Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini(CCM) Lazaro Nyalandu ambaye wiki iliyopita alijitoa katika chama hicho, Jumanne wiki hii amemtembelea waziri mkuu wa zamani na Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA, Edward Lowassa ofisini kwake(oval) Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Nyalandu amemshukuru Lowassa kwa kuonesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM,”mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,".
Kwa upande wake Lowassa ambaye alitoka CCM 2015 alimkaribisha Nyalandu upinzani na kumweleza," nimefarijika kuja huku karibu sana tushirikiane na kwa hakika 2020 tutavuka daraja(tutashinda),".

0 Comments:
Post a Comment