Showing posts with label Breaking News. Show all posts
Showing posts with label Breaking News. Show all posts

 Helikopta Iliyombeba Rais wa Iran Yahusika Katika Ajali, Vyombo vya Habari vya Serikali Vinaripoti



Vyombo vya habari vya serikali vinaripoti kuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi alikuwa kwenye helikopta ambayo ilitua kwa dharura siku ya Jumapili.

 Helikopta hiyo pia ilisemekana kumbeba Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian. 

Waziri wa Mambo ya Ndani alisema waokoaji bado wanajaribu kufika eneo la ajali kutokana na hali mbaya ya hewa. 

Hali ya waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo bado haijajulikana, na hakuna mawasiliano yaliyofanywa.



Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, Rais Raisi alikuwa akielekea katika mji wa Tabriz, kaskazini magharibi mwa Iran, baada ya kurejea mpakani na Azerbaijan ambako alifungua mabwawa ya Qiz Qalasi na Khodaafarin.


Ukungu mkubwa unafanya msako kuwa mgumu katika eneo ambalo inadhaniwa kuwa huenda helikopta hiyo ilitua, kulingana na ripota wa shirika la habari la Fars. Alisema mwonekano katika eneo la milima na misitu ulikuwa chini hadi takriban mita tano tu. Eneo hilo ni kama kilomita 50 kaskazini mwa Tabriz.


Ahmad Alirezabeigi, Mbunge wa Iran kutoka mji wa Tabriz, amewaambia waandishi wa habari mjini Tehran kwamba waokoaji bado hawajapata eneo la helikopta iliyombeba rais na waziri wa mambo ya nje. 

Aliongeza kuwa helikopta nyingine mbili katika msafara huo zilitua salama. Kanda za video zimeibuka kwenye televisheni ya taifa zikionyesha waumini wakimuombea afya rais katika mji mtakatifu wa Mashhad.


Rais wa Iran Ebrahim Raisi ni Nani?

Ebrahim Raisi, mwenye umri wa miaka 63, alichaguliwa kuwa rais katika jaribio lake la pili mwaka wa 2021. Anaonekana kama mhubiri mwenye msimamo mkali na anachukuliwa kuwa mrithi wa Ayatollah Khamenei siku moja, kiongozi mkuu wa nchi hiyo tangu 1989. 

Mnamo mwaka wa 2019, Kiongozi Mkuu alimteua kwenye nafasi yenye nguvu ya mkuu wa mahakama. 

Raisi pia alichaguliwa kuwa naibu mwenyekiti wa Bunge la Wataalamu, baraza la makasisi lenye wanachama 88 walio na jukumu la kumchagua Kiongozi Mkuu ajaye.



 15 WAFARIKI  AJALI ILIYOHUSISHA LORI NA MAGARI MADOGO MATATU, SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYOMBO VYA USALAMA



Watu kumi na tano wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha lori na magari mengine madogo matatu katika eneo la by Pass Ngaramtoni wilaya Arumeru Mkoa wa Arusha.



Akitoa taarifa hiyo katika eneo la ajali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP, Justine Masejo amesema ajali hiyo imetokea februari 24,2024 muda wa saa 11 jioni ambapo iliyohusisha lori na magari madogo matatu katika eneo la Ngaramtoni Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.


Kamanda Masejo amesema wanaendelea na uchunguzi wakina  kubaini chanzo haiisi cha ajali hiyo.


Aidha amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya mount Meru kutambua miili ya waliofariki katika ajali hiyo.


RAIS ATUMA SALAMU ZA POLE 

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya watu 15 katika ajali iliyohusisha magari manne eneo la Ngaramtoni, mkoani Arusha," anaandika Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ukurasa wake wa X Na kuongeza.


"Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa waliopoteza jamaa zao katika katika ajali hii. Ajali hizi zinachukuwa wapendwa wetu, nguvu kazi ya Taifa na mihimili ya familia. Naendelea kutoa wito kwa kila mmoja kuzingatia sheria za usalama barabarani katika matumizi ya vyombo vya moto. 


"Naagiza vyombo vyetu vya ulinzi, usalama na udhibiti kuendelea kuhakikisha vinasimamia sheria kikamilifu, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara wa vyombo vya usafiri na udhibiti wa leseni kwa madereva wanaorudia kuvunja sheria mara nyingi na wakati mwingine kusababisha watu kupoteza maisha.


"Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina,".




 Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki dunia leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dar es Salaam.


Taarifa ya kifo chake imetangazwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango.

 

Mtoto wa kwanza wa Mhubiri maarufu Dr. GeorDavie na Director wa video za Bongofleva, Nisher (Nic Davie), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, December 12, 2023, saa nane na dakika tisa, katika hospitali ya Selian (ALMC) Jijini Arusha.


Familia imethibitisha kifo hicho ambapo unafanyika nyumbani kwa baba yake Kisongo, Arusha. Habari zaidi kuhusu kifo chake zitatolewa baadaye.



Nisher ameacha pengo kubwa katika tasnia ya Bongofleva, akiongoza video maarufu kama "Kijukuu" na "Nje Ya Box." 

Msiba unaleta huzuni si tu kwa familia ya Dr. GeorDavie bali pia kwa tasnia ya muziki nchini.

Mipango ya mazishi na taratibu nyingine itatangazwa na familia. Taarifa za kifo chake zilithibitishwa kupitia ukurasa wa Instagram wa baba yake mzazi, Nabii Geodavie. 



 SAKATA la mwanamke  ,Teddy Malya, (31)kuuawa na hawara na kisha mwili wake  kukutwa umetupwa kwenye shamba la migomba  ukiwa utupu limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi kumkmta mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye inadaiwa amekiri kuhusika na mauaji hayo.

Mwili huo ulipatikana maeneo Ilboru Kisiwani, wilayani Arumeru Mkoani Arusha anakoishi marehemu  majira ya saa 2:30 asubuhi na wapita njia ambapo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mt Meru.

Mwanamke huyo anadaiwa kutoonekana siku moja kabla ya mwili huo kugundulika na wapita njia ukiwa kwenye shamba hilo la migomba huku majani yakiwa  yamevurugika .

Taarifa za wakazi wa eneo hilo zimedai kwamba marehemu alikuwa na mahusiano ya siri na mwanaume mwingine ambaye anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kwa kuwa inadaiwa alikuwa na ugomvi  akimtuhumu marehemu kutoa ujauzito wake, Jambo ambalo Mme wa marehemu alikanusha.

Mme wa marehemu, Richard Lanyuni(42) alieleza kuwa aligundua mke wake kuuawa baada ya kupokea taarifa za wapita njia kuwa kuna mtu amelala kwenye shamba la migomba ndipo alipofika na kuukuta ni mwili wa marehemu mkewe akiwa amepoteza maisha.

Akihojiwa na waandishi wa habari Lanyuni alieleza kwamba marehemu mkewe ambaye hufanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya Mbege hakuonekana kurejea nyumbani mida ya kawaida na ilipotimu majira ya saa saba usiku aliamua kulala ndipo kesho yake alipata taarifa za mkewe kuuawa.

“Mke wangu anafanya biashara ya kuuza pombe za kienyeji siku hiyo hakurejea nyumbani lakini nimeambiwa siku ya tukio alionekana akiwa na kijana mmoja anayefahamika.kwa jina moja la Baraka,”alisema Lanyuni na kuongeza.

.....Kuhusu mke wangu kuwa na mahusiano na mwanaume huyo siwezi kujua Ila hakuwa na ujauzito Ila naomba vipimo  vya kitaalamu vifanyike kujua kama kweli alikuwa na ujauzito maana anashughuli zake mimi siwezi kumchunguza sana.

Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani hapa, (RPC) , Justin Masejo amesema kuwa wanamshikilia mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume (jina limehidhadiwa kwa ajili ya uchunguzi)  Kwa tuhuma za kumuua mwanamke huyo.

Amesem kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa amekiri kuhusika na tukio hilo akidai kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu na siku ya tukio waliokuwa pamoja kwenye pombe na kulitokea ugomvi wa kutoelewana  .

“Mpaka Sasa tunamshikilia mtu mmoja ambaye amekiri kuhusika na mauaji hayo lakini tunaendelea na upelelezi ili kujiridhisha zaidi kama mhusika ni yeye peke yake ama kuna wengine”alisema Kamanda.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiroriki, Emmanuel Lazaro akidai kwamba mtuhumiwa alikuwa anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu enzi za uhai wake na siku ya tukio walionekana wakiwa pamoja wakinywa pombe.

Mwenyekiti huyo alieleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na baadhi ya nguo zake na viatu kukutwa eneo la tukio Jambo ambalo waliamini anahusika na mauaji hayo.

“Huyo jamaa alikamatwa kwenye nyumba mojawapo hapo mtaani amejificha na kilichopelekea ni baada ya viatu vyake pamoja na nguo kukutwa eneo la tukio,”alieleza Lazaro.

Hatahivyo alifafanua kwamba Jambo jingine lililowatia wasiwasi ni baada ya kumkuta mtuhumiwa akiwa na majeraha ya meno sehemu mbalimbali za mwili wake kitendo kinachoashiria waliokuwa na purukushani na marehemu kabla ya mauti kumfika.

 Alieleza kuwa marehemu kabla ya mauti kumfika alionekana akiwa na mtuhumiwa katika bar mojawapo mtaani hapo wakinywa pombe kabla ya kupatikana  akiwa ameshafariki.

“Tukio hili limetushtua sana sisi Kama wakazi wa huu mtaa Kwa kuwa sio la kawaida lakini tumeukuta mwili wa marehemu ukiwa hauna nguo na inaonekana alibakwa kabla ya kuuwawa”alisema Lazaro.

Baadhi ya majira wanadai kwamba mtuhumiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu wakidai kwamba mtuhumiwa alikasirishwa na hatua ya marehemu kudai kutoa ujauzito wake Jambo ambalo liliibua sintofahamu.

Prof Mwesiga Baregu

  MJUMBE wa kamati Kuu ya Chama Cha Demekrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Prof Mwesiga Baregu amefariki dunia kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akiendelea na matibabu. 


Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na familia hiyo zimethibitisha kutokea kwa kifo hicho  ambapo taarifa rasmi itatolewa na familia.


Profesa, Baregu alilazwa hospitalini hapo Februari 16, mwaka huu baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku inayofuata na Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Chadema, Tumaini Makene ilieleza kuwa hali ya  Prof Baregu iliendelea kuimarika taratibu tangu afikishwe hospitalini hapo ambapo alikuwa akipatiwa matibabu chini ya uangalizi maalum.


Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi ...


 

RAIS, John Pombe Magufuli ameaga Dunia.

Kifo cha Magufuli kimetangazwa rasmi usiku wa  Jumatano Machi 17, mwaka huu na makamu wake Samia Hassan Suluhu.

Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliopo jijini Dar es Salam kutokana na matatizo ya moyo.

Akithibitisha kifo hicho Suluhu amesema kwamba rais Magufuli alianza kuugua mnamo tarehe 14 mwezi Machi na kulazwa katika hospitali hiyo ambapo alifariki.

Aliyekuwa Ras mkoani Arusha, Richard Kwitega enzi za uhai wake



 KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha Ndugu Richard Kwitega amefariki dunia kwenye ajali iliyotokea Magugu akielekea Dodoma kikazi.

Aliyekuwa Ras mkoani Arusha, Kwitega enzi za uhai wake


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Kimanta amethibitisha kutokea kwa kifo hicho Cha Katibu Tawala Richard Kwitega.



 



 

 Mbunge wa zamani wa Maswa ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Maji kwa vipindi tofauti, Dk. Pius Ng’wandu amefariki dunia.

Dk. Ng’wandu amefariki dunia jana katika hospitali ya Somanda, Bariadi alipopelekwa kwa matatizo ya shinikizo la damu.



Waziri huyo amefariki dunia ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu alipofunga ndoa na mkewe.



Aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Maji, Nyumba na Maendeleo ya Mji mwaka 1985 hadi 1987.

Pia, Dk. Ng’wandu alikuwa Waziri wa Maji 1987 hadi 1990, nafasi ambayo aliishika tena mwaka 1996 hadi 1999.


Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Motisun Group ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa Mabilionea wachache nchini Tanzania na mfanyabiashara, Subhash Patel inadaiwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha karibu kimedokeza kuwa, kifo hicho kimetokea mapema leo na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Hivyo kupata undani wa habari hii usisite kutembelea website yetu mara kwa mara.


 


Afisa itifaki Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Swalehe Mwidadi na mfanyakazi Ofisi ya masijala, Amina Mshana leo wakiwasilia mahakama ya wilaya ya Arusha 

Amina Mshana akiwa kwenye mahakama ya wazi ya wilaya ya Arusha akisubiri kusomewa mashitaka yanayomkabili


Awali mwandishi wa Habari Lucas Myovela aliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari akidai watuhumiwa hao Kwa pamoja  walimteka, kumtisha Kwa silaha na kumdhalilisha kwa kumvua nguo kisha kupiga picha.



OFISA itifaki (protocol officer) mkoani Arusha,( jina linahifadhiwa) anatuhumiwa kumteka, kumpiga na kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mwandishi wa habari wa  kujitegemea, Lucas Myovela.
Aidha anadaiwa kumtisha kwa silaha, bastola na jambia huku wakimrekodi picha za utupu (video) ambapo walifanikiwa kuchukua fedha taslim elfu 75 alizokuwa nazo pamoja na kiasi kingine kutoa kwenye akaunti yake ya M Pesa.
Baada ya kukamilisha nia yake, ofisa itifaki huyo akisaidiana na watu wengine watatu anadaiwa kumpeleka Myovela kwenye kituo cha kati cha polisi na kudai kuwa ni jambazi aliyetaka kuwaibia gari.
Akiongea na waandishi wa habari nje ya kituo kikuu cha kati cha polisi Arusha, Myovela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya kupigiwa simu na mfanyakazi wa kike kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa, (jin linahifadhiwa).

Alidai mwanamke huyo aliwahi kuwasiliana naye siku za nyuma akimuomba amsaidie kupata watetezi wa kisheria kwani alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na ofisa itifaki huyo ambapo hataki kuendelea nayo kutokana na manyanyaso ya kupigwa.

Myovela anadai kuwa manamke huyo alimweleza kuwa ofisa itifaki huyo alimnunulia samani za ndani na vitu vingine ambavyo yuko tayari kumlipa ili waweze kuachana ambapo jumapili majira ya  saa 10 mwanamke huyo alimwambia amepata ushahidi wa sauti aliyomrekodi ofisa itifaki juu ya suala hilo hivyo ni muhimu wakaonana.

Anadai alimjibu kuwa kwa wakati huo hawataweza kuonana kwani alikuwa Moshi Mkoani Kilimanjaro akishughulikia matibabu ya Baba yake mzazi ambapo alimtaka akirudi Arusha wawasiliane.

Myovela alisema kuwa Amina alimpigia simu majira ya saa tatu usiku akimsisitiza ni muhimu waonane ambapo Myovela aliamua kuchukue usafiri wa pikipiki kutoka USA River maeneo ya Nelson Mandela anakoishi mpaka  Ngulelo alipotakiwa kukutana na Amina.

“Nilipofika nilimkuta yupo kwenye gari lake akaniambia kaa, nikakaa kwenye kiti cha mbele mguu mmoja nimeweka chini ili nimsikilize. Akawa anaendelea kuchat kupitia simu yake ya kiganjani lakini akawa ananiambia ndiyo ananitafutia hiyo sauti nikusikilizishe haikupita hata dakika tano akaja ofisa itifaki huyo na watu wengine watatu, ambapo wengine walikuwa ameziba sura zao kwa 'mask' usoni,".

"Wakishirikiana na (ofisa itifaki) walinifunga kamba iliyopita kichwani, shingoni wakanishika yule binti akauliza twende wapi wakasema twendeni Sakina wakaniambia tulia hivyo nikawa nimetulia tulipofika Sakina sehemu waliyopaki gari ni pambezoni mwa daraja,".

"Baada ya hapo wakaanza kunipiga kwenye gari 'wakanisearch' wakanivua sweta, simu zangu zote wakachukua, wakanitupia kwenye daraja bahati kule chini kulikuwa na maji nimeumia mguu tu wakazunguka wakaja na ndoo wakati huu mimi fahamu zangu kama hazipo sawa,".

"Wakanivuta mpaka nje ya daraja wakaanza kunipiga wakanitoa suruale nikabaki na vesti pamoja na boxer, wakanirudisha tena kwenye maji kama dakika 40 mpaka saa saba  kasoro usuku, wakaniamba wanataka laki 5, kwa sasa hizi hela ulizo nazo tunachukua zote nilikuwa na elfu 75 kwenye siku una shilingi ngapi wakaniambia toa pass word,".

"Walikuwa na kitu kama jambia na kitu kama bastola wakaniamba tofauti na hapo ubongo tunautawanyisha nikawapa password ya mpesa wakaangalia salio wakajirushia na ushahidi uko kwenye simu yangu hata jana nimeaonyesha hapa polisi,"

" Wakaniambia niwabe password ya kadi ya benki nikawaambia sikumbuki mpaka nikaangalie kwenye note book yangu wakatoa hiyo jambia wakaniambia hatuna haja hata ya kukukata vua hiyo boxer nikabakia uchi wakanza kunirekodi nikiwa uchi wakaniambia hizo hela zilizoko hapa kwenye akaunti yako zote tunachukua,". 
"Akaniambia tofauti na hapo tunataka laki 5 kufikia kesho (jumatatu) jioni nikawaambia sawa haina tatizo wakaniambia tofauti na hapo hizi video tunazozirekodi tutazitupia mitandaoni hiyo kesho jioni nikawaambia sawa,"
" Mmoja akasema tumchuke tumfungie kwenye mawe huku mtoni mwingine akasema hapa tumtafute askari wakataja kama majina ya askari wawili wanipe kesi basi wakanirudishia suruale yangu nivae kwa sababu boxer walikuwa wameshaichana,". 

"Wakaniambia tembea kwa miguu sisi tunakufuata nyuma kwa gari sikwenda umbali mrefu nikaanguka mwili ulikuwa umeisha nguvu.Akashuka jamaa mmoja mimi nikawekwa siti ya nyuma ofisa itifaki huyo alikuwa amekaa mbele wakaja mpaka kituo cha polisi Ngarenaro kikawa kimefungwa ndipo wakanileta hapa Central,".
Myovema anasema baada ya kufika polisi  Central "Wakasema huyu jamaa alitaka kutuibia gari lakini hakuweza tumemuwahi, polisi wakawauliza mbona anavuja damu wakamwambia alikuwa anajaribu kukimbia ameanguka kwenye mto tukamshika,"/
Myovela alisema kuwa alikanusha madai hayo ya ofisa itifaki na wenzake kwa kujitambulisha kwa polisi sanjari na kutoa vitambulisho vyake vinavyoonyesha yeye ni mwandishi wa habari.

" Nikawaambia hawa wameniteka hata sasa tunavyoongea hizo simu zao zina video walizonirekodi wakisema wanataka fedha. Basi polisi akawaweka chini ya ulinzi akachukua simu zao ofisa itifaki akakimbilia kwenye gari kufuta video lakini yule mmoja wakadai aliondoka na simu yangu kubwa,".
"Baada ya polisi kumuona ofisa itifaki amejifungia kwenye gari wakamgongea akafungua mlango wakachukua simu walipoifungua wakaona video nzima ya namna walivyonifanyia unyama,".
Myovela alisema kuwa aliandika maelezo mpaka saa 11 alfajiri akapatiwa fomu malum ya polisi kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu (PF 3) ambapo alienda hospitali ya mkoa ya Mount Meru ndio akairjesha kituo cha polisi cha kati.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa kuwa kuna mtu alitembea na mke wa mtu hivyo akaweka mtego wa kumpata mtuhumiwa hivyo jeshi la polisi litafanya uchunguzi kubaini ukweli ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Hata hivyo hakuwa tayari kutaja majina ya mtu anayedaiwa kufumania wala kufumaniwa na mke wa mtu kwa kile alichodai kufanya hivyo ni kuingilia upelelezi.

Majira ya mchana siku ya Jumatatu ofisa itifaki huyo alionekana akiwa kwenye ofisi maeneo ya polisi akiwa  amefuatana na askari wa upelelezi hata hivyo haikujulikana mara moja endapo yuko chini ya ulinzi au la.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Arusha (APC), Claud Gwandu alisema kuwa kitendo cha kutekwa na kudhalilishwa Myovela ni kitendo cha kikatili ambacho akifai kufumbiwa macho.
“Naamini kuwa Lucas ameonewa, na hata kama anamakosa kulikuwa na taratibu ambazo zilitakiwa kufuatwa na siyo kuitwa usiku na kuanza kuteswa kwa kuwekwa ndani ya maji, kuvuliwa nguo,kupigwa picha na kunyang’anywa vitu vyake vitendo hivi havikubaliki," alisema Gwandu na kuongeza.
“Tunataka watu wote waliofanya hivyo wachukuliwe hatua kwa bahati nzuri, wanajulikana na siyo wale wasiyo julikana tunataka hatua kali zichukulie na wafikishwe kwenye mikono ya sheria”








Imepostiwa kwenye akaunti inayoaminika kuwa ni ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo juu ya sakata la Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema (CHADEMA) Kuhamia CCM. 

katika Akaunti Hiyo Imewekwa Picha inayomuonesha Mbunge Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa RC Gambo na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

Hii akaunti inaaminika kuwa ni ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Picha aliyopost Mh. Mrisho Gambo.
Baadhi ya Comment za Wafuasi wa Akaunti ya RC Mrisho Gambo.


Tetesi pia zimeonekana kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha Ukata huo huku zaidi zikidai Siku ya jumatano Lema anatarajiwa kuongea na vyombo vya Habari kuthibitisha kukihama CHADEMA na kujiunga na CCM.


Awali Tulikupa updates kuhusiana na taarifa za kuvamiwa Nyumba ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, (CHADEMA), 


Sasa tumekuletea hizi picha za risasi zinazodaiwa kutumika katika Shambulio hilo ambalo  Mbwa waliokuwepo Nyumbani hapo waliuawa . 
Nasari amesema yeye na mkewe wamenusurika lililotokea usiku WA  kuamkia leo baada kukimbia ambapo ametoa taarifa kituo cha polisi Usa River.





Mabaki ya baadhi ya risasi zinazodaiwa  zilitumika Kushambulia Nyumbani kwa Mbunge Joshua Nasari.

Jitihada zetu za kuitafuta Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha japo Simu yetu imekuwa haipokelewi kwa zaidi ya Mara kadhaa 
Taarifa iliyotufikia Majira ya Usiku imedai watu hao wamefyatua risasi huku na kule huku kukiwa na taarifa ya kuuawa Mbwa waliyokuwa wakiwabwekea

Mbunge Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki anekuwa akiweka bayana Mara kadhaa kuhusu shutuma za kudaiwa kuwa kwenye list ya wabunge wa upinzani wanaofuatiliwa kutaka kuuawa.

VOA TV News & Habari Tanzania zimemtafuta Mbunge huyo iwapo kama amesharipoti tukio hilo na kuhusu usalama wake. Japo simu take haiku patikana Ila taarifa ya za uhakika zimeeleza Mbunge Hugo yupo Salama licha ya kuuawa kwa Mbwa kadhaa hapo nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Arusha Elias Mungure wakuiongea na vyombo vya Habari hivi punde Arusha

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh. Freeman Mbowe amesema chama hicho kimesusia uchaguzi huo wa Marudio kwenye kata zote za jimbo la uchaguzi la Arumeru Mashariki kata hizo ni pamoja na Makiba , Maroroni , Ngabobo , Leguruki na Ambureni.

Mbowe amesema chama hicho kinaitaka Tume ya Taifa ya uchaguzi kuitisha kurudiwa uchaguzi tena kwenye kata hizo za Arumeru Mashariki.

chaguzi kwenye kata hizo zimeharibika kwa sababu mbali zilizoelezwa na Uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Arusha kupitia kwa Katibu wa chama hicho Mkoa Elias Mungure ambaye amesema kumekuwa na Dosari nyingi ikiwemo vitendo viovu vinavyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwatoa nje mawakala wa chama hicho, 

Matatizo ya barua za utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi msimamizi Mkuu wa uchaguzi nazo zimetajwa kuwa Changamoto zilizopelekea chama hicho kususia uchaguzi huo.

Vitendo vya kihalifu dhidi ya Wafuasi na mawakala wa chama hicho navyo vimekuwa sababu nyingine ambapo ushahidi wa video umeonesha mmoja wa viongozi wa chadema tawi la Makiba akikatwa kikatili kwa mapanga na watu waluodaiwa kuwa ni wafuasu wa CCM. 

Hadi hivi sasa Habari Tanzania imefanya jitihada za kuntafuta Mkurugenzi wa Arusha DC ambaye ndiye anasimamia uchaguzi kwenye jimbo hilo suala ambalo halikufanikiwa kutokana na Mkurugenzi Huyo kutokupokea simu. Jitihada kumtafuta zinaendelea.