AVE YAKABIDHI MILIONI 15 KWA VIKUNDI VYA LEVOLOS

Mkurugenzi wa Umoja wa VICOBA Arusha, (AVE),   Grace Macha akikabidhi nakala ya mhamala wa Benki inayoonyesha fedha zimewekwa kwenye akaunti ya vikundi husikia kwa Afisa mtendaji wa mtaa wa Levolosi, Cecilia Ngowi  ambaye alimwakilisha afisa maendeleo kata hiyo.

Umoja WA Vicoba Arusha, (AVE) umekabidhi shilingi milioni 15 Kwa vikundi vitatu vya wanawake na vijana vya kata ya Levolos.

Fedha hizo ni za halmashauri ya jiji la Arusha ambapo AVE amepewa jukumu la kusimamia fedha hizo kwa kata hiyo.

 Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi ya kata ya Levolosi ambapo vikundi vilivyopatiwa mkopo huo ni kikundi cha kinamama cha Baraka na vikundi viwili vya vijana vya Watano na Levolos native Association.



Afisa mtendaji, Ngowi akikabidhi hati ya mhamala wa benki kwa mwakilishi wa kikundi cha kinamama cha Baraka.



 Grace aliwataka vikundi vinakabidhiwa mikopo hivyo viwe vinazingatia muda wa marejesho na kuwataka viongozi na wanavikundi hivyo kuwa na desturi ya kufuatiliana kwa karibu ili kuhakikisha kila mmoja anatumia fedha hizo kama ilivyokusudiwa.

Grace Macha Mkurugenzi wa Arusha Vicoba Empowerment Ltd. Akifurahia jambo na vikundi vya Kijasiriamali Kwenye hafla fupi ya kupokea Fedha za mikopo kutoka kwa kampuni hiyo.
Aidha Bi. Grace akasisitiza kuwa moja ya umuhimu wa kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ni kuwezesha vikundi vingine ambavyo vimepitishwa na Kata baada ya kuwa na sifa viweza kupata mikopo  kwa wakati.

Wanachama wa Vikundi hivyo wakijadiliana machache baada ya kukabidhiwa stakabadhi ya malipo kutoka kwa kampuni ya Arusha Vicoba Empowerment Ltd.

0 Comments:

Post a Comment