Showing posts with label SHERIA. Show all posts
Showing posts with label SHERIA. Show all posts

 

Happy Lazaro, Arusha.

Serikali imeweka bayana kuwa mafanikio ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yatategemea kwa kiwango kikubwa mchango wa Mawakili wa Serikali, hususan katika kusimamia masuala ya kisheria yanayohusu miradi mikubwa ya maendeleo na uwekezaji.



Akifunga mafunzo maalumu ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali yaliyofanyika jijini Arusha, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Zainab Katimba, amesema wakati umefika kwa mawakili hao kuwa zaidi ya washauri wa sheria na kuwa wadau muhimu wa maendeleo ya Taifa kupitia utaalamu wao.



Ameeleza kuwa mafunzo hayo yamekusudiwa kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto mpya zinazojitokeza katika mazingira ya utawala na uchumi, huku akiwataka kutumia maarifa waliyoyapata kuboresha usimamizi wa mikataba, utoaji wa ushauri wa kisheria na utatuzi wa migogoro kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi.



Kwa mujibu wa Katimba, Serikali inahitaji wataalamu wa sheria wanaoweza kufanya uchambuzi wa kina, kufikiri kimkakati na kuhakikisha kila mkataba au uamuzi wa kisheria unalinda rasilimali za Taifa na kuchangia ukuaji wa uchumi.



Amesema anaamini washiriki wa mafunzo hayo watakuwa chachu ya mabadiliko katika taasisi wanazotoka na wataongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao, hatua itakayosaidia kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.



Naye Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Samwel M. Maneno, amesema programu hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya taaluma ya sheria, ikijumuisha mada kuhusu mikataba ya kimkakati, ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), usimamizi wa vihatarishi vya kisheria, usuluhishi wa migogoro pamoja na matumizi ya Akili Unde (AI) katika utoaji wa huduma za kisheria.



Aidha, amewataka  Mawakili wa Serikali kuendelea kuyafanyia kazi maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kuongeza ubora wa utendaji wa taaluma ya sheria, ikiwa ni pamoja na kusoma na kuyatumia mafunzo yaliyomo katika kitabu Mama Samia Doctrine of Law ili kuimarisha uchambuzi wa masuala ya kisheria na usimamizi wa mikataba ya Serikali.



Mafunzo hayo ya Bespoke 2026, yaliyobeba kaulimbiu "Repositioning State Attorneys for Strategic Legal Leadership in Realizing Tanzania Development Vision 2050," yaliwakutanisha Mawakili wa Serikali kutoka wizara, taasisi, wakala na mamlaka za serikali za mitaa kwa lengo la kuongeza ufanisi wa uongozi wa kisheria katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya Taifa.



 



Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeiomba serikali kuwapatia magari saba kwa ajili ya kanda zake saba ili kuimarisha utoaji wa huduma za msaada wa kisheria katika maeneo ya pembezoni mwa nchi.



Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama hicho, Rais wa TLS Boniface Mwabukusi alisema kuwa kuna changamoto kubwa ya miundombinu inayokwamisha mawakili kufika maeneo ya mbali ambako wananchi wanahitaji msaada wa kisheria.

"Tulikuwa tunaomba serikali ione umuhimu wa kuipatia TLS magari saba kwa ajili ya hizo kanda ili kutekeleza wajibu ilio nao wa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi, legal aid kwa watu walio pembezoni," alisema Mwabukusi.

Aliongeza kuwa chama hicho kinatambua wajibu wake wa kuimarisha utawala wa sheria kwa uaminifu, upendo na utii kwa mamlaka, na kusisitiza kuwa hawana maslahi binafsi bali wanalinda maslahi ya Taifa.

"Tunapotekeleza wajibu wetu watu watuvumilie kwa sababu hatuna maslahi binafsi ila ulinzi wa Taifa letu kwa uaminifu," alisema.



Katika hotuba yake, Mwabukusi alielezea kusikitishwa kwake na baadhi ya watu wanaozuia wananchi kwenda mahakamani, akieleza kuwa ni haki ya msingi kwa kila mtu kusikilizwa na kuona mifumo ya haki inavyofanya kazi.

"Juzi nimeona watu wanaenda mahakamani limekuwa zoezi la kivita, nimeona cinema za akina Amita Bachan... watu wanaeuka kuzuia watu wasiende mahakamani. Kwenda mahakamani ni haki, watu waende wakasikie, wakaone haki ikitendeka," alisema.

Aidha, TLS kimeishauri serikali kuanzisha chombo maalum cha kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi hususani yanayohusu haki za binadamu na utawala bora, kikisema kuwa chombo hicho kinapaswa kuwa na mamlaka kamili na uwezo wa kutoa maelekezo yenye uzito kama amri za mahakama.



Akizungumzia masuala ya Utawala Bora na Katiba Mwabukusi amesema, "Kumekithiri vitendo vya Utekaji na kupotea kwa watu TLS inatoa Rai kwa kuundwa kwa chombo huru kinachoweza kusimamia Law enforcement Agency, Uwezi kupeleka police kesi inayowahusu waichunguze wenyewe,".


Mkutano huo wa mwaka wa TLS umeongozwa na kauli mbiu isemayo "Uchaguzi na utawala wa sheria: wito wa uangalizi wa kisheria na uwajibikaji katika mfumo wa uchaguzi wa Tanzania."

Akielezea kauli mbiu hiyo, Mwabukusi alisema: "Kauli mbiu hii inasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa misingi ya utawala wa kisheria inazingatiwa katika kila hatua ya mchakato wa uchaguzi kuanzia maandalizi, upigaji kura hadi utoaji wa matokeo."



Kwa upande wake, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Boniface Simbachawene, alipongeza TLS kwa mchango wake katika kuimarisha utawala bora na demokrasia nchini.

"TLS ni muhimu katika kutoa miongozo ya kisheria na kuhamasisha demokrasia," alisema Simbachawene.



Aliongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TLS katika juhudi za kuboresha mifumo ya kisheria na utawala bora, huku akisisitiza kuwa mabadiliko ya kikatiba na kisiasa yanapaswa kuzingatia maoni ya wananchi.




 


Timu ya watoa huduma wa msaada wa Kisheria kupitia kampeni ya "Samia Legal Aid Campaign" imeagizwa kuorodhesha majina ya watumishi wa serikali katika sekta mbalimbali watakaobainika kutajwa na wananchi kuwa wanachochea migogoro inayopelekea wananchi kuichukia Serikali.



Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, wakati akiongea na wataalam wa sheria wakiwemo mawakili, maofisa maendeleo ya jamii pamoja na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali waliokutana kwa ajili ya kupanga mikakati ya utatuzi wa changamoto za wananchi katika halmashauri saba za Mkoa wa Arusha pamoja na kuainisha changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi katika kila idara husika.


Makonda alisema, "Kuna baadhi ya maofisa maendeleo ya jamii wanalalamikiwa kwa kupindisha sheria ikiwemo watumishi wengine hivyo katika kampeni hiyo endapo kuna watumishi wanalalamikiwa kukwamisha utatuzi wa migogoro kwa wananchi wakuu wa timu husika kutoka Wizara ya Katiba na Sheria waandike majina yao kisha mwisho wa kampeni hiyo watoe taarifa kwake ili hatua stahiki zichukuliwe."



Aidha, alisisitiza kuwa, "Kuna baadhi ya watumishi wanatajwa na wananchi kutokana na tabia ya kukwamisha mambo tunaomba majina yao, lakini pia naomba timu hizi zianishe changamoto zote zilizoibuka ili kupelekwa mahali husika kama polisi, uhamiaji, idara ya kazi na kwingineko ili hatua stahiki zichukuliwe."



Vilevile, Mkuu huyo wa Mkoa aliwasihi watoa huduma kuhakikisha wanawasilikiliza wananchi wanaofika kwa msaada, akisema, "naomba timu hizi zianishe changamoto zote zilizoibuka ili kupelekwa mahali husika kama polisi, uhamiaji, idara ya kazi na kwingineko ili hatua stahiki zichukuliwe." 


Aliongeza kuwa ni muhimu kwa watoa huduma hawa kujiuliza "nafsini kwao je maamuzi watakayotoa ni sahihi na hakuna upendeleo ili wahusika wapate haki yao kwa mujibu wa changamoto zao."



Kwa upande mwingine, Ester Msambazi, ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, alieleza kuwa kampeni hii ilianza kutekelezwa mwaka 2023 na Mkoa wa Arusha ni wa 23 tangu kampeni hii kuanza. 





Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri kuanza kutoa msaada huu kwa wananchi, akisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha haki inapatikana kwa urahisi.


Uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika Machi 28, 2025 kwenye viwanja vya Ngarenaro, ambapo Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, pamoja na  Makonda watahudhuria. 


Katika uzinduzi huo, huduma na elimu za kisheria zitolewe, ikiwa ni pamoja na huduma kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Polisi, na idara na ofisi mbalimbali za serikali ambazo zitatoa huduma za bure kwa wananchi. Baada ya uzinduzi, timu husika zitakwenda uwandani kuanza kazi rasmi Machi 29, mwaka huu.


Kampeni hii ni muhimu kwa kuhakikisha haki inatolewa kwa wananchi bila vikwazo, na inaonekana kuwa ni hatua muhimu katika kudhibiti tabia za baadhi ya watumishi wa serikali wanaochochea migogoro au kukwamisha haki.


 


Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, imemhukumu mchungaji Daud Nkuba maarufu kwa jina la Komando Mashimo, Nabii Nikaya, (Mchungaji Mashimo) kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili kati ya matatu aliyokuwa akishtakiwa nayo.

Mashimo ametiwa hatiani kwenye mashtaka ya kuingia kwa jinai na kuharibu mali, huku akiachiliwa huru kwenye shtaka la kutishia kwa vurugu.

Mshitakiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka matatu ambapo upande wa Jamhuri umethibitisha makosa mawili dhidi yake na kushindwa kuthibitisha shtaka la kutishia kwa vurugu.

Hukumu hiyo ilitolewa leo Machi 18, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemalila, baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha makosa dhidi ya mshitakiwa bila kuacha shaka yoyote.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Rugemalila alisema, "Nimeridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa Jamhuri na vielelezo, ambapo wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili. Hata hivyo, mshtakiwa ameachiliwa huru kwa shtaka la tatu kwa kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo."

Aidha, alisema, "Mshtakiwa katika kosa la kuingia kwa jinai, mahakama inakupa adhabu ya kwenda jela miezi sita, na kosa la kuharibu mali, mahakama inakutia hatiani na kukupa adhabu ya kwenda jela miaka miwili. Pia, mahakama inakuachia huru kwa kosa la kutishia kwa vurugu kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha shtaka dhidi yako. Hivyo, utatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani."

Kabla ya kusomewa adhabu, mshitakiwa alipata nafasi ya kujitetea, ambapo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa sababu ana familia inayomtegemea.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu, uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kama sheria inavyoelekeza, ili iwe fundisho kwake na kwa jamii nzima.

Awali, ilidaiwa kuwa, Novemba 22, 2023, mchungaji Mashimo alifanya uhalifu katika maeneo ya Mbezi Luis Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, kwa kuingia kwa jinai katika ardhi inayomilikiwa na Frola Mwashaa. Aidha, aliharibu ujenzi wa nyumba iliyokuwa eneo hilo, kinyume cha sheria.

Pia, ilidaiwa kuwa, katika shtaka la tatu, alimtishia Ramson Vicent kwa vurugu.

 


Arusha – Mawaziri wameongeza nguvu katika kampeni ya Mama Samia Legal Aid, ambayo imewanufaisha mamia ya wakazi wa Arusha tangu ilipoanza jijini hapa Machi 1, 2024. 


Kampeni hii ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8, 2025, ambapo Arusha itakuwa mwenyeji.



Akizungumzia mafanikio ya kampeni hiyo, Ndejembi amesema: "Tunashukuru kuona kwamba wananchi wengi wameweza kupata msaada wa kisheria. Hii ni fursa kwao kuelewa haki zao na namna ya kuzilinda."

Wakizungumzia ujio wa mawaziri kuelekea maadhimisho hayo, baadhi ya Mama Lishe wa Mkoa wa Arusha wameeleza kuwa wanathamini juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, ambazo zimewapatia fursa mbalimbali za kiuchumi na uwezeshaji.

"Tumeona mambo mengi mazuri tunayofanyiwa na Rais Samia pamoja na Mkuu wa Mkoa wetu. Kwa kweli, tumefaidika sana na hatuna wasiwasi. Kura zetu ni za Rais Samia kwenye uchaguzi mkuu ujao," amesema mmoja wa Mama Lishe.


Maandalizi ya maadhimisho hayo yanaendelea, huku kampeni ya msaada wa kisheria ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao.

 


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi wa umma ambao wamekuwa chanzo cha migogoro kwa wananchi, hususan migogoro ya ardhi. 


Aidha, ameeleza kuwa kwa muda mrefu, unyanyasaji wa kijinsia umeonekana kama tatizo linalowakumba zaidi wanawake na watoto, lakini sasa hali imeanza kuonyesha sura mpya ambapo wanaume nao wanakumbwa na manyanyaso ya kijinsia. 



Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro, takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 53 ya watu waliopokea msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid ni wanaume, huku wanawake wakiwa asilimia 47.



Akizungumza jijini Arusha katika maonesho ya kuelekea kilele cha Wiki ya Wanawake Duniani, Waziri Ndumbaro alisema kuwa huduma hiyo ya msaada wa kisheria imeshatolewa katika mikoa 22 nchini na bado mikoa tisa. Alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amemtuma kwenda Arusha kushughulika na kero za wananchi, hasa zinazohusiana na migogoro ya ardhi na unyanyasaji wa kijinsia.


"Nimekuja kuweka kambi Arusha pamoja na timu ya wanasheria zaidi ya hamsini kutatua migogoro ya wananchi, na nikimaliza kuongea na nyinyi naanza kusikiliza kero zenu," alisema Ndumbaro.

Alibainisha kuwa serikali inachukua hatua kali dhidi ya watumishi wa umma wanaosababisha mateso kwa wananchi kwa makusudi, hasa wale wanaohusika na dhuluma ya ardhi na ukandamizaji wa haki.

Kero za Wananchi



Baadhi ya wananchi waliotafuta msaada wa kisheria ni pamoja na Padre Gabriel Ole Kilelo, mkazi wa Ngorongoro, ambaye alimweleza Waziri Ndumbaro namna Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro na maofisa wa ardhi walivyohusika katika kumnyang’anya maeneo yake. 


Alidai kuwa Mkurugenzi huyo alimnyang’anya ardhi yake licha ya yeye kutoa sehemu ya eneo lake bure kwa ajili ya huduma za jamii, akamzuia kupata wafadhili, na hata kumyima tenda za halmashauri kupitia shirika lake la Kidupo, linaloshughulika na elimu kwa watoto wa jamii ya kifugaji.

Alisema kuwa chanzo cha mgogoro wake na halmashauri hiyo ni juhudi zake za kuitetea serikali katika kutatua mgogoro wa ardhi katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo, mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 30.



Kutokana na malalamiko hayo, Waziri Ndumbaro aliagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro na maofisa wa ardhi wilayani humo wafike katika banda la Katiba na Sheria siku inayofuata, Februari 5, 2025, kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo.

Mikoa Inayoongoza kwa Changamoto za Kisheria



Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro, mkoa wa Geita umeongoza kwa changamoto nyingi za kisheria. Alisema kuwa kampeni ya Mama Samia Legal Aid imewafikia watu zaidi ya milioni nane kwa njia ya elimu mtandaoni, huku zaidi ya watu milioni mbili wakihudumiwa moja kwa moja tangu mpango huo uanze mwaka 2023.


"Kigoma tuna changamoto ya uraia, huku katika mikoa mingine wananchi wengi waliojitokeza walikuwa na matatizo ya migogoro ya ardhi, mirathi, na unyanyasaji wa kijinsia," alisema Waziri Ndumbaro.


Aidha, alisema kuwa kati ya mikoa 22 iliyohudumiwa, migogoro mingi imehusu ardhi, ambapo wanawake wengi wanadhulumiwa, hasa kwenye mirathi.

"Sheria yetu iko vizuri kabisa, inatambua mchango wa kila mtu kwenye ndoa. Hata mwanamke au mwanaume ambaye hana kazi ana mchango wake. 


Shida kubwa ni pale ambapo mwanaume akifariki, maisha yanaendelea. Lakini mwanamke akifariki, hakuna tatizo. Lakini mwanaume akifariki, wanataka asirithi, wamtimue kwenye nyumba na asirithi mali. Hapo kuna changamoto kubwa sana," alifafanua Waziri Ndumbaro.

Ukandamizaji wa Kijinsia na Ukatili

Akizungumzia unyanyasaji wa kijinsia, Waziri Ndumbaro alisema kuwa katika baadhi ya maeneo, ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa. Alitoa mfano wa ndoa ya utotoni iliyovunjwa mkoani Shinyanga, ambapo msichana aliyekuwa amemaliza elimu ya sekondari alinusuriwa siku ya harusi na kurudishwa shuleni.

"Tulivamia harusini na kumnusuru mtoto ambaye sasa anamaliza kidato cha sita. Hii inaonesha jinsi kampeni hii ilivyo na umuhimu mkubwa kwa jamii yetu," alisema.

Kuhusu adhabu za ukatili wa kijinsia, Waziri alisema kuwa wakati wa ziara yake gerezani, baadhi ya wafungwa walilalamika kuwa adhabu ya miaka 30 kwa makosa ya ubakaji, ulawiti, na unyanyasaji ni kubwa.

"Niliwaambia kuna hoja bungeni, wanataka mkihukumiwa mkahasiwe. Niliwauliza kama wako tayari, wakasema hapana," alisema Waziri Ndumbaro.

Aidha, alisema kuwa suala la dhamana kwa makosa ya ukatili wa kijinsia linapaswa kufanyiwa kazi kwa umakini mkubwa ili kuzuia wahalifu kuendelea kuhatarisha maisha ya waathirika.

"Haya masuala ya makosa ya ukatili wa kijinsia ni makubwa, inabidi tukaze nati. Maoni na hoja za wananchi zifike bungeni ili watu hao wasipewe dhamana kama ilivyo kwa makosa ya utakatishaji wa fedha haramu. Tunaona kwa sasa watu wanaanza kuyaogopa," alisema.

Mpango wa Kuendeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria katika Wizara ya Katiba na Sheria, Esther Msambaza, alisema kuwa mpaka sasa kampeni hiyo imeshafanyika kwenye mikoa 22, na wamebakiza mikoa tisa.

Alisema kuwa lengo la kampeni hiyo lilikuwa kuwafikia wanawake na kuwapa elimu kuhusu haki na wajibu wao katika nyanja mbalimbali, ikiwemo kijamii, kiuchumi, na kisiasa.

"Wanaume wengi wanapojitokeza, migogoro yao inapohusisha familia, hutatuliwa kwa njia ambayo inaleta utulivu kwenye jamii. Hii inaonesha kuwa msaada wa kisheria una athari chanya kwa familia na jamii kwa ujumla," alisema Msambaza.

Aliongeza kuwa serikali inafanya mazungumzo na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ili kuanzisha vituo vya kudumu vya Mama Samia Legal Aid katika mikoa mbalimbali, ili mpango huu uwe endelevu hata baada ya kipindi cha Rais Samia Suluhu Hassan.


"Tunapoondoka kwenye kila mkoa, tunaacha wanasheria wanaoendelea kutoa huduma. Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wanapata msaada wa kisheria kwa muda wote," alisema.


Kwa mujibu wa Waziri Ndumbaro, baada ya kukamilisha mikoa yote, kampeni hiyo itaelekezwa kwa wanamichezo ili kuhakikisha sekta zote zinaguswa na huduma hii muhimu.



Deputy Minister of Constitution and Legal Affairs, Jumanne Sagini, has urged government lawyers to offer timely and appropriate advice to the government and its institutions, including leaders, on how to handle and resolve disputes with citizens or investors without compromising national interests.



Sagini made these remarks while inaugurating a three-day training session for government lawyers, starting on May 20, 2024,  in Arusha.


"In this area, I would like to advise you to be more 'proactive rather than reactive.' When you see signs that our leaders' actions might lead to conflicts in contract execution, do not wait for things to go wrong. You, the government lawyers, are here to preemptively offer advice to prevent situations from deteriorating. Waiting until matters escalate to judicial or arbitration bodies domestically or internationally makes the task more difficult. Early intervention could avert such negative outcomes," said Deputy Minister Sagini.



He also commended the Office of the Solicitor General for its significant achievements, including defending the government in claims and arbitration cases, which has saved substantial government funds in a short period since the office's establishment.


The Deputy Minister expressed the Ministry of Constitution and Legal Affairs' hope that the lawyers would use this training as a catalyst to continue these successes and foster a new enthusiasm for advancing these achievements for the benefit of the government, the country, and its citizens.


Solicitor General Dr. Boniphace Luhende outlined three main agendas for the training. The first agenda was the launch of the Office of the Solicitor General's logo, which will serve as an identifier in various communications. The second agenda involved training for government lawyers on various presentations and discussions. The third agenda was to evaluate how the Office of the Solicitor General, in collaboration with various government institutions, has managed and coordinated the handling of domestic and international claims and arbitration cases.


Since 2020, the Office of the Solicitor General has been organizing training sessions for government lawyers to enhance knowledge and skills in various complex areas of their work, aiming to increase efficiency and professionalism in their daily duties. In 2024, a total of 500 lawyers from all ministries nationwide, the Office of the Attorney General, the Office of the Attorney General Zanzibar, public institutions, the Office of the National Prosecutor, government agencies, public corporations, regulatory authorities, and various colleges across the country have participated.




Chama cha Mawakili Tanganyika TLS kupitia kwa Rais wake Tundu Lissu kilitangaza mgomo wa siku mbili kususia shughuli za Mahakama kuwaunga mkono Mawakili wa IMMMA Advocates kufuatia Ofisi zao kuvamiwa na kulipuliwa.
Hali ya sintofahamu imeendelea miongoni mwa Mawakili katika Mkoa wa Mwanza ambao pia ni Wanachama wa Chama hicho ambapo kumekuwa na mgawanyiko huku baadhi wakiunga mkono na kususia shughuli za Mahakama lakini wengine wakionesha kupinga hatua hiyo na kuendelea na shughuli za Mahakama kama kawaida kwa sababu mbalimbali.




Msomaji wetu Leo taarifa nyingine kubwa ni kuhusu watoto waliotekwa jijini Arusha .
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema Ametoa kauli baada ya utekaji huo ...
Video ya VOA TV Hii hapa.



Watoto waliotekwa mpaka sasa:
1. Maureen David (6yrs), anaishi Mtaa wa Olkereyan kata ya Olasiti.

2. Ikram Salim (3yrs), anaishi Mtaa wa Burka kata ya Olasiti.

3. Ayubu Fred (3.8yrs), anaishi Mtaa wa FFU kata ya Muriet

4. Bakari Selemani (3.6yrs), anaishi Mtaa wa FFU kata ya Muriet

Kwa taarifa za kimtandao mtekaji anaonekana yupo maeneo ya Olasiti buga ya chumvi


Mwenyekiti huyu 'Daudi Safari' Aeleza A-Z Jinsi Watoto alivyotekwa Arusha .. play video hapa


baada ya hapo VOA TV Ilifika katika Kituo kikuu cha polisi Arusha (Central Police) Kuthibitisaha iwapo kama Jeshi hilo limechukua hatua zipi baada ya tukio hilo la utekaji Wa Watoto hatimaye hakukua na mafanikio yoyote kwakua RPC Hakuepo ofisini kake.
Video hii hapa na iko LIVE!



Mahakama ya Korea Kusini imemuhukumu bosi wa kampuni ya Samsung, Lee Jae-yong kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la utoaji rushwa.
Bilionea huyo ambaye pia ni makamu wa rais wa kampuni hiyo ya utengenezaji vifaa vya umeme alishtakiwa kwa kosa hilo ambalo pia lilisababisha aliyekuwa rais wa nchi ya Korea Kusini, Pak Geun-hye kuondolewa madarakani.
Mbali na kosa hilo la utoaji rushwa ambalo alishtakiwa nalo, makosa mengine yaliyokuwa yanamkabili ni pamoja na wizi wa mali ya umma na kuficha mali nje ya nchi.
Hata hivyo wakili wa tajiri huyo, Song Wu-cheol amedai kuwa anaamini mahakama itabatiisha hukumu hiyo. Lee Jae-yong alikalia kiti cha uongozi katika kampuni ya Samsung kuanzia mwaka 2014 baada ya baba yake kupatwa na aradhi ya mshtuko wa moyo.

'Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 25, 2017 imeutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mfanyabiashara Yusuf Manji ili matokeo ya kesi hiyo yajulikane mapema.
Rai hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na wataeleza hatua ulipofikia katika tarehe itakayopangwa tena.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanajitahidi kukamilisha upelelezi ili matokeo yake yajulikane mapema ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi August 31, 2017.
Mbali ya Manji washtakiwa wengine ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere ambao wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi na Usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 200 na mihuri.' Source : Millardayo.com



JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Dkt Modester Opiyo, agoma kuahirisha kesi kutokana na mawakili wa Serikali kutokuwepo badala yake akaagiza watafutwe mpaka wapatikane kesi iweze kuendelea.

Jaji huyo aliagiza hayo jana baada ya wakili wa mleta rufaa, mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (CHADEMA), Sheki Mfinanga kuomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa kwa shauri hilo la rufaa kwani mawakili wa Serikali hawapo.

Aidha, Wakili Mfinanga,  aliomba mahakama impatie hati nyingine  ya kuwaita mawakili hao wa Serikali mahakamani hapo ili awapelekee tena ingawa wenye jukumu hilo ni Mahakama.

Jaji Dk Opiyo alisema kuwa hapendi kuona shauri hilo la rufaa ya jinai namba 48/2017 iliyowasilishwa Lema linavyokaa bila kuendelea kwani lilifika mbele yake kwa mara ya kwanza mwezi machi mwaka huu.

"Mimi hainisaidii chochote kesi hii kuendelea kukaa hapa, naomba namba ya simu ya wakili Njau au Nuda  (wakili wa Lema, Sheki akajibu hana ila akadai amewaona mahakamani hapo wakamwambia wana kesi nyingine mahakama ya hakimu mkazi Arusha) nenda kawaite," aliagiza Jaji huyo.

Baada ya kuwasili mawakili hao, Innocent Njau na Khaliki Nuda  walidai kuwa ofisi yao haijapata wito wa Mahakama kwa ajili ya shauri hilo jambo ambalo Jaji Dk Opiyo aliwahoji kama hawakuwa na wito ilikuwaje wakili wa Serikali, Penina Joachim alikuwa mahakamani hapo wakati shauri hilo lilipotajwa Mei 10, mwaka huu.

Wakili Njau aliomba kwa jana shauri hilo liendelee kusikilizwa kama ilivyokuwa imepangwa ila wao wataenda kufuatilia kwenye masjala ya ofisi yao kuona kama kuna hati hiyo ya wito wa mahakama.

Julai 12, mwaka huu shauri hilo lilishindwa kuendelea mahakamani hapo baada ya Mawakili wa Serikali kushindwa kutokea mahakamani hapo.

SHAURI HILO KUSIKILIZWA KWA NJIA YA MAANDISHI

Jaji Dk Opiyo alimwagiza wakili wa Lema kuwasilisha mahakamani hapo hoja zake za rufaa kwa njia ya maandishi Agosti 30, mwaka huu ambapo upande wa Jamhuri watatakiwa kuwasilisha hoja za majibu Septemba 13, huu.

Alisema kuwa mawakili wa Lema watawasilisha hoja za ziada Septemba 20, mwaka huu kabla ya kukutana Mahakamani hapo Septemba 27, mwaka huu kwa ajili ya kupanga tarehe ya kutoa uamuzi.

RUFAA

Uamuzi mdogo uliokatiwa rufaa ulitolewa februari 8, mwaka huu na Hakimu Mkazi,Bernad Nganga,  wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,  kwenye shauri la jinai namba 352/2016 ambaye alitupa pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa Lema wakitaka  shauri hilo likasikilizwe na majaji watatu kutokana na hati ya mashitaka kujumuisha masuala ya  kikatiba.

Akisoma uamuzi huo mdogo, Hakimu Mkazi, Nganga alisema kuwa mara baada ya kupitia hoja za pande zote mbili ameamua shauri hilo liendelee kwenye mahakama hiyo huku akidai kuwa endapo kuna masuala ya kikatiba yatakosa majibu basi itawanufaisha upande wa utetezi.

"Ushahidi wa Jamhuri kushindwa kutolewa  hautakuwa na madhara kwa mshitakiwa bali utamfaidisha na hoja ya shauri kuwa na masuala ya kikatiba, hoja hiyo huwezi kuitambua kwa kuangalia vifungu alivyoshitakiwa navyo mshitakiwa na kama ni hivyo hoja hiyo iletwe wakati wa utetezi kama kesi itafika hatua ya utetezi.

"Pingamizi zinatupiliwa mbali na mahakama hii haijaona haina uwezo wa kusikiliza hivyo tutaendelea na kesi ya msingi," alisema hakimu Nganga akihitimisha uamuzi wake.

Alisema, alipitia hati ya mashitaka inayoeleza kuwa Lema anashitakiwa kwa kosa la kushawishi kutenda kosa kinyume na kifungu cha 390 na cha 35 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jianai  ambapo anadaiwa kuhamasisha watu kufanya kusanyiko na maandamano isivyo halali.

"Baada ya kupitia hati hiyo na kwa mujibu wa kifungu cha 390 kinaelezea mtu akihusika na kushawishi kosa,hata kama halina madhara huyo mtu ni mkosaji.Kifungu cha 35 kinaelezea iwapo mtu akikutwa na hatiani kwa kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili au faini au vyote viwili kwa pamoja," alisisitiza hakimu huyo

Baada ya uamuzi huo wakili wa Lema, Sheki Mfinanga aliwasilisha kusudio la kukata rufaa kwa njia ya mdomo kwa kile alichoeleza kuwa hawajaridhika na uamuzi huo na kuomba kuwasilisha notisi hiyo ambayo ina nguvu sawa na rufaa huku akiomba kupatiwa mwenendo wa kesi hiyo pamoja na uamuzi huo mdogo  ili waweze kuandaa rufaa hiyo na kuwasilisha Mahakama Kuu.

"Tunaupinga uamuzi huu ulioutoa na tunaomba kuwasilisha notisi ya kukata rufaa ambayo ina nguvu sawa na rufaa na tunaomba shauri lisiendelee kwanza mpaka Mahakama Kuu ikasikilize rufaa yetu dhidi ya uamuzi huu," alisema Mfinanga.
Kinachoendelea kesi ya Mfanyabiashara Yusuf Manji..

Upande wa serikali umewasilisha pingamizi la awali Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga maombi ya dhamana ya mfanyabiashara Yusuf Manji. Pingamizi hilo limewasilishwa leo na wakili wa serikali, Paul Kadushi mbele ya Naibu Msajili, Sian Mustafa kutokana na Jaji Isaya Arufan anayesikiliza maombi hayo kutokuwepo.

Katika pingamizi hilo, wakili Kadushi amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana ya Manji.


 Pia kiapo kilichowasilisha cha kuhusu dhamana kinadosari kisheria, pamoja na kuwepo kwa vifungu visivyo sahihi. Baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Msajili Mustafa ameahirisha kesi hiyo hadi August 7/2017 kwa ajili ya kusikilizwa.