LOWASSA Aionya CHADEMA Kumtaja taja Gambo "..Anapata umaarufu.."

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimeendelea na mkutano wake wa kampeni za chaguzi Mdogo za marudio nchini.

Kwa Mkoa wa Arusha chama hicho Leo kimefanya mkutano Mkubwa wa kampeni katika uwanja wa mpira wa kijiji cha Makiba. 

Mkutano huo pamoja na kuhudhuriwa na maelfu ya Wananchi wa kata ya Makiba kwenye jimbo la Uchaguzi la Arumeru Mashariki linaloongozwa na Mbunge mwenye umri Mdogo Joshua nasari umehutubiwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa.
Lowassa amesema Taifa linahitaji katiba mpya ili kuweka uwiano baina ya raia. Amesisitiza kuwa taifa linahitaji kuwa Moja masuala yanayodaiwa ya ukabila hayafai kwa  taifa la watu wanaopenda amani.

Lowassa pia ameitaka chama cha demokrasia na maendeleo chadema kutomtaja taja Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwani kwa dhana hiyo kinampatia umaarufu.

Chadema kimekuwa kikimlaumu Gambo katika masuala mbalimbali.

Aidha Lowassa ameuambia umati  wa maelfu ya watu kuwa Chama cha mapinduzi kinapaswa kujenga umoja na amani kwa watanzania kama chama kinachoongoza  kuliko kuwagawa kikanda na kikabila kama inavyodaiwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari akamnadi Mgombea Udiwani kata ya Makiba Mwanamama Joyce Lutha huku mwana mama huyo akionekan kuwa na ushawishi Mkubwa.

Akijinadi Mgombea Udiwani Makiba Joyce Lutha akaipa kipaumbele chake kwenye Soko katika kata hiyo, Huduma bora ya afya na miundombinu ya barabara.  

Kuhusu soko Joyce Lutha amesema kata hiyo Haina soko kabisa hivyo jukumu lake la kwanza ni kujenga Soko ili kukuza pato la ndani la Halmashauri.

Huku kingine  kikiwa Huduma ya afya ambapo haina umeme na barabara ya kuifikia kituo hicho.

Chama hicho kinaendelea na mikutano take ya kampeni nchini hadi November 25 Mwaka huu ambapo 26 November kunatarajiwa kufanyika uchaguzi.

Naye Mbunge wa Simanjiro James Milya amesema Sana Makiba wana sababu zote za kumchagua Joyce Lutha kwa sababu ameonesha uwezo wa kuwatumikia wakazi Makiba huku akishi nao kwenye kata hiyo.

Milya kabla ya kumnadi Mgombea huyo akaeleza sababu za wananchi kuikimbilia CHADEMA ikiwa ni pamoja na kuwa Chama hicho kina dhamira halisi ya maisha ya watanzania na siyo CCM .

0 Comments:

Post a Comment