Showing posts with label Updates. Show all posts
Showing posts with label Updates. Show all posts
 MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha),Halima Mdee ameitaka jamii kupaza sauti pale inapobaini kuwepo kwa unyanyasaji dhidi ya mtoto na kupigania haki ya mtoto wa kike kupata uongozi .
Akizungumza katika kituo cha watoto yatima cha Samaritan Village kilichopo Moshoni,jijini hapa katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chama cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) alisema kuwa lazima jamii ipaze sauti zao ili watoto wabaki salama pale inapoonekana kuna dalili za unyanyasaji.
Aidha alisema kuwa pamoja na chamgamoto nyingi anazozipata kama mbunge, kamwe hatanyamaza na ataendelea kumtetea mtoto na kuitaka jamii iwe mstari wa mbele kupinga ndoa za utotoni kwa mtoto wakike.
Alisema watoto katika jamii wanafanyiwa ukatili mwingi, hivyo mtu yoyote anayejitokeza kulea watoto yatima anapaswa kupongezwa na kuungwa mkono kwani hilo ni taifa la kesho.
Katika maadhimisho hayo bawacha mkoa wa Arusha imetoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu katika kituo hicho cha watoto yatima Kama Sehemu ya maadhimisho .
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Arusha,Cesy Ndosi alisema kuwa wameamua kuungana na watoto yatima katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya chama hicho kama kutambua mchango wa watoto kwa taifa na kuitaka jamii kuyakumbuka makundi yaliyosahaulika kama watoto na wazee .
Naye Mratibu wa kituo cha yatima Samaritan Village, Josephat Mmanyi alishukuru kwa msaada huo na kusema kituo lina watoto 50 wenye umri wa miaka 21 hadi mwaka mmoja na wapo ngazi mbalimbali za shule.Hata hivyo alisema kituo bado kinachangamoto ya gharama za uendeshaji.
Alitumia fursa hiyo kimwomba Halima Mdee kupanda mti kituoni hapo ili kuamsha ari ya watoto wake wanaotamani kuwa wanasheria kama yeye. Play Video fupi hapa chini..

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure 

Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Mh.Halima Mdee Mara baada ya kuwasili katika Safari Hotel kwa ajili ya kuhudhuria Kongamano la Miaka 25 ya CHADEMA ambapo yeye ni Mgeni Rasmi.

August 20 usiku taarifa zilidai kuugua kwa Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya wakati akiwa rumande baada ya kukamatwa na Polisi Tarime ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya Tarime.


VOA TV Imempata Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Hippolite Tarimo ambaye amesema hali ya Mbunge huyo inaendelea vizuri na tayari ameandikiwa rufaa ya kwenda Hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi.
Ester Bulaya aliugua akiwa rumande baada ya kushikiliwa na Polisi kufuatia kumkamata akiwa Hotelini Tarime August 19, 2017.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinalitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha maamuzi yake dhidi ya wabunge wa CUF. 

Kituo kimesema kinafuatilia kwa karibu mwenendo wa Demokrasia Nchini, na kukiita kitendo cha Bunge la Jamhuri kupokea na kuridhia maamuzi ya Prof. Lipumba kuwa ni kitendo cha kuudharau Mhimili wa Mahakama, hivyo kulitaka kurejelea maamuzi yake.

TAMKO LA HAKI ZA BINADAMU HILI HAPA SOMA LOTE,





Huku nako, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif, amemjia juu Mhe. Ndugai kwa maamuzi hayo.. 

Akiwasilisha katika kilichosemwa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu, Maalim amesema hata kama maamuzi ya Spika na Tume yangestahili, basi yasingestahili kufikiwa bila kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Chama (ambaye ni yeye) na hata Profesa Lipumba anamtambua.. ambapo kwa mujibu wa katiba yeye ndie mtendaji mkuu wa maamuzi ya Chama.

Maalim amesema kikawaida tu, Spika angetakiwa kujiridhisha kwani licha ya kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama ndie Mratibu Mkuu wa Mikutano likiwemo Baraza kuu la Uongozi.
Maalim alimalizia kusema hilo linaloitwa Baraza Kuu lililowavua ubunge wabunge wao halikuundwa na wajumbe stahiki.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Elias Nawera abadili mwenendo wake kiutendaji na ashirikiane vizuri na Mkuu wa wilaya hiyo Samwel Jeremiah.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Alhamisi hii, wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.
Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.
“Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili,” alisisitiza Waziri Majaliwa.
Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu wa kuwatumikia Watanzania.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja na kufikia malengo ifikapo 2020. by Bongo5

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani.

Mhandisi Hamad Masauni amesema “RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutaki uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania,”

“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria.”  alisema Masauni






MAGUFULI AKUMBUKA: Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuonyesha Mkewe Mama Janeth Magufuli kitanda alichokuwa akitumia kulala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera.

Dkt Magufuli amemweleza mkewe kuwa alivunja hilo dirisha na mpaka leo halikutengenezwa ambapo leo hii amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukarabati dirisha na madirisha mengine ya shule hiyo.
Dkt Magufuli yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili mkoani humo.
Picha/Ikulu, Tanzania
#bbcswahili #Tanzania #Magufuli

Ripoti za kuaminika zinasema kuwa, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia na mwana wa mfalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman amekoswakoswa kuuawa kwa risasi ndani ya familia ya kifalme ya Saudia. 
Hayo yamethibitishwa na mtaalamu wa masuala ya kisiasa na ya kimataifa Dakta Hazam Hazam ambaye amefichua kwamba, Muhammad bin Salman amefyatuliwa risasi na watu wa ndani ya falimia ya kifalme ya Saudi Arabia.
Dakta Hazam ambaye yeye mwenyewe ni raia wa Saudi Arabia amesema kuwa, sababu ya kutoonekana hadharani mrithi huyo mpya wa kiti cha ufalme tangu baada ya kuchaguliwa na baba yake baada ya kumbwaga na kumuuzulu Muhammad bin Nayif, ni hali tete na isiyokuwa na utulivu inayotawala familia ya kifalme ya Saudia.
Dakta Hazam amongeza kuwa, mivutano na hitilafu baina ya mirengo na makundi hasimu ndani ya familia ya kifalme ya Saudi Arabia imepamba moto baada ya kuchaguliwa Muhammad bin Salman kuwa mrithi wa kiti cha mfalme na yaliyojiri baada yake na ripoti zinasema mmoja kati ya watoto wa Muqrin bin Abdul Aziz alifyatulia risasi Muhammad bin Salman na mmoja kati ya ndugu zake ambaye amejeruhiwa vibaya. Ripoti zinasema Muhammad bin Salman mwenyewe amepigwa risasi mkononi.
Mtaalamu huyo wa masuala ya kimataifa anasema, picha zinazoonyeshwa kwa sasa za Muhammad bin Salman si za sasa. Amesema kuwa vikao vimekuwa vikifanyika kila siku ndani ya ukoo unaotawala wa Aal Saud ili kupata suluhisho la hitilafu na mivutano hiyo na kwamba juhudi hizo bado hazijazaa matunda. READ MORE        
Taarifa iliyotolewa kwa umma na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imeeleza kuwa kuanzia sasa kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio, anayetaka kununua au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama husika pamoja na Mamlaka hiyo.
Pia uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Kwa sasa hapa nchini drone zimekuwa zikitumika kwa ajili ya kupiga picha za angani maeneo ya mashamba makubwa, mkusanyiko mkubwa wa watu. Pia zimekuwa zikitumika mara nyingi katika kuandaa video za muziki.

PARS TODAY , TEHRAN-IRAN 

Kauli ya Rais Magufuli kuhusu wanafunzi wanaopata mimba yawakasirisha wanawake"

"Wanawake wamekasirishwa na matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ya kupiga marufuku kurejea shule wasichana wanaopata ujauzito hata baada ya kujifungua.
Wanaharakati mbalimbali wa masuala ya wanawake wamekosoa kauli hiyo na kumtaka Rais Magufuli kuomba msamaha kwa matamshi hayo. Aidha baadhi ya wanaharakati wa masuala ya eneo wameitaka serikali ya Tanzania kutazama upya sheria inayomfukuza shuile msichana mwanafunzi anayepata mimba. 
Shirika moja la wanawake barani Afrika limemtaka Rais Magufuli aombe msamaha na wakati huo limewataka wanawake kusimama na kuipinga sheria hiyo ya Tanzania. 
Sheria iliyopitishwa mwaka 2002 nchini Tanzania inaruhusu kutimuliwa wasichana wanaopata mimba wakiwa shuleni.

Wanafunzi wasichana wa Shule ya Sekondari ya Weruweru ya Moshi Tanzania

Sheria hiyo inasema kuwa, wasichana wanaweza kufukuzwa shuleni kwa ''makosa yanayokiuka maadili na ndoa''.
Ni kwa muda sasa makundi ya haki za wanawake yamekuwa yakiishinikiza serikali ya Tanzania kubadilisha sheria hiyo, ingawa mpaka sasa juhudi hizo hazijazaa matunda. 
Mjadala kuhusiana na sheria hiyo umeibuka tena nchini Tanzania baada ya hivi juzi Rais Magufuli kunukuliwa katika mkutano wa hadhara akiwaonya wasichana wa shule kwamba ''unaposhika mimba mambo yako yamekwisha''.
Rais wa Tanzania aidha alisema, wanaume wanaowatia mimba wasichana wa shule pia nao wanapaswa kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 30 na kuweka nguvu zao walizozitumia kuwatunga mimba wasichana hao kulima wakiwa jela." pars today
BBC Swahili , LONDON - UINGEREZA "

Matamshi ya Magufuli kuhusu wasichana wa shule waliotungwa mimba yawakasirisha wanawake Tanzania" 

"
Rais John Magufuli
"Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.
Amesema; “Ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili lakini sekondari, darasa la kwanza  kupeleka walio na watoto, tunapoteza maadili yetu, watazaa mno.”
 “Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. Hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema.



                                     

Makamu wa Rais Wa Tanzania amesema Serikali haitarudi nyuma katika kupambana dhidi ya Rushwa.

"Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na mubimu katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu" alisema Mama Samia Suluhu
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Picha zote kwa hisani ya Mama Samia Suluhu.













 Dkt. Laurean Ndumbaro Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi Wa uma. Yupo mkoani Singida kwa ajili ya hafla iliyowakutanisha watumishi Wa uma huku lengo likiwa kusisitiza uadilifu Wa kiutendaji katika shughuli za umma.



Hivi karibuni Tuliripoti Habari ya kufungia Gazeti la Mawio na Serikali kupitia Wizara ya Habari vijana na Utamaduni chini ya Waziri Mh. Harrison Mwakyembe. Sasa leo ni zamu ya VOA Swahili ya Marekani kwa kuchapiaha story hiyo kwa mapana zaidi.





Waziri mkuu Kassim Majaliwa Amemuagiza Mkurugenzi Wa Wilaya ya Misungwi kuitiaha kikao kifuatia kero ya mahala pakujenga soko eneo la Kigongo.