Kwa wale wafuatiliaji wa Mashindano ya Vipaji nchini Marekani Hii sasa yaweza kuwa Habari njema zaidi kwao na ikawa Habari mbaya kidogo kishabiki.
Pamoja na Mengine mengi ya kufahamu kuhusiana na Tamasha la Vipaji nchini humo kwanza ni AGT-American Got Talent ambayo inaratibu na kuyaendesha Matamasha hayo ya Vipaji nchini Marekani.
September 13 kulifanyika Mchujo wa kuelekea Fainali ambapo Mchujo ulianza kwa washiriki kupandishwa jukwaani wote. Nakuanza na kikundi cha kwanza.
Macho ya Halaiki yalikuwa kwa mtoto wa miaka 09 ambaye ana kipaji cha kuimba cha kipekee sana Angelica Hale
Angelica alitangazwa wa kwanza kuendelea na Fainali za michuano hiyo huku mtoto mwingine ambaye Naye alikuwa na ushawishi mkubwa alikuwa Celine Tam ambaye kwa bahati yake hakufanikiwa kuchaguliwa kuelekea Fainali.
Tazama mchuono wa Mchujo ulivyokuwa hapa chini. VOA TV News .





0 Comments:
Post a Comment