ozo ulioombwa na Freeman Mbowe kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, umesaidia wananchi kuweza kusikiliza na kuangalia live ambacho alikuwa akiseme Kamanda Lissu.
Katika mwongozo huo kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Mbowe aliomba mwongozo wa kiti juu ya kukatika kwa matangazo ya moja kwa moja ya kikao cha bunge wakati Lissu alipokuwa akiwasilisha ufafanuzi wa wachache kwenye Kamati Namba 4.
Alikiambia kiti kuwa pamoja na unyeti wake, mchakato wa Katiba Mpya ni suala la wananchi, ambao wanapaswa kujua kila kinachoendelelea, sasa hatua gani zinachukuliwa pale ambapo matangazo ya moja kwa moja yanakatishwa pale ambapo mjumbe mmoja anaanza kuwasilisha maoni ya watu wachache kwenye moja ya kamati.
Sitta baada ya kupata 'briefing' kutoka kwa Katibu wa Bunge juu ya kitu gani hasa kilichotokea hadi matangazo yakakatwa, aliahirisha bunge na akatoa maamuzi kuwa Kamanda Lissu ataendelea na ufafanuzi wake Jumatatu ijayo. So, stay tuned...
Yafuatayo ndiyo maoni ya wajumbe wachache katika Kamati ya Bunge Maalum la Katiba namba 4, yaliyokuwa kwenye taarifa ya kamati hiyo, ambayo yalipaswa kutolewa ufafanuz
MAONI YA WAJUMBE WALIO WA WACHACHE KATIKA KAMATI NAMBA NNE KUHUSU SURA YA KWANZA NA SURA YA SITA YA RASIMU YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
[Kanuni ya 32(4) ya Kanuni za Bunge Maalum, 2014]
UTANGULIZI
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sura ya Kwanza na Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (‘Rasimu’) ndizo msingi ambao Rasimu yote imejengwa juu yao. Wakati Sura ya Kwanza inagusa suala la muundo wa Muungano katika ibara moja tu kati ya ibara tisa, Sura yote ya Sita inahusu ‘Muundo wa Jamhuri ya Muungano.’ Suala la Muungano na hasa Muundo wake limetawala mjadala wa kisiasa na kikatiba wa Tanzania kwa zaidi ya miaka thelathini. Ndio maana katika waraka wake wa siri kwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (‘CCM’), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya chama hicho imetamka kwamba “muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi.”
Suala hili pia limetawala mchakato wa Katiba Mpya tangu ulipoanza miaka mitatu iliyopita. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Joseph Sinde Warioba wakati wa kuwasilisha Ripoti ya Tume yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar tarehe 30 Disemba, 2013: “Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu Rasimu ya awali ilipotolewa ... ni Muungano wa Tanzania. Jambo kubwa limekuwa juu ya muundo wa Muungano.”[1]
Umuhimu wa suala hili unathibitishwa pia na uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum kuelekeza kwamba Kamati zake Namba Moja hadi Kumi na Mbili zianze kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu. Haya ni maoni ya wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne juu ya Sura hizi mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mjadala wa Kamati Namba Nne kuhusu Sura za Kwanza na Sita za Rasimu unathibitisha pia umuhimu wa suala la muundo wa Muungano katika mjadala mzima wa Rasimu. Kama Taarifa ya Kamati yetu inavyoonyesha, Kamati Namba Nne imeshindwa kufanya uamuzi kuhusu suala hili katika ibara za 1 na 60 za Rasimu. Katika ibara ya 1 ya Sura ya Kwanza, wajumbe walio wengi walipata kura 22, ambayo ndiyo theluthi mbili ya kura za wajumbe wote 33 wa Tanzania Bara wa Kamati Namba Nne. Kwa upande wa Zanzibar, wajumbe walio wengi walipata kura 9 ambayo ni pungufu ya kura 13 zinazohitajika ili kufikisha idadi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 19 wa Zanzibar.
Kwa upande wa ibara ya 60, wajumbe walio wengi walipata kura 22 za wajumbe kutoka Tanzania Bara, ambazo ni theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote 33 kutoka Tanzania Bara. Aidha, kwa Zanzibar, wajumbe walio wengi walipata kura 8, ambazo pia ni pungufu ya kura 13 zinazotakiwa kufikisha idadi ya theluthi mbili ya wajumbe wote 19 kutoka Zanzibar. Kwa sababu hiyo, ibara za 1 na 60 za Rasimu hazikupitishwa au kuamuliwa na Kamati Namba Nne kama inavyotakiwa na kifungu cha 26(2) cha Sheria na kanuni ya 64(1) ya Kanuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Sasa tunaomba kwa ridhaa yako, tuwasilishe hoja na sababu za maoni ya wajumbe walio wachache katika Kamati Namba Nne kuhusu Sura hizi mbili ambazo ndio ‘moyo wa Rasimu.’
SURA YA KWANZA
Sura ya Kwanza ya Rasimu inahusu ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Sehemu ya Kwanza ya Sura hiyo inazungumzia ‘jina, mipaka, alama, lugha na tunu za Taifa.’ Ibara ya 1 inaitambulisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; ibara ya 2 inatangaza ‘eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’; na ibara ya 3 inaweka utaratibu wa ‘alama na sikukuu za Taifa.’ Vile vile ibara ya 4 inaweka utaratibu wa lugha ya Taifa na lugha za alama, wakati ibara ya 5 inahusu ‘tunu za Taifa.’
Kwa upande wake, Sehemu ya Pili ya Sura ya Kwanza inaweka masharti ya ‘mamlaka ya wananchi, utii na hifadhi ya Katiba. Ibara ya 6 ya Sehemu hiyo inatoa ufafanuzi wa ‘mamlaka ya wananchi’; ibara ya 7 inafafanua uhusiano kati ya ‘watu na Serikali’; ibara ya 8 inashurutisha ‘ukuu na utii wa Katiba’; na ibara ya 9 na ya mwisho inaweka ‘hifadhi ya utawala wa Katiba.’
IBARA YA 1
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kama maelezo yake ya pembeni (marginal note) yanavyoonyesha, ibara ya 1 inaitambulisha ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Ibara ya 1(1) inatamka kwamba “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.”
Kwa upande wake, ibara ya 1(2) inafafanua kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.” Mwisho, ibara ya 1(3) inatukumbusha kwamba “Hati ya Makubaliano ya Muungano ... ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.”
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Wajumbe walio wachache wa Kamati Namba Nne wanapendekeza mabadiliko ya jina la nchi yetu kutoka jina la sasa la ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ kuwa jina jipya la ‘Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.’ Aidha, wajumbe hao wanapendekeza kuacha kutajwa kwa Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 katika ibara ya 1(1) na (3) ya Rasimu. Badala yake, inapendekezwa kwamba Katiba hii ndiyo iwe msingi wa Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.
Kwa mapendekezo haya, ibara ya 1(1) itasomeka kama ifuatavyo: “Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar ni Shirikisho ambalo limetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.” Kwa mantiki hiyo, ibara ya 1(2) itasomeka: “Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar ni Shirikisho la kidemokrasia linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu, kujitegemea, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na lisilofungamana na dini.” Aidha, ibara ya 1(3) itasomeka: “Katiba hii ndio msingi mkuu wa Shirikisho la Jamhuri za Tanganyika na Zanzibar.” Zifuatazo ni hoja na sababu za mapendekezo haya.
SHIRIKISHO AU MUUNGANO?
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Katika nusu karne ya uhai wake, nchi yetu imeitwa ‘Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’ Hata hivyo, katika kipindi chote hicho, Katiba na Sheria za nchi yetu hazijawahi kufafanua kwa uwazi aina au haiba ya ‘Muungano’ huu. Matokeo ya kukosekana kwa ufafanuzi huu ni kwamba katika nusu karne hiyo, kumekuwa na mjadala mkubwa wa kikatiba, kisiasa na kitaaluma kuhusu suala la kama Jamhuri ya Muungano ni dola ya muungano (a unitary state), au ni dola ya shirikisho (a federal state). Majibu ya swali hili yamekuwa na athari za moja kwa utambulisho, haki, maslahi na wajibu wa Washirika wa Muungano huo, yaani Tanganyika na Zanzibar, na hasa kwa wananchi wa nchi hizi mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kukosekana kwa ufafanuzi wa aina ya muungano wetu haujawa suala la mijadala ya kisiasa na kikatiba peke yake, bali kumekuwa ni chanzo cha migogoro mikubwa ya kisiasa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Migogoro hii ilianza tangu mwanzo kabisa wa Muungano wakati wa sakata la kuwa na ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Magharibi kwa upande wa Tanganyika na ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa upande wa Zanzibar.
Aidha, kati ya mwaka 1964-1967 ulizuka mgogoro mkubwa kuhusiana na uwakilishi wa Zanzibar katika iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania; kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuundwa kwa CCM mwaka 1977, na katika mjadala wa marekebisho ya Katiba wa mwaka na baadae ‘kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa Zanzibar’ mwaka 1983/1984.
Baadae mwaka 1988 ulitokea mgogoro mkubwa uliopelekea kung’olewa madarakani kwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad na baadae kufukuzwa katika CCM; wakati wa harakati za kudai kura ya maoni kuhusiana na M
A MUST READ; MAONI YA WACHACHE KAMATI NAMBA 4-HOJA ZA WANANCHI WENGI
Saturday, April 12, 2014
No Comment
0 Comments:
Post a Comment