MUNGURE Kuwaburuza RC Gambo na RC Mnyeti Mahakamani , Nape , Kinana waponea Chupu Chupu

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Elias Mungure akimnadi Mgombea Udiwani kata ya Makiba Joyce Lutha

Wakati kampeni za Uchaguzi Mdogo zikielekea ukingoni mwa siku ya uchaguzi ambayo inatarajiwa hapo jumapili ya 26/November Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefanya mkutano wake wa mwisho kwenye kijiji cha Makiba iliyoko kata ya Makiba jimboni Arumeru Magharibi.

Mkutano huo umefanyika ikiwa ni siku moja tu baada ya kufanyika mkutano wa Chama cha mapinduzi CCM kwenye kata hiyo. 

Katika mkutano uliofanyika Leo wa CHADEMA agenda kubwa imekuwa uelimishwaji wa wapiga kura, kumnadi Mgombea wa Udiwani kata hiyo Joyce Lutha, Na miradi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati , ofisi za kata , changamoto za elimu, uhitaji wa umeme na miundombinu ya barabara.

Aidha Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Elias Mungure akafafanua sheria za uchaguzi pamoja na kuainisha jinsi ambavyo amedai viongozi wa umma hasa wateule wa Serikali iliyoko madarakani Wakuu wa mikoa , na viongozi wengine wanavyovunja sheria za uchaguzi kwa kujihusisha na kampeni kinyume cha sheria za nchi.
Mungure amesema Kitendo cha viongozi wa serikali kukibeba chama cha mapinduzi ni kinyume cha sheria huku akisisitiza kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria kwa kuwapeleka mahakamani viongozi ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakishiriki kuibeba chama cha mapinduzi CCM.

Tazama hii video fupi kutoka VOA TV News.

Chama cha mapinduzi Jana kilifanya mkutano wake wa kampeni kwenye kata Makiba ambako kunadaiwa ulikuwa mkutano uliozingwa na matusi dhidi ya viongozi wa upinzani akiwemo Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nasari . 

Mkutano wa Chama cha mapinduzi uliohudhuriwa na Katibu wa chama hicho taifa Abduraman Kinana ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Gambo Mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye. Ambapo inadaiwa mkutano huo uli gubikwa na matusi yaliyoelekezwa kwa Mbunge Joshua Nasari. 

Katika hatua nyingine Mungure amemshangaa Katibu Mkuu CCM Taifa Abduraman Kinana kwa kuwaacha  Viongozi kutukana matusi huku yeye akishuhudia. 

Mungure amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kuacha kuvuraga uchaguzi unaotarajiwa kufanyika November 26 akidai huu siyo Mkoa wake yeye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara . 

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru Welly Njau amesema siyo jambo zuri kwa viongozi kutukanana matusi ya nguoni hadharani na kwamba viongozi watumie lugha ya maendeleo huku akiwataka Wananchi wa Makiba kuichagua CHADEMA kwani ndicho chama pekee kinachoweza kuleta mabadiliko kwenye kata hiyo.

Njau aliorodhesha miradi ya muhimu inayohitajika kwa haraka katika kata hiyo imetengewa zaidi ya Millioni mia saba  kwa ajili ya Maendeleo ya kata hiyo kwa sekta ya Kilimo cha umwagilaji ukarabati wa madarasa na nyumba za watumishi kwenye vituo vya afya. 

Zimebaki siku mbili kuelekea kilele cha uchaguzi Mdogo wa marudio nchini ambapo November 26 kunatarajiwa kufahamika mbivu na mbichi kwenye kata zote 43 kulizosimamishwa wagombea Udiwani. Vyama vya CHADEMA ACT-Wazalendo , CCM , NRA na vyama vingine vinashriki katika uchaguzi huo.

Hapa chini IPO Video Inayonesha Mungure akifafanua jinsi alivyoshtaki Mkurugenzi wa Meru DC kuhusu tuhuma za uwizi wa kura na barua take hiyo kujibiwa na Time ya Taifa ya Uchaguzi kwa kumtaka Mkurugenzi huyo kutojihusisha na Mchakato wote wa uchaguzi.

0 Comments:

Post a Comment