Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts

 


Na Queen Lema, Arusha

 

MKOA wa Arusha unatarajiwa kusimama miguu yote miwili kesho Agosti Mosi, wakati Princess Lounge, moja ya kumbi maarufu na zenye mvuto mkubwa wa kipekee barani Afrika Mashariki, itakapofanya maadhimisho makubwa ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.


 Akizungumza kuelekea tukio hilo la kihistoria, Mkurugenzi wa Princess Lounge, Catherine Urasa, amesema wameandaa sherehe kubwa na ya kukata na shoka itakayoweka historia mpya ya burudani mkoani Arusha.

Catherine amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwake, Princess imekuwa nguzo kuu na kichocheo kikubwa cha sekta ya burudani, huku ikisifika kwa kulisha vyema hisia za wapenda bata na starehe mkoani hapa.

Alieleza kuwa kwa kuzingatia Arusha ni kitovu cha utalii nchini, Princess Lounge imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenda sambamba na hadhi hiyo kwa kutoa burudani na huduma za kiwango cha kimataifa zinazovutia wageni wa ndani na nje ya nchi.


"Tunatimiza mwaka mmoja sasa wenye mafanikio makubwa sana. Tunafurahi kwa upendo na mapokezi tuliyopata, na tunapenda kuwaahidi wateja wetu kuwa tumejipanga vyema zaidi kuendeleza na kuiboresha sekta hii ya burudani kwa viwango vya juu zaidi," alisema kwa kujiamini Catherine.


Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo amejivunia namna biashara hiyo ilivyoweza kuwa mkombozi kwa vijana kwa kutengeneza fursa za ajira kwa wale ambao hapo awali hawakuwa na kazi kabisa.


"Kama mnavyojionea wenyewe, hapa tuna mabinti warembo na wachapakazi ambao ni sehemu ya nembo yetu. Pia tuna vijana mahiri wa muziki (DJs) na wataalamu wa kuchoma nyama tamu na zenye ladha ya kipekee, ambao wote kwa pamoja ndio siri na nguzo ya mafanikio ya Princess," aliongeza.


Kufuatia hatua hiyo, Catherine ametoa wito na mwaliko rasmi kwa Watanzania wote na wakazi wa jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi kesho kusherehekea kwa pamoja mafanikio hayo, ambapo kutakuwa na mfululizo wa burudani za kusisimua, vinywaji vya kila aina, na vyakula vya kutosha.

 


Tuzo za muziki za Trace Afrika, zilizofanyika kwa mara ya kwanza Visiwani Zanzibar, Tanzania, usiku wa kuamkia leo, zilikatizwa ghafla baada ya maji kujaa karibu na jukwaa, hali iliyosababisha sintofahamu kwa mashabiki na wageni waalikwa.


Tamasha hilo lilianza kwa kuchelewa kutokana na upepo mkali na mawimbi, na waandaaji walilazimika kusogeza muda wa kuanza hadi saa 4 usiku. Msanii wa Tanzania, Marioo, alikuwa wa kwanza kutumbuiza kabla ya wasanii wengine kuendelea na burudani. Hata hivyo, shughuli hiyo ilikatizwa ghafla mnamo saa 9:20 usiku, ikiwa bado katika hatua za mwanzo za kutangaza washindi wa tuzo hizo.

Ingawa sababu rasmi haikutangazwa jukwaani, tukio hilo lilizua minong’ono na malalamiko kutoka kwa waliohudhuria. Kabla ya kusitishwa, msanii Rema kutoka Nigeria alitangazwa kuwa Msanii Bora wa Kiume wa Mwaka na pia kushinda Tuzo ya Albamu Bora kupitia albamu yake Heis.


Tuzo zingine zilimwendea P. Prime kutoka Nigeria kama Mtayarishaji Bora wa Muziki, Josey kutoka Ivory Coast kama Msanii Bora wa Nchi zinazozungumza Kifaransa, Joe Dwet File (Ufaransa/Haiti) kama Msanii Bora wa Diaspora, na Duquesa kutoka Brazil.


Licha ya changamoto hiyo, tamasha hilo lilishuhudia burudani ya nguvu kutoka kwa wasanii wakubwa wa Afrika, akiwemo Diamond Platnumz wa Tanzania, Harmonize, na Bien wa Kenya.

 



Dar es Salaam, Februari 22, 2025 - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo za Komedi iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki, Jijini Dar es Salaam. 



Rais Samia alishiriki katika tukio hilo kwa lengo la kutambua na kuhamasisha sanaa ya ucheshi nchini.


Katika hafla hiyo, Rais Samia alipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na washindi wa tuzo mbalimbali, ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wao katika sekta ya burudani na sanaa ya ucheshi.



Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia alisema, "Sanaa ya ucheshi ni moja ya sekta muhimu katika kukuza vipaji na kutoa ajira kwa vijana wetu. Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wasanii wa ucheshi ili kuhakikisha wanapata mazingira bora ya kufanya kazi zao."

Mmoja wa washindi wa tuzo hizo, mchekeshaji maarufu nchini, alieleza furaha yake kwa kutambuliwa katika jukwaa hilo muhimu.

"Kushinda tuzo hii ni heshima kubwa kwangu na kwa wachekeshaji wote. Tunashukuru kwa kutambuliwa na kwa sapoti tunayopata kutoka kwa viongozi wetu," alisema mshindi huyo.

Mratibu wa tuzo hizo alieleza kuwa lengo la tukio hilo ni kuinua sekta ya ucheshi na kuwaweka pamoja wachekeshaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

"Tumeandaa tuzo hizi ili kuonyesha thamani ya sanaa ya ucheshi na kuhamasisha vipaji vipya. Tunaamini kuwa kupitia matukio kama haya, wasanii wa ucheshi wataendelea kupata nafasi zaidi kwenye sekta ya burudani," alisema mratibu huyo.

Hafla hiyo iliendelea kwa burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa vichekesho na muziki, huku washiriki wakipata fursa ya kufurahia vipaji vya wachekeshaji wa ndani na nje ya nchi. Tukio hilo liliashiria hatua kubwa katika kuthamini na kukuza sanaa ya ucheshi nchini Tanzania.

 

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa, amewataka  wasanii na watengenezaji wa Tamthilia ya HUBA inayorushwa na DStv kuutangaza utamaduni wa Tanzania duniani ili wageni wengi watembelee nchi hiyo.

Amesema hayo leo Februari 12, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akiagana na kundi hilo lililoondoka kwenda  nchini Dubai kuandaa kazi zao.


Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuona filamu za Tanzania zinakuwa na ushindani katika  soko la kimataifa.



Katika tukio hilo  Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa wizara Dkt. Hassan Abbasi na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo ambao wote walizawadiwa  vyeti vya shukrani kwa  kutambua mchango wao kwenye tasnia ya Filamu.

 




Kundi la wanamuziki wa Hiphop la Weusi litakiwasha jijini Arusha siku ya Eid Mosi kwenye ukumbi wa Cocoriko Kijenge.


 Mkurugenzi wa Cocoriko Club, John Mdenye, amewaeleza waandishi wa habari leo kuwa tayari maandalizi yamekamilika. 

"Kesho tutakuwa na shoo kubwa, kundi zima la Weusi watakuwa hapa. Shoo hii tumeiandaa vizuri kweli na wasanii wote wa Arusha watakuwa hapa,"

"Tutakuwa na wasanii wengine wa bendi yetu kama Michael Jackson na wengine hivyo nawakaribisha wananchi wote wa Arusha wanaopenda burudani waje kusherekea sikukuu za Eid.,"

"Kuanzia mchana tutakuwa na burudani mbalimbali, tutakuwa na chakula na vinywaji waje wale wanywe wafurahi pamoja na familia zao,". 

Mdenye amesema kiingilio wakati wa usiku kitakuwa shilingi 10,000 kwa eneo la kawaida na  VIP wameandaa vizuri kwa watu special watalipa 15,000  kwa hiyo akawakaribisha sana wapenda birudani, wote kufika na kupata burudani.
  
"Shoo hii haijawahi kufanyika sehemu yoyote hapa Arusha. Kama mnavyojua Weusi ni watoto wetu wa huku Arushahivyo shoo hiii tumeiandaa kwa staili kitofauti ambayo wateja wetu na wapenzi wa Weusi watafurahia shoo hii," amesema.


Shabiki wa Weusi, Kolumba Mbabaz amesema kuwa Weusi wameamua kuiheshimisha Arusha kwani kwa sasa wana albam yao ya Air Weusi ambapo hii ni shoo yao ya kwanza jijini hapa tokea waachie albam hiyo.

"Arusha sasa ni halisi kutokana na hali ya hewa ya baridi na mvua za hapa na pale hivyo Weusi tumewapa jukumu moja siku ya Eid Mosi yaani wafanye shoo watu wajisahau  kama wako kwenye Arusha ya baridi," amesema Kolumba.

Amesema nyimbo za weusi zinaweza kusikilizwa na watu wa rika zote kwani zimezingatia maadili hivyo wazazi wanaweza kufika wa watoto wao Cocoriko na wakaondoka wakiwa wamesuuzika roho zao kutokana na burudani watakazopatiwa

 

Kundi la Hiphop la Weusi linaundwa na Joh Makini, Lord Eyez, Nikki Wapili na Gnako Werawera ambapo wana zaidi ya miaka mitatu tokea wafanye shoo jijini hapa.



Wasanii hao ambao ni wenyeji wa Arusha wanaoendesha shughuli zao za kumuziki jijini Dar es Salaam hivi karibuni wameachia rasmi albamu yao  mpya kwa jina 'Air Weusi'.

Ina nyimbo 14 na mbili tu ndiyo za ambapo walioshirokishwa ni Khadoja Kopa na Big Boso J.O.J. O.




Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ameahidi kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuboresha mifumo ya hakimiliki ili kuhakikisha wasanii wa mawanda mbalimbali wananufaika kila kazi zao za ubunifu zinapotumika iwe kwenye redio, TV, mitandaoni na kila sehemu ya biashara.




Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo jioni hii jijini Dar es Salaam alipokutana na waandaaji wa muziki na filamu, Madj na wasambazaji wa kazi za sanaa ikiwa ni mikakati ya pamoja ya kutatua kero za sekta hiyo.

"Tangu Cosota ihamie Wizara ya Habari tumeendelea kuboresha mifumo ya ndani ya kiutendaji ikiwemo kuandaa mifumo mipya ya kimtandao kusajili kazi kiurahisi, kuboresha Kanuni ili wanaokamatwa na kazi za wasanii watozwe faini papo hapo na zaidi tumeiongezea taasisi wafanyakazi na vitendeakazi hasa usafiri na hivi sasa tayari Cosota imeshafungua Ofisi Dodoma. Wasanii wakae tayari kunufaika na mifumo bora zaidi ya kukusanya haki zao," alisema Dkt. Abbasi.

Katika mikutano hiyo wadau wa sekta ya Sanaa pia wameomba kujengewa kumbi za maonesho na burudani na kupunguziwa utitiri wa kodi ambazo Katibu Mkuu Dkt. Abbasi amewataka waainishe kodi zenye kero ili zijengewe hoja Serikali.


 

 


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali leo Novemba 30, 2020, jijini Dar es Salaam, ameanza ziara ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo zinazoratibu masuala ya sanaa nchini.

Dkt. Abbasi ameelekeza taasisi hizo kuwa kiungo kati ya wadau wa sanaa na Serikali na amezitaka ziwe karibu na wadau hao, ziwahudumie kwa karibu na zaidi zibuni mambo mapya ya kuishauri Serikali katika kutekeleza azma ya kuiinua sekta ya sanaa nchini. 

"Serikali imeahidi kuinua sekta ya sanaa na dhamira kubwa ipo; ni juu yenu kushirikisha wadau ili kupata mrejesho sekta inataka kufanyiwa nini na Serikali ili ikue; zama za wanatasnia na taasisi za sanaa kuwa mbali na kila mmoja anakwenda na lake zimekwisha," alisema Dkt. Abbasi.


MUIGIZAJI  na mchekeshaji maarufu bongo Steven Nyerere, amesema anatamani kukutana na Rais Magufuli amshauri azime data, ili watu wasitumie mitandao ya kijamii kwa kufanya umbea na kuongea habari za uongo za kuchafuana.

Akizungumza na www.eatv.tv, Steve Nyerere amesema iwapo atapata fursa hiyo atamsahuri Rais Magufuli kufuata wanachokifanya China, ambapo wao wamepiga marufuku utumiaji wa mitandao ya kijamii mbali mbali, na kutumia mitandao mingine ya kwao kwa ajili ya kukuza uchumi wao na sio kwa ajili ya kupiga umbea na kueneza habari za uongo.

“Bado tunahitaji kuwa na mwenendo wa China, nitafurahi sana siku Magufuli akizima data, na nadhani kuna haja ya kumshauri Mheshimiwa Rais, kwa sababu kama tunataka kujenga Tanzania ya viwanda, ni lazima siku moja tuzime data hata mwezi nadhani tutafikia malengo, tena andika kabisa Nyerere anatamani kuonana na Magufuli amnong'oneze kuhusu data, azime tu hata nwezi, ili watu wafanye kazi, amesema Steve Nyerere.

Steve ameendelea kwa kusema kwamba ….. “asilimia 90 wanaishi kwenye mitandao na kubuni vitu ambavyo haviingizi taifa hata pato, nia ni kuliongezea taifa pato, wenzetu China wameendelea kutokana kutoipa nafasi mitandao kuihairbu China yao, wameipa nafasi kwa ajili ya kutangaza biashara na utalii, sasa sisi tumeipa nafasi kwa jili ya umbea”,.

Steve Nyerere ametoa kauli hizo zote kutokana na watu kuzusha taarifa kuwa mke wake amemkimbia, baada ya kugundua amezaa nje ya ndoa na muigizaji Welu Sengo.


MUIMBAJI mwenye mbwembwe nyingi, Gigy Money amewashukia watu wanaomsema mitandaoni juu ya uamuzi wake wa kutoka kwenda kufanya kazi kabla ya arobaini ya mtoto wake.
amesema  atafanya chochotee kwa ajili ya mtoto wake ambapo akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram
>>>“Ogopa sana mapenzi ya mama na mtoto yani Mama anaweza kujikuta anafanya lolote kwa ajili ya kesho ya mwanae ata awe chizi hawezi kumtupa mwanae haijalishi wakati wa mimba mangapi yamepita nachowaza saivi ni binti yangu tu ataaa kudanga ntadanga npo serious mjue nawale ambao mnanitukana kwann kipindi hiki nafanya kazi natoka kabla ya 40 Naomba”
“Niwajibu kiufupi kama mkubwa utaelewa kama mtoto endelea kunijazia comments za matusi yaaani ni iviii (utamaduni wa mtanzania ni njaaa ukiwa na njaaa unaweza fanya lolote sidhani kama ningekua napewa kila kitu ningetoka tu) so usilaumu kitabu tu kwasabu juu umeona fuvu ukajua iko kitabu kinahusu mazombie …. kisome kwanza. Ndio uogope Muwe na siku njema” – Gigy Money

Msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiondoka katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kutumikia adhabu yake ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika ofisi hizo zilizopo eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo. Lulu atatumikia kifungo hicho mpaka novemba 12 mwaka huu. Picha na Ericky Boniphace  
Huyo ni Elizabeth Michael, ambaye ameanza maisha mapya ya kifungo cha nje katika Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Jumatatu wiki hii.
Ametimiza siku ya tatu tangu aanze kutumikia jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani. Ameshatimiza saa 12 kati ya saa 512 anazodaiwa mpaka atakapomaliza kifungo hicho cha nje Novemba 12, mwaka huu.
Msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiondoka katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kutumikia adhabu yake ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika ofisi hizo zilizopo eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo. Lulu atatumikia kifungo hicho mpaka novemba 12 mwaka huu. Picha na Ericky Boniphace  
Mmoja wa wafanyakazi wa usafi kutoka kampuni binafsi katika wizara hiyo, anasema kuwa Elizabeth maarufu zaidi kwa jina la Lulu amekuwa akifika wizarani hapo saa 12 asubuhi na huondoka kati ya saa 4:00 mpaka 4:30 asubuhi.
“Mfano jana (Jumanne) aliondoka saa nne na nusu, leo (Jumatano) kaondoka kama ulivyomuona mwenyewe (saa 4:15 asubuhi).
Msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiondoka katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kutumikia adhabu yake ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika ofisi hizo zilizopo eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo. Lulu atatumikia kifungo hicho mpaka novemba 12 mwaka huu. Picha na Ericky Boniphace  
Amesema kuwa Lulu huletwa na gari binafsi saa 12 asubuhi na tangu aanze kazi za kufagia na kudeki pamoja na usafi mwingine kwa ujumla amekuwa akifanya kazi hizo kwenye ghorofa ya nne ya wizara hiyo.
Lulu ambaye alihukumiwa miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Steven Kanumba amebadilishiwa adhabu na tangu Jumatatu anatumikia kifungo cha nje.
Gari lililombeba msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael likiondoka eneo zilipo ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anthony Siame

Source Mwananchi

MASKINI! Mwanamama mkongwe wa filamu za Kibongo, Illuminata Poshi ‘Dotnata’, amepata pigo baada ya kufiwa na mama yake mzazi, Ildegalda Alphonce aliyefariki dunia juzi, Jumatatu, asubuhi katika Hospitali ya Boch, Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Dotnata alisema kuwa, kifo cha mama yake kimeacha pengo kubwa katika familia kwani kama mzazi, alikuwa na umuhimu mkubwa kwao, lakini ndiyo mapenzi ya Mungu hawawezi kuyapinga.
“Kufiwa na mama siyo jambo dogo, ni kubwa mno, mama yetu ametuachia pengo kubwa na tutamkumbuka sana kwa mengi, ameugua kansa (hakupenda kutaja ya nini) kwa muda mrefu na ameteseka sana kwa kweli ndipo Mungu akaamua kumpumzisha. Tunaumia sana, lakini inabidi tukubaliane na kilichotokea maana kila nafsi lazima itaonja mauti. Tulimpenda mama yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema Dotnata huku akilia kwa uchungu.
Mwili wa mama wa Dotnata ulitarajiwa kusafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera, lakini mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni walikuwa hawajapanga siku ya kuusafirisha na msiba upo nyumbani kwa dada yake Dotnata, Segerea, Dar. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.  Amen!
Source motomoto news





2017 zimefanyika Cover ya nyimbo nyingi sana na wasanii wengi pia ila hii ya Raymond RayVanny imekuwa lazima iongoze. 
Usisahau Tuzo za Uganda Entertainment RayVanny ameshinda kwa kishindo cha aina yake baada ya kuwagaragaza Wizkid,Davido.. Play hii video hapa chini.

Diamond Platnumz

US Dollar Millioni 4.1 ni kiasi cha Fedha zinazokadiriwa kuwa analipwa msanii wa Marekani RickRoss na Kampuni ya Vinywaji vikali 
Luc Belaire ya nchini ufaransa. 


Siku moja iliyopita Kampuni hiyo ilimtangaza mshirika wake mpya msanii nyota wa Afrika staa wa wimbo wa 'Eneka' Diamond Platnumz.

Ambapo kwa maana hiyo Diamond anaungana na Mastaa wengine wakubwa wa dunia akiwemo RickRoss ambaye anadaiwa kuwa na hisa kubwa katika Kampuni hiyo.


Diamond Platnumz

Swali linalo vuma kwa sasa ni kwamba Je! Diamond Platnumz analipwa kiasi gani cha Fedha baada ya kuingia mkataba mkubwa na Kampuni hiyo ya Ufaransa? 

Je atalipwa Sawa na RickRoss ambaye anaingiza kiasi cha dollar za Marekani Millioni 4.1 Sawa na zaidi ya Tsh. Billioni 8 !!