technological gaps, even though 76% believe they could source more raw materials locally within the EAC.
The sector-specific breakdown of factories operating below 75% capacity includes:
  • Leather and Footwear: 86% of firms (with 79% postponing investments).
  • Edible Oils: 75% of firms (with 59% postponing investments).
  • Textiles and Apparel: 74% of firms (with 61% postponing investments).
The study identified six core bottlenecks choking industrial growth: restricted access to raw materials, lack of production-cycle finance, technology deficiencies, weak buyer-supplier linkages, skill gaps, and high trade operating costs.
Calls for Harmonized Trade Instruments
Industry experts stressed that regional trade mechanisms must operate as a single, coherent system rather than a fragmented network. Dr. Margaret Chemengich of Charmy Investments pointed out that 25 out of 39 "stays of application" affecting these value chains have been repeatedly renewed in every national budget since the 2022/23 financial year, disrupting market stability. Discrepancies also persist in tariffs; for example, the applied duty on refined sunflower oil ranges from 26% in Tanzania to a steep 60% in Uganda.


Frank Dafa, Executive Director of the Confederation of Tanzania Industries (CTI), alongside other regional panellists, emphasized the need to link agriculture and livestock directly to manufacturing through tighter vertical integration. They urged the private sector to back their policy proposals with hard evidence regarding production capacity, market demand, and employment impact to facilitate data-driven policy reviews.
Commercially Viable Solutions


The Chief Guest, Amedeus Arbogast Mzee from Tanzania’s Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, concluded that the region must move toward commercially viable solutions backed by clear timelines and measurable outcomes.


Delegates ultimately recommended a framework of priority actions focused on stabilizing raw material supply chains, introducing flexible value-chain financing, upgrading shared environmental and testing infrastructure, and standardizing conformity assessments to reduce cross-border business friction. Progress will be rigorously monitored through key performance indicators, including regional sourcing volumes, compliance costs, and overall industrial capacity utilization.

 


Na Mwandishu Wetu


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuimarisha uwezo wa nchi katika kujiandaa na kukabiliana na maafa kwa kutoa mafunzo kwa Timu ya Taifa ya Kukabiliana na Dharura, inayolenga kuongeza ufanisi wa uratibu na utekelezaji wa hatua za kukabiliana na matukio ya dharura.



Hayo yameelezwa leo tarehe 22 Oktoba, 2026, jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maudhui ya Ndani, Condrad Millinga, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu wakati akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Jim James Yonazi.


Milinga amesema, mafunzo kwa timu hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha mfumo wa usimamizi wa maafa nchini, hususan katika kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa, taarifa sahihi zinapatikana na tathmini za madhara zinafanyika kwa wakati ili kuokoa maisha, kulinda mali na kupunguza athari kwa jamii.



“Timu hii ina majukumu mbalimbali, yakiwemo kushiriki katika operesheni za kukabiliana na maafa, kufanya tathmini za awali ili kubaini hatua za haraka zinazopaswa kuchukuliwa pamoja na kushauri kuhusu mahitaji ya ziada ya rasilimali pale inapohitajika” amesema Bw. Milinga.


Aidha, ameitaka timu hiyo kushiriki katika tathmini za kina za uharibifu na mahitaji yanayotokana na maafa ili kubaini mahitaji ya muda mfupi, wa kati na mrefu kwa maeneo yaliyoathirika.


Ametaja majukumu mengine ya Kamati hiyo ni kutoa ushauri kwa Kamati ya Wataalam ya Kitaifa ya Usimamizi wa Maafa kuhusu mikakati bora ya kukabiliana na maafa, kuunganisha kongani za kukabiliana na maafa na kushiriki katika mafunzo mbalimbali yanayolenga kuongeza ujuzi na uwezo wa wadau wa kukabiliana na dharura.



Aidha timu hiyo, itashiriki katika kutafuta rasilimali muhimu kwa ajili ya operesheni za dharura na kushirikiana na Idara husika katika kuandaa mipango ya kukabiliana na matukio ya dharura yanapotokea.


Kwa mujibu wa Millinga, hatua hiyo italenga kuimarisha utayari wa nchi katika kukabiliana na maafa kwa kuhakikisha kuwa maamuzi yanayofanywa yanazingatia taarifa sahihi, tathmini za kitaalam na mahitaji halisi ya maeneo yaliyoathirika.


Pia amewasisistiza wajumbe wa Timu ya Taifa ya Kukabiliana na Dharura kufanya kazi kwa ukaribu na Idara ya Menejimenti ya Maafa, chini ya uratibu wa Kituo cha Taifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura.


Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye ulemavu) Brigedia Jenerali Hosea  Ndagala amesema, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wajumbe wa Timu uelewa wa pamoja, taratibu za utendaji na namna ya kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao.  


Pia yanalenga kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kati ya wajumbe wa Timu ya Taifa ya Kukabiliana na Dharura na Idara ya Menejimenti ya Maafa ili kuhakikisha kuwa taarifa, tathmini na hatua zinazohitajika wakati wa dharura vinapangwa na kuratibiwa kwa ufanisi.

 


Waziri wa Madini wa Tanzania, Anthony Mavunde, ametoa wito mzito wa kutaka nchi za Afrika kuacha kuwa chanzo cha malighafi kwa viwanda vya nje na badala yake kutumia utajiri wake kujenga viwanda vya ndani, kuongeza ajira, na kukuza uchumi. Msimamo huo ameuwasilisha Oktoba 21, 2026, jijini Accra, Ghana, wakati wa kikao cha pande mbili kati yake na Waziri wa Ardhi na Maliasili wa Ghana, Emmanuel Armah-Kofi Buah.


Viongozi hao wamejadili fursa za kipekee za kuimarisha usimamizi na maendeleo ya Sekta ya Madini kwa manufaa ya nchi zote mbili. Katika kikao hicho, mambo makuu yafuatayo yamejadiliwa kama nguzo za ushirikiano:


  • Uwezeshaji wa Wachimbaji Wadogo: Kuangalia wachimbaji wadogo kwa jicho la uwezeshaji ili wachangie kikamilifu kwenye uchumi badala ya kufanya kazi kwa kujitenga.
  • Komesho la Kusafirisha Madini Ghafi: Kusitisha tabia ya kusafirisha madini ya kimkakati kama dhahabu, shaba, grafiti, na lithiamu kwenda nje bila uongezaji thamani (kuyeyusha, kusafisha, na kuchakata) ndani ya Afrika.
  • Utafiti wa Kijiolojia: Kubadilishana utaalamu, teknolojia, na taarifa za kijiolojia ili kuimarisha uwezo wa kutambua rasilimali na kujadili mikataba ya uwekezaji kwa kujiamini zaidi.
  • Ushiriki wa Wazawa (Local Content): Kuhakikisha wananchi wanakuwa wamiliki wa biashara, wawekezaji, na wasambazaji wa huduma migodini badala ya kubaki kama wafanyakazi pekee.
  • Mikataba ya Maendeleo ya Jamii: Kujifunza kutoka Ghana namna mikataba inavyohakikisha jamii zinazozunguka migodi zinashiriki na kunufaika moja kwa moja na matokeo ya uwekezaji.


  • Mwaliko wa Kitaalamu: Anthony Mavunde amemwalika Waziri wa Ghana kutembelea Tanzania katika miezi ijayo ili kuanzisha vikundi kazi vya kitaalamu vya pamoja (joint technical working groups).


Huku dunia ikielekea kwenye nishati safi na teknolojia mpya zinazohitaji madini mkakati, ushirikiano huu wa Tanzania na Ghana unaenda kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika.