DKT. ABBASI AONGOZA MAANDALIZI YA TUZO ZA KIMATAIFA ZA WORLD TRAVEL AWARDS SERENGETI

 


SERENGETI, TANZANIA — Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Novemba 18, 2026 ameongoza kikao muhimu cha Kamati ya Maandalizi ya Hafla ya Ugawaji Tuzo za Kimataifa za Utalii (World Travel Awards - WTA), zinazotarajiwa kufanyika Desemba 12, 2026 ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


 

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Dkt. Abbasi amesisitiza kuwa tukio hilo lina hadhi ya juu kimataifa, hivyo maandalizi yote lazima yaendane na ukubwa wake ili kuhakikisha linafanyika kwa viwango vya hali ya juu vitakavyoacha alama duniani.


Amesema Tanzania imepata fursa adhimu ya kujitangaza zaidi kimataifa kupitia hafla hiyo kubwa, ambapo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti itakuwa mwenyeji wa wageni mashuhuri, wawekezaji, na wadau wa sekta ya utalii kutoka pembe zote za dunia.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambayo inatambulika kote duniani kwa maajabu ya uhamaji wa mamilioni ya Nyumbu (The Great Wildebeest Migration), inatarajiwa kuwa jukwaa maalum la kuonesha ulimwengu uzuri wa vivutio vya kipekee vya Tanzania pamoja na ubora wa huduma zake za utalii.
Kwa habari zaidi za utalii, kitaifa na kimataifa, tembelea tovuti yetu: www.habaritanzaniahub.co.tz
Usisahau ku-Like, ku-Share na ku-Follow kurasa zetu za mitandao ya kijamii ili usipitwe na matukio muhimu!
Hashtags:
#HabariTanzaniaHub #UtaliiTanzania #Serengeti #WorldTravelAwards #WTA2026 #VisitTanzania #TheRoyalTour #TanzaniaUnforgettable #MaliasiliNaUtalii #DktHassanAbbasi #WildebeestMigration

0 Comments:

Post a Comment