![]() |
| Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (Kulia) na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa |
Waziri Mkuu mstaafu na mjumbe wa Baraza kuu la chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Edward Lowassa ameshiriki katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Marudio kata ya Mororoni Arumeru Mashariki.
![]() |
| Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoani Arusha Mh. Amanj Golugwa |
Mkutano huo wa kampeni uliofurika maelfu ya watu ulihudhuriwa pia na uongozi wa chama hicho kikanda ukiongozwa na Katibu wa Chama hicho Kanda ya Kaskazini na mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Amani Golugwa , Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure na viongozi wengine.
Awali akihutubia Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nasari aliwaeleza wakazi wa Kata hiyo Kuwa ni baada ya kukiuzulu kwa aliyekuwa Diwani wa kata hiyo hata hivyo Nasari Ambaye ana ushawishj Mkubwa katika jimbo hilo alifafanua kinagaubaga cha vitendo vya kurubuniwa kwa madiwani wa chama hicho.
Nasari amefafanua kwa undani mchakato mzima tangu ulipoanza hadi ulipo malizika.
Aidha Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Amani Golugwa aliwataka wananchi wa Mororoni kufanya maamuzi sahihi ifikapo 26 November huku akiwapa pole kwa Diwani aliyejiuzulu. "..Niwape pole kwa mtoto huyu ambaye hakuwa riziki.."
![]() |
| Umati Mkubwa wa wafuasi wa CHADEMA walipokuwa wakimlaki Lowassa. |
Kwa upande wake Edward Lowassa aliwasisitizia wana Mororoni kwamba wasifanye makosa siku ya uchaguzi kwa kumchagua Bw. Mbise anayewania kiti hicho cha Udiwani Mororoni.
Licha ya kunyesha mvua kubwa wananchi walikomaa wakisubiri kile watakachosema viongozi wa CHADEMA waliofika Kwenye kata ya Mororoni.
- Pamoja na kuwashukuru kwa kumpigia kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Mh. Lowassa aliwashukuru wakazi hao kwa mapokezi makubwa waliomfanyia Leo.
Tazama video hapa alichoongea Lowassa.
PICHA KATIKA MATUKIO PALIPOFANYIKA MKUTANO WA KAMPENI ZA CHADEMA KATA YA MORORONI ARUMERU MASHARIKI.
![]() |
| Dakika chache akihutubia Lowassa katika mkutano huo Kushoto Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari wa pili kulia ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Elias Mungure. |
![]() |
| Nyomi ya watu waliohudhuria mkutano wa kampeni za uchaguzi Mdogo wa CHADEMA kata ya Mororoni. |
![]() |
| Wananchi wakimsalimia Lowassa baada ya kumaliza Hotuba yake fupi. |
![]() |
| Wananchi walivyozingira Gari la Mh. Lowassa wakati akiondoka katika kata ya Mororoni akikamilisha mkutano wa kumnadi Diwani anayepeperusha Bendera ya CHADEMA katika uchaguzi wa marudio. |
![]() |
| Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Taifa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Mororoni. Kulia ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Elias Mungure |












0 Comments:
Post a Comment