Korea Kaskazini imekamilisha mikakati yote ya Mpango wake wa Silaha za Nyukilia

Shirika la habari linalomilikwa na serikali ya Korea Kaskazini limesema nchi hiyo imefikia malengo yote ya kukamilisha uendelezaji wa nyuklia na makombora. 

Nchi hiyo imedai hivyo kwenye tahariri iliyochapishwa jana Jumamosi kwenye gazeti la Rodong Sinmun linalomilikiwa na Chama cha Wafanyakazi kinachotawala nchi hiyo. Tahariri hiyo inasema jukumu pekee lililobaki sasa ni kwa nchi hiyo kuonyesha ushupavu wake.

Waangalizi wanagusia kuwa kwenye tahariri hii ya sasa Korea Kaskazini imeashiria kuwa imepiga hatua zaidi kwenye uendelezaji wa silaha za nyuklia na makombora. 

Waangalizi hao wanasema Korea Kaskazini inazidi kuonyesha msimamo wake dhidi ya ziara ijayo ya Rais Donald Trump wa Marekani barani Asia.

0 Comments:

Post a Comment