ACE-AFRICA Watekeleza Sera ya Rais Magufuli kwa Vitendo

Katika kutekeleza  juhudi za serikali ya awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kuwa Tanzania ya viwanda Shirika lisilo la kiserili la ACE - AFRICA limetoa msaada wa mashine ya kusagia na kukobolea nafaka kwa kikundi cha wajasiriamali cha Loluvo kijiji cha Oloitushula kata ya Musa kwa lengo la kufanya kiwanda cha usindikaji wa unga wa nafaka.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hiyo Meneja wa Idara ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ndugu Salumu Lubuva kwenye ofisi ya kijiji cha Oloitushula amesema kuwa shirika la ACE AFRICA linaunga mkono juhudi za serikali kwa vitendo kwa kuwezesha wananchi kujiunua  kiuchumi  ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2035 kwa Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Lubuva amesema kuwa shirika limetoa mashine kwa kikundi cha Loluvo yenye thamani ya shilingi 6,200,000/= kwa lengo la  kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kubadilisha maisha yao, familia zao na jamii kwa ujumla.

Amefafanua kuwa mashine hiyo inatakiwa kufanyika kiwanda cha kusindika unga na kuweka kwenye vifungashio na kuuza kwa wingi zaidi.

Aidha Lubuva amefafanua kuwa kabla ya kuwakabidhi mashine wajasiriamali hao walianza kwa kuwawezesha kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuweza kuendesha biashara ikiwa ni pamoja na  kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi, kutunza kuweka na kukopo, masoko na kuziona fursa. 

Hata hivyo Lubuva amewaasa wajasiriamali hao kusimamia vizuri mradi huo kwa endapo watashindwa kuendeleza mashine hiyo itanyang'anywa na kupeleka kwa wahitaji wengine na zaidi amewataka wajasiriamali  hao kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za migogoro ya kuendesha biashara ya pamoja kwenye vikundi.

"Inapotokea kutokuelewana ni  vema kukaa na kuzungumza kwa kushirikisha viongozi wa kata na kijiji pamoja na shirika letu ili kutatua mgogoro na kusonga mbele" amesema Lubuva

Naye mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi shirika la Ace Africa ndugu John Emanuel amesema kuwa wametoa mashine hiyo ili ifanyike kuwa  kiwanda kidogo ambapo licha ya kutoa huduma ya kusaga na kukoboa nafaka za wananchi wanaowazunguka wanapaswa kwenda mbele zaidi kutengeneza unga kwa kufunga kwenye mifuko na kuuza ndqni na nje ya kata ya Musa.

"Mradi huu wa mashine muufanye kuwa kiwanda cha kusindika  na kupark  unga ili  kuuza ndani na nje ya kata ya Musa hata mkoa mzima wa Arusha na Tanzania nzima" amesema John

Mwenyekiti wa kikundi cha Loluvo ndugu Upendo John ameonesha furaha yake na kukiri kuwa mashine hiyo ni mkombozi  wa kujikwamua kiuchumi na jamii ya wananchi wa Oloitusha.

Aidha amefafanua  kuwa  licha ya kuwa mashine hiyo kuwapatia fedha za kuinua vipato lakini pia mashine hiyo itawezesha kusaidia jamii yao kupata huduma ya kusaga na kukoboa karibu  zaidi tofauti na hapo awali huduma ya mashine haikuwepo kijijini hapo.

"Hii ni kiwanda kidogo mashine imekuja kutukomboa kwa kuwa tumekuwa tukipata huduma ya kusaga umbali wa zaidibya kilomita kumi,  tunaenda kusaga Nengun'gu  kule Monduli au Kisongo madukani sasa huduma ipo nyumbani" amesema mwenyekiti huyo

Evaline Wlison mwanakikundi amethibitisha kuamini kuwa mashine hiyo itawakwamua kiuchumi na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kufikia malengo waliyoyakusudia wakati wa kuomba msaad huo wa mashine.

Aidha  Shirika la Ace Africa linategeme kutoa mashine tatu ikiwa mashine mbili zimeshatotolewa moja kwa kikundi cha wajasiriamali wa kijiji cha Oloitushula na Ngorbob kata ya Matevesi na wanategeme kutoa mashine nyingine kijiji cha Olelosi kata ya Kimnyaki.

Shirika la Ace Africa linafanya shughuli mbalimbali za kijamii kwenye kata 12 za Tarafa ya Mukulat katika halmashauri ya Arusha ikiwa ni pamoja na uelimishaji wa Haki na ulinzi na usalama wa mtoto, Afya ya Lishe pamoja na uwezeshaji vikundu vya wananchi kiuchumi.

PICHA ZA MATUKIO YA MAKABIDHIANO YA MASHINE HIYO.



0 Comments:

Post a Comment