Showing posts with label Wanawake. Show all posts
Showing posts with label Wanawake. Show all posts

 


 

Arusha, Tanzania – Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati imetoa majiko ya nishati safi kwa wachoma nyama wa mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuondokana na matumizi ya nishati chafu kama mkaa na kuni. Hatua hii inalenga kulinda afya za wananchi na kuhifadhi mazingira kwa kupunguza ukataji miti hovyo.



Akizungumza leo Machi 07, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda ametangaza kuwa wachoma nyama wote wa mkoa huo watawekewa mpango wa kupata majiko mbadala ya nishati safi. 



"Kuanzia sasa, shughuli zote za uchomaji nyama Mkoani Arusha zitatumia nishati safi. Tunataka kulinda afya za wananchi wetu na mazingira yetu," alisema Makonda.



Kwa upande wake, baadhi ya wachoma nyama walioanza kutumia nishati safi walieleza tofauti kubwa kati ya nishati hiyo na mkaa. 



Walisema kuwa majiko hayo mapya yanapunguza moshi na yanawapatia faida zaidi kiuchumi.



Makonda aliongeza kuwa wananchi watakaohudhuria hafla ya Nyama Choma jioni ya leo watapata fursa ya kuonja nyama zilizochomwa kwa kutumia nishati safi, akisisitiza kuwa juhudi hizi zinaungwa mkono na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. 



"Tunapenda wananchi waje waonje ladha ya nyama iliyopikwa kwa nishati safi. Huu ni mwanzo wa mabadiliko makubwa kwenye sekta ya chakula na mazingira," alisisitiza.



Hatua hii inakuja wakati serikali ikiendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama njia ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya za wananchi.



 

Na Gift Mongi, Moshi

Ni maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambapo huadhimishwa May12 ya kila mwaka duniani kote .






Katika maadhimisho haya mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amesema mwanamke bado ana nguvu kwenye jamii na hivyo anastahili uwezeshwaji.


'Tunaungana na wanawake kwenye hii siku yao niseme mwanamke bado ana nguvu kwenye jamii wanapokwama sisi tutafanya 'anasema


Bi Theresia Komba ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM)ambapo ameeleza umuhimu wa mwanamke katika familia na jamii kwa ujumla wake!


Mosi anasema ili jamii iweze kujikwamua katika nyanja zote lazima nyuma iwepo nguvu ya mwanamke ambaye ndiye muasisi wa mafanikio.


Pili mwanamke ni nyenzo katika mafanikio yoyote yale na katika hilo yapo mengi yanayoonekana kupitia mheshimiwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


'Ndio kafanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi tu huu ni ushahidi kuwa bado wanawake tunaweza!"anasema Bi Theresia


Anaenda mbali zaidi na kuongeza kubwa wanawake hawa kuaminika na kuonekana kama sio sehemu ya jamii kitu ambacho sio sahihi


'Mwanamke hakuaminika ilibidi ukitaka kufanikiwa umtegemee mwanaume ila sasa kuna utofauti  yaani tunajitambua'anasema Mwenyekiti huyo


Beatrice Mgaya ni mama wa mtoto mmoja anayeishi Pasua mjini Moshi ambapo anasema siku hii muhimu kwao alikua hakumbuki ila akawapa kongole wanawake wanaofanya vyema katika nyanja mbalimbali 


'Nisiseme uongo leo niliishi ila kwa wenzetu wanaofanya vyema hatuna budi kuwapongeza lakini kuwatia moyo vilevile 'anasema

 WAZIRI wa maendeleo ya Jamii Jinsia na makundi maalumu, Dkt Dorothi Gwajima,anatarajiwa kuwa mgeni rasimi kwenye kilele cha siku ya Mwanamke anayeishi Kijiji duniani itakayoadhimishwa Kijiji cha Olevolos kata ya Kimnyaki, Wilayani Arumeru Oktoba 15 .


Madhimisho hayo kitaifa yanafanyika Kijijini hapo kutokana na Kijiji hicho Nchini kuanzisha Sheria ya kutoa adhabu kwa kila mkazi atakae kiuka maadili ikiwemo kuvaa mavazi ya mlegezo maalumu kata K ,kunyoa kiduku watatozwa shilingi elfu 50.


Lengo la kuanzishwa Sheria hiyo ni kudumisha maadili yaliyo mema na kuweza kuwarejesha wale wote walioacha maadili kurejea kwenye maadili mema ambayo yatakuwa ni mfano wa kuigwa.



Akifungua  mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na Jukwaa la Mwanawake Kijijini 2023 kwenye uwanja wa Kijiji cha Olevolosi kata ya Kimnyaki Wilayani Arumeru,Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha,Blandina Nkini,amehimiza Jamii kuzingatia maadili Ili kuondoa mmomonyoko wa maadili ambao kwa sasa limekuwa ni tishio kubwa Kwa wananchi wa Vijijini na mijini.


Amesema chanzo cha mmomonyoko wa maadili  ni familia kuyumba na kushindwa kutimiza wajukimu na uwajibikaji  kuna sababisha mmomonyoko wa maadili hivyo iwapo familia zitasimama imara mmomonyoko huo hautakuwepo


Amesema kuwa  Wanawake ndio wazalishaji wakubwa lakini wamekuwa wakikandamizwa Kwa kunyimwa hali ya kumiliki mali na kushirikisha kwenye maamuzi.


Afisa usitawi wa Jamii Mkoa wa Arusha,Denis Mgie,amesema kuwa Kijiji hicho kimeweka Sheria hiyo baada ya kuwepo changamoto Katika malezi,hivyo Kijiji hicho kimekuwa Wakala mkubwa wa mabadiliko Katika malezi na makuzi ya watotonchini.


Amesema kuwa kauli ya kusema sitaki mtoto wangu  ateseke imetumika vibaya  siku tulizania  tumelea kumbe tumeharibu.


Amesema kuwa Jamii inatakiwa kuongoza Kwa misingi mizuri kwa kuweka misingi ya watoto na Vijana Ili kuelewa nafasi ya mzazi au mlezi .


Amesema mmomonyoko wa maadili pia unaochangiwa na baadhi ya wazazi au walezi kutokuwajibika  kulea watoto kwa kuacha jukumu hilo la kulea watoto kwa dada wa kazi na matokeo yake mtoto akiwa mkubwa atampeleka mzazi kwenye Kituo cha kulea wazee


Amesisitiza kwamba  malezi ya watoto ni nguzo muhimu Katika  kuelekea kuwa na taifa lenye watu wanaojitambu.


Kauli mbiu ya madhimisho hayo inasema Wezesha Wanawake wanaoishi Kijijini kwa uhakika wa chakula , lishena uendelevu kwa familia .