Limefanyika Bonanza la CHAVITA la michezo katika kata ya Sombetini jijini Arusha kwa kucheza mpira Wa miguu kati ya timu ya mpira Wa miguu ya timu ya CHAVITA FC na mkeka FC.
Katika mchezo huo timu ya Mkeka Ilishinda Chavita FC bao 3 kwa moja huku washindi wakipokea jezi kwa kila timu.
Lupi Mwaisaka kaimu Mkurugenzi Wa chama cha Viziwi Chavita amesema mashindano hayo yalikuwa na lengo la kujenga ushirikiano baina ya jamii ya watu wasiosikia (viziwi) na jamii nyingine.
Mgeni rasmi katika Bonanza hilo alikuwa Mstahiki Meya wa jiji la Arusha ambaye aliwakilishwa na Madiwani James Lyatuu wa Unga Limited , Melance Kinabo wa Themi ambao waliisihi jamii kutowatenga viziwi huku wakiisihi jamii kuwa wasiwafiche viziwi wawalete karibu ili jamii iwe na mshikamano.

0 Comments:
Post a Comment