Home
About Us
Contact Us
Home
MATUKIO
HABARI
KITAIFA
KIMATAIFA
SHERIA
HIVI PUNDE: Mahakama yapiga 'STOP' Bomoa Bomoa Dar
Sunday, August 20, 2017
No Comment
Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeziwekea kinga ya muda nyumba 286 zisibomolewe wakati operesheni ya ubomoaji wa nyumba zilizoko ndani ya umbali wa mita 121.5 kutoka katikati ya Barabara ya Morogoro ikiendelea maeneo ya Kimara mpaka Kiluvya jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo wa Mahakama ulitolewa juzi na Jaji Leila Mgonya kutokana na maombi ya zuio yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wakazi hao 286 wa maeneo ya Ubungo- Maji hadi Kiluvya wakiomba itoe zuio la muda hadi kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Maombi hayo ya zuio la muda kusubiri uamuzi wa kesi ya msingi yamepangwa kusikilizwa Agosti 30 mwaka huu baada ya upande wa wajibu maombi (Serikali) kuwasilisha hati ya kiapo kinzani.
Hata hivyo, wakati wakisubiri usikilizwaji wa maombi ya zuio la muda, wananchi hao kupitia kwa wakili wao, Benito Mandele waliwasilisha maombi ya dharura wakioomba mahakama hiyo iamuru hali iendelee kuwa kama ilivyo kwa sasa hadi maombi hayo yatakaposikilizwa.
Wakili Mandele amesema kuwa waliamua kupeleka maombi hayo ya kudumisha hali iliyopo kwa sasa baada ya kuona Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) wameanza kutekeleza operesheni hiyo wakati maombi yao ya zuio yakiwa bado hayajasikilizwa.
Jaji Mgonya anayesikiliza shauri hilo alikubaliana na maombi hayo na kuamuru hali iendelee kuwa kama ilivyo kwa sasa hadi tarehe hiyo ya maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Kwa uamuzi huo, Tanroads ambayo ndiyo mtekelezaji wa operesheni hiyo haitaweza kuzigusa nyumba hizo hadi hapo mahakama itakapoelekeza vinginevyo baada ya usikilizwaji wa maombi hayo ya zuio la muda kusubiri kesi ya msingi kumalizika.
Wakili Mandele amesema kuwa watakachofanya baada ya kupata hati ya amri hiyo ya mahakama wataitoa nakala nyingine na kuwagawia kila mdaiwa kwa ajili ya kuiweka kwenye nyumba yake.
Katika kesi ya msingi namba 284 ya mwaka 2017, wananchi hao wanaiomba mahakama itamke kuwa wao ni wamiliki halali wa maeneo hayo yenye mgogoro na kwamba hawapo katika hifadhi ya barabara.
Maombi hayo yanasikilizwa na Jaji Crencecia Makuru na amepanga kutoa uamuzi kuhusu pingamizi hilo Agosti 30, uamuzi ambao ndio utakaotoa hatima ya maombi hayo kama yataendelea kusikilizwa au yatatupiliwa mbali.
Awali Tanroads ilimetoa notisi kwa wakazi wote walio katika umbali wa mita 121.5 kutoka katikati ya barabara ya Morogoro kila upande, kuanzia Ubungo Maji hadi mpakani mwa Dar es Salaam na Pwani kuvunja nyumba zao kwa madai kuwa wapo kwenye hifadhi ya barabara.
https://youtu.be/PeeFSA6wjLk
Newer Post
Older Post
Home
0 Comments:
Post a Comment
About Me
Grace Macha
Karibu msomaji wangu Utapata habari za siasa Uchumi, matukio na kijamii zilizohaririwa kwa kuzingatia maadili ya habari
View my complete profile
Blogu Marafiki
Follow Us!
Zinazo Somwa Zaidi
FARU VICKY ALIVYOCHANGANYWA NA FARU TELELE NA KUMPIGA CHINI FARU JOHN
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro Hayawi hayawi sasa yamekuwa, tarehe 22 Septemba, 2026 wahifadhi Duniani kote wanaungana kuadhimisha siku ya...
WATUPWA GEREZANI KWA KUTENGENEZA NA KUKUTWA NA POMBE BANDIA PAMOJA NA STAMP FEKI ZA TRA
Mahakama ya Wilaya ya Arusha imetoa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa mtuhumiwa mmoja na kuwaachia wawili kwa masharti kufua...
KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro Ilinenwa “KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA”, ndivyo walivyofanya waumini wa Parokia ya Mt. Petro Masan...
Kilio cha Mzazi Sekenke: Kapteni Mbutu Amlilia Mwanae Aliyepoteza Maisha Kwenye Ajali ya Polisi na Lori la Mafuta
SINGIDA: Watu 12, wakiwemo askari polisi watano na mahabusu, wamepoteza maisha kufuatia ajali mbaya iliyotokea leo asubuhi katika Mlima wa ...
Tanzania Strengthens Trade and Investment Ties with the European Union and South Korea
Dar es Salaam, February 18, 2025 – Prime Minister Kassim Majaliwa held discussions today with the European Union (EU) Ambassador to Tanza...
NGORONGORO KUZALIWA UPYA
Wilaya ya Ngorongoro ipo katika hatua za mwisho ya mapitio na kupitisha mkakati mpya wa miaka mitano unaodhamiria kufanya mageuzi makubwa ya...
PALU Seeks Advisory Opinion from African Court on Women’s Inheritance Rights
Arusha, Tanzania, — The Pan African Lawyers Union (PALU), in partnership with the Clooney Foundation for Justice, has formally filed a reque...
TANAPA Receives Modern Truck to Support Community Engagement in Serengeti
Serengeti, Tanzania – The Tanzania National Parks Authority (TANAPA) has received a modern ISUZU truck worth USD 177,966 from the Frankfur...
DAR MAIZE EXPORTERS SAY THEY ARE CONFORMING WITH TRADE RULES
BY GRACE MACHA IN ARUSHA Commodity exporters to Kenya have distanced themselves from a recent 'rogue traders' remark by a Kenyan ca...
INTERNAL AUDITORS WANT RECOGNITION, RESOURCES AND SECURITY
BY GRACE MACHA IN ARUSHA Internal auditors want full recognition from the heads of their respective institutions and adequate resources to i...
MAKTABA
Habari
(1074)
Magazeti
(846)
Newspaper
(237)
Tourism
(131)
UTALII
(131)
siasa
(122)
Breaking News
(117)
CHADEMA
(100)
Kimataifa
(80)
Updates
(73)
Michezo
(68)
Ngorongoro
(65)
Habari kuu
(53)
DIAMOND PLATNUMZ
(44)
Habari za Kimataifa
(39)
MAHAKAMANI
(38)
Burudani
(35)
SHERIA
(31)
Tanzia
(27)
KILIMO
(26)
AFRICA NEWS
(22)
UTEUZI
(22)
Uhalifu
(9)
Teknolojia
(8)
Utafiti
(4)
Urembo
(1)
Contact Us
Name
Email
*
Message
*
0 Comments:
Post a Comment