MUNGURE Kaeleza Hali ya Majeruhi Wafuasi wa CHADEMA walioshambuliwa Siku moja kabla ya Uchaguzi wa Marudio Arumeru Mashariki

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Elias Mungure ametueleza machache kuhusu hali za wafuasi wa chama hicho waliojeruhiwa hivi karibuni kwenye Mchakato wa Chaguzi za Marudio.

Hilo limejiri kwenye jimbo la uchaguzi la Arumeru Mashariki katika kata ya Makiba  "Leo Jioni hii baada ya kuwapeleka waanga walioshambuliwa na crew ya CCM Makiba Usiku wa kuamkia Uchaguzi Hosipitalini, Wamepata matibabu na mmoja ameruhusiwa,Mmoja bado yuko hosipitali ya Mbuguni na hali yake ni Mbaya Bado,mmoja amelazwa Tengeru Hospital,Mmoja ambaye ni M/kiti wa Tawi Makiba Nixoni Mbise CHADEMA tuko naye kwa usalama maana aliwataja wauwaji kwenye clip ambayo iko kwenye mitandao akiwa Hosipitalini.Amepata matibabu sana Lakini Kesho tutampeleka kwenye Matibabu Hosipitali yenye X-RAY maana Hapa Tengeru hakuna.
  Yuko imara Sana japo anaumwa sana.Jioni hii RCO wa Mkoa na OC CID wamekuja kuchukua maelezo yake na tuko nao.
  Hii ni baada ya kuona kwenye mitandao Chadema tumechukua hatua ya matibabu kwa waanga wa shambulio." Mungure

0 Comments:

Post a Comment