Wafuasi 12 wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mawili ya shambulio la kawaida na kufanya fujo Novemba 3 katika mahakama ya mwazo ya maromboso jijini Arusha.
Wakisomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Obadia Mongi mwendesha mashtaka wa polisi Pc Nasoro amesema washtakiwa hao kwa pamoja wali wanashtakiwa kwa makosa hayo na kusababisha maumivu makali kwa malalamiko Jirani Juma Jumanne
Shtaka la kwanza ni Fujo ambapo washtakiwa hao akiwemo katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini Innocent Kisanyage kwa pamoja mnamo November 3 mwaka 2017 SAA 11: 45 jioni eneo la kwamurombo walimfanyia Fujo mlalamikaji jumanne.
Baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa walikana shtaka hilo kwa pamoja na kusomewa shtaka la pili ambalo ni shambulio la kawaida ambapo siku hiyo na tarehe hiyo baada ya kumfanyia Fujo mlalamikaji waliwapiga mateke na kumsababishia maumivu makali sana kosa ambalo ni kinyume cha sheria.
Washtakiwa hao kila mmoja walikana shtaka hilo na ndipo hakimu alitoa masharti ya dhamana ambayo iko wazi kwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili nakala ya barua inayotambulika na serikali ya Mtaa pamoja na kila mmoja kuwekewa bondi ya shilingi laki 6.
Hata hivyo washtakiwa hao wametakiwa kurudi tena mahakamani hapo 16 .11.2017 ili kusomewa mashtaka yao.
Washtakiwa hao ni pamoja na Katibu wa Mbunge,Innocent Kisanyange (28) ,Edwin Christopher (30) Pascal Lucas(25) ,Nasoro Ally(25),Godson Samwel (34)Joram Baraka (24) Balozi Shana (37), SesiliaLucas (27) ,Aureria Lucas(21), Rehema Juma(26),Amina Musa (18) na Yohani Michael (33)

0 Comments:
Post a Comment