UPDATESzaUCHAGUZI: Halima Mdee, Ester Bulaya Waivuruga Arumeru Mashariki, Maelfu ya wakazi wafurika

Maelfu ya wafuasi wa CHADEMA Walifurika kwenye kampeni za Chama hicho katika kata ya Makiba jimbo la Arumeru Mashariki.

Kampeni za uchaguzi mdodo wa marudio unaendelea maeneo mbalimbali nchini ambapo vyama vya CHADEMA , CCM na ACT-Wazalendo vimewatambulisha na kuwa nadi wagombea wao.

Leo kwenye kata ya Makiba Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha kumefanyika mkutano wa kampeni za chama cha demokrasia na maendeleo mkutano uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa kata ya Makiba kuwasikiliza viongozi wa Chadema taifa , Mkoa Wilaya na Mgombea Udiwani kata hiyo Bi. Joyce Ritha.

Mkutano huo ulikuwa tofauti na mikutano mengine ya siasa za chama hicho kwani kipekee ulihudhuriwa na mwenyekiti wa baraza la wanawake LA chama hicho Taifa Mh. Halima Mdee , Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya ,Katibu wa Mkoa wa chama hicho Mh. Elias Mungure na mwenyeji Mbunge wa jimbo la Uchaguzi la Arumeru Mashariki.
Kingine cha kufahamu na cha kipekee katika mkutano wa kampeni wa Chadema ni kuwa Mgombea wa kiti cha Udiwani kata ya Makiba ni Mwanadada Joyce Rutha ambaye anaonekana kuwa na ushawishi Mkubwa.

Awali Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha akiratibu mikutano hiyo Elias Mungure alisema Chama hicho siku zote kimekuwa chama makini katika utendaji wake hivyo wananchi waendelee kukiamini na kumpigia kura Mgombea Udiwani kata hiyo Mwanadada Joyce Rutha.

Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya alihutubu akiwaeleza wana Makiba kuwa kumchagua Mwanamke ni ishara ya maendeleo kwa jamii iliyoendelea. Bulaya pia alieleza jinsi yeye alivyoweka historia mkoani Mara kwa kuwa Mwanamke wa kwanza Mbunge na kuwashinikiza Wakazi wa kata Ya Makiba kumchagua Joyce Rutha kuwa Diwani wao.
Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima Mdee akipokea wanachama aliyekihama chama cha mapinfuzi na kuingia CHADEMA Leo.

Aidha Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima Mdee akashika stage na kuhutubu huku akielekeza nguvu kubwa ya hotuba yake kuuchambua utawala wa Rais Magufuli na kwamba ni utawala unaokiuka Haki za kisheria.

Halima Mdee aliwaeleza wakazi hao kuwa wasikubali kudanganywa danganywa kwa kuambiwa maneno maneno ambayo ni ameyaita ya kidanganyifu.

Kwa upande wake mwenyeji wa mkutano huo Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasari (Dogo Janja) akafafanua kinagaubaga cha kujiuzulu kwa aliyekuwa Diwani wa kata hiyo , huku akifafanua kuwa na kuwa mzalendo na kumkejeli kuwa ni Mwanaume aliyeolewa kwa mahari ya shilingi Millioni mbili.

Joyce Rutha Mwanadada Anayeonekana kuwa mahiri akajinadi kwa mbwembwe huku akitanabaisha Yale ya muhimu atakayoyafanyia kazi kipindi atapokuwa Diwani wa kata ya Makiba.

Joyce Rutha amesema kata ya Makiba inakabiliwa na Changamoto chungu nzima ikiwa ni pamoja na Tatizo sugu la maji , Afya , elimu na Kuahidi kujenga Barabara inayopitika nyakati zote za majira ya mvua na kiangazi.
Mkutano kama huo unatarajiwa kufantika tena hapo Jumanne 21/November katika kata hiyo hiyo ya Makiba huku kukiwa na taarifa kuwa utahudhuriwa na aliyekuwa Mgombea urais Tanzania , Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa na Waziri mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowassa.

0 Comments:

Post a Comment