HABARI: Mamia waandamana St.Louis kupinga Mahakama kumwachia polisi alimuua raia wa Marekani mwenye asili ya uafrika.

Maandamano ya mamia ya watu yameendelea leo katika mji wa St Louis nchini Marekani, kupinga hukumu ya mahakama iliyoamuru polisi mzungu aliyemuua mtu mweusi mwaka 2011 kuachiwa huru.

Maandamano hayo yaliyoanza siku ya ijumaa baada ya hukumu hiyo kutolewa na mahakama, mamia ya watu katika mji wa Missouri leo wanatimiza siku ya tatu kuandamana wakisema kuwa maisha ya watu weusi hayatakuwa na thamani kama watamuachia mtuhumiwa huyo .
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la AFP, mpaka sasa zaidi ya waandamanaji 33 wamekamatwa na polisi huku polisi 11 wakijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Ijumaa usiku.
Polisi huyo aliyejulikana kwa jina la Jason Stockley 36, aliondolewa mashtaka mahakamani ya kumuua, Antony Lamar Smitjh 24 mwaka 2011.
Bwana Smith alikuwa baba wa mtoto mmoja na kwa mujibu wa Polisi huyo alidai kuwa Smith alikuwa anafanya biashara ya madawa ya kulevya.

0 Comments:

Post a Comment