BREAKING NEWS: Mgombea Udiwani Muriet Kupitia NRA Ajiuzulu na kukiunga mkono CHADEMA

Mgombea Udiwani Muriet kwa tiketi ya chama cha NRA ajiengua kwenye kinyang'aro hicho nakumuunga mkono Mgombea Udiwani wa Chama cha demokrasia CHADEMA Ndugu Simon Moses Mollel.

Mgombea huyo amesema sababu ya kujiuzulu mwake ni kwamba viongozi wake wakuu wa chama Sana ukaribu wa kikazi na chama cha mapinduzi CCM huku akidai wamemtelekeza yeye kataika harakati nzima ya Kampeni kuelekea 26/November siku ya uchaguzi.

Aidha alizidi kufafanua kuwa njia pekee yalufanya ikawa kujiengua katika kinyang'anyiro hicho na kuiunga mkono chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Hata hivyo alipoulizwa iwapo kama ameandika barua ya kujiuzulu rasmi Mgombea huyo amsema ameshaiandika barua hiyo Leo tarehe 21/011/2017 nakumfikishia Msimamizi Mkuu wa uchaguzi kata ya Muriet.

Ikumbukwe zimebaki siku tano tu kueleke uchaguzi Mdogo wa Marudio Muriet nabkatika kata mbalimbali nchini ambako kunafanyika uchaguzi Mdogo wa marudio.

Zaidi unaweza kuplay Hii vedeo hapa chini kutoka VOA TV News 

0 Comments:

Post a Comment