![]() |
| Kwenye Picha anaonekana Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure mstahiki Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro. |
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure amesema chama hicho tayari kimeonesha dalili za kushinda kwenye chaguzi za marudio nchini ambazo zinafanyika kwenye Kata 43 nchini kote.
Akizungumza na waandishi wa Habari napema kwenye ofisi za chama hicho kanda ya kaskazini Mungure amesema shughuli za kampeni za chama hicho zimekuwa na mwitikio Mkubwa kwa Wananchi.
Katibu wa mkoa Mungure ametaja asilimia za ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi wa marudio hususani kwenye Mkoa huu wa Arusha ambapo amesema kwenye kata ya Muriet iliyoko katika jiji la Arusha Chama hicho kinategemea kushinda kwa asilimia 90% , Ngabobo asilimia 85% Huku Ambureni ikitajwa kuwa asilimia 95% kupata takwimu za kata zingine zaidi unaweza kuplay hii video hapa chini.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akailalamikia serikali kuhusu mchakato kuelekea siku ya uchaguzi kwamba kumekuwa viashiria vya uvunjifu wa amani. Tazama video hapa kumsikia Lema


0 Comments:
Post a Comment