Lowassa alivyomtembelea Lissu

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemtembelea hospitalini mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

 Mjumbe huyo  wa Kamati Kuu CHADEMA amefika leo kwe hospitali ya Nairobi anapopatiwa matibabu Lissu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 38 na watu wasiojulikana wakati akiingia nyumbani kwake mjini Dodoma mwezi uliopita.
Lowassa alifika hospitalini hapo akiwa ameambatana na Mke wake, Regina Lowassa na aliyekuwa mbunge wa Longido,  Onesmo Ole Nangole


0 Comments:

Post a Comment