![]() |
| Diwani wa Themi Mh. Melance Kinabo katika kikao cha kamati ya bodi ya shule ya msingi Themi akihudhuria kikao Maalum cha kamati inayojadili changamoto ya Choo cha walemavu ambapo alialikwa mfadhili. |
Shule ya msingi Themi imepata ufadhili mnono wa kujengewa vyoo vya kisasa kwa ajili ya wanafunzi wa watoto walemavu wa macho (vipofu).
Akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya shule hiyo Mfadhili Mama Isabela D. Mwampamba amesema ameguswa sana na ada wanayopata watoto hao walemavu, nakuahidi kujenga vitundu sita (6) vya choo kwa ajili ya watoto hao.
Kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa mbili tu kimejadili mambo kadha wa kadha lakini kubwa lilikuwa changomoto ya choo kinachomudu walemavu.
Watoto walemavu wamekuwa na hatari ya kupatwa na UTI , Pia wamekuwa wakikumbwa na hatari ya kudunbukia chooni.
![]() |
| Kutoka kulia ni Diwani wa Themi Melance Kinabo Katikati ni Mfadhili Bi. Isabela Mwampamba. |












0 Comments:
Post a Comment