Nanyaro azidi kukufanya makubwa kata ya Levelosi -Arusha

Diwani wa kata ya Levelosi mhe. Nanyaro Ephata ameendelea kufanya makubwa ndani ya kata yake baada ya jana kukabidhi unga na sukali na kukagua ujenzi wa jiko la kisasa kwenye shule ya msingi Levelosi ikumbukwe mwenyezi uliopita hospitali ya Levelosi alifanikiwa kuipandisha hadhi na kuwa hospitali ya wilaya.
Baada ya kufanikiwa kuipandisha hadhi hospitali ya Levelosi na kuwa hospitali ya wilaya diwani Nanyaro ameendelea kufanya makubwa ndani ya kata ya levelosi baada ya jana kukabidhi unga na sukari kama kawaida kwaajili ya watoto wa shule hiyo kupata uji na walimu kupata chai.
Pia Diwani huyo alikagua ujenzi wa jiko la kupikia na kushuhudia walimu wakiahamia kwenye nyumba alizo zisimamia ..Akiongea na waandishi wa habari Mwalimu mkuu(Kaaya) wa shule hiyo alisema waalimu na wanafunzi wanamshukru sana diwani huyo kwa juhudi zake za kuhakikisha shule hiyo ina kuwa ya kisasa kabaisa kwani kwasasa kuna miradi zaidi ya mitano inaendelea shuleni hapo na miwili ikiwa imekamilika kwa 100% na mitano 70% kama mnavyoona kuna mradi wa thamni ya mil 12 wa kuvuna maji ya mvua ambao unaendelea kwa sasa huku chama chake kikiwa kimeahidi kupaka rangi mabati ya majengo yote ya shuleni hapo hii hijawahi kutokea alisema Mwalimu Kaaya
naye mwalimu Fred aliye pokea unga na sukali alisema wana mshukru Diwani huyu wa chadema kwa juhudi zake kwani sasa wanafunzi wanaafya na hata mahudhulio yameongezea sana ambalo ndiyo lilikuwa dhumuni la kuwapatia watoto uji
.






0 Comments:

Post a Comment