BISIMBA AELEZA MAZITO WALIYOTETA NA LISSU

Leo Mungu amenipa neema kumuona Mh. Tundu Antipas Mughway Lissu nimeuona kwa macho muujiza kuwa Tundu pamoja na marisasi yale yote ameniona na kuniamkia nakunipa pole. Yaani yeye ndio anatupa sisi moyo kuwa Kufa mtu hufa mara moja tusiogope kusimamia haki, kusema ukweli, kutetea wanaoonewa.

Nimepata nguvu mpya.Watanzania Tundu anawasalimu. Nimemuona anabariki.Mke wake mpenzi naye anaendelea na huduma kwa moyo mkuu ndiye niliye naye pichani.Waliotenda tendo lile wamrudie Mungu maana yupo tena yu hai na amewaonyesha ukuu wake. Mungu akamilishe uponyaji kwa Lissu.

*Helen Kijo Bisimba*

0 Comments:

Post a Comment