IPU Waazimia Kudhibiti na Kutumia Akili Unde Kuimarisha Demokrasia

 


Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) umeazimia kuwepo kwa mifumo imara ya kudhibiti matumizi ya akili unde (AI) na teknolojia za kidijitali ili kukabiliana na changamoto za upotoshaji wa taarifa, uvujaji wa siri na ukiukwaji wa haki za binadamu duniani.

Mbali na udhibiti huo, umoja huo umesisitiza kuwa teknolojia hiyo inapaswa kutumika kama fursa ya kuimarisha ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya umma. Hatua hii itasaidia kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuwapa wananchi nafasi kubwa zaidi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kibunge.

Msimamo huo ni miongoni mwa maeneo makuu matano ya utekelezaji yaliyoainishwa kwenye Tamko la Arusha lililowasilishwa wakati wa kuhitimishwa kwa Mkutano wa 153 wa IPU jijini Arusha. Tamko hilo lilisomwa kwa pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania IPU pamoja na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya IPU kutoka Bangladesh, Barrister Jahrat Adib Chowdhury.

Mkutano huo pia ulihitimishwa kwa tukio kubwa la kihistoria ambapo Spika wa Bunge la Australia, Milton Dick, alichaguliwa kuwa Rais mpya wa IPU, akichukua nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

#IPU153Tanzania #AkiliUnde #TamkoLaArusha


0 Comments:

Post a Comment