WAKILI MWALE AREJESHWA TENA MAHAKAMANI

WAKILI maarufu jijini Arusha, Median Mwale na wenzake watatu wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha muda huu wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Wakili Mwale na wenzake, Don Bosco Gichana raia wa Kenya, Boniface Mwimbwa na Elias Ndejembi, walikamatwa jana na polisi muda mfupi baada ya mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuwaachia huru baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, (DPP) kuamua kuliondoa shauri hilo mahakamani.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea, David Mrango aliwaachia huku akisisitiza kuwa kama wanaliondoa shauri hilo kwa nia njema basi wasiwakamate tena kwani tayari washitakiwa hao walishasota magereza Kwa zaidi ya miaka sita sasa.



Awali wakili wa utetezi, Albert Msando aliwasilisha pingamizi akitaka mahakama isikubaliane na maombi ya DPP kwani alitakiwa kutoa sababu za kutokuendelea na kesi hiyo nawalikuwa na muda wa miaka miwili kufanya hivyo lakini hawakuwa ya Jambo alilodai kuwa kinachofanyiia  ni matumizi mabaya ya sheria.

DPP ameanda polisi  ndani na nje ya mahakama waliovalia sare na ambao hawajavalia sare na magari hapo nje ili wakiondoa hii kesi,wawakamate watuhumiwa na kuwafungulia tena kesi upya,"alisema na kuongeza


"Tangu Agosti 2011 watuhumiwa hawa hawajawahi kuwa nje ya gereza labda wakiletwa mahakamani na hii siyo mara ya kwanza DPP kuondoa kesi na kufungua upya.Tunataka haki hivyo kesi hii isikilizwe kwani sheria haipaswi kutumika kuadhibu watuhumiwa kama wanavyofanya sasa,kuwanyanyasa watuhumiwa,"


Akijibu hoja hizo  wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya,alipinga hoja hizo kwa madai sheria haimlazimishi DPP kutoa sababu ya kuondoa kesi mahakamani pindi akiona kuna haha ya kufanya hivyo.

Kwa upande  madai ya Wakili wa utetezi kuwa DPP ameandaa polisi ili wakiondoa kesi hiyo washitakiwa  wawakamate tena alisema haiwezi kujibu hoja hiyo kwani inahitaji ushahidi.


Hii ni kara ya pili kwa DPP kuondoa shauri hilo mahakamani ambapo Novemba 23 mwaka 2015,shauri hilo liliondolewanna washitakiwa hao kukamatwa na polisi na kufunguliwa kesi upya.

Wakili Mwale na wenzake, walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 44 yakiwamo ya utakatishaji fedha haramu, kughushi nyaraka na kukutwa na mali zilizopatikana kwa njia za uhalifu ambapo shauri hilo likifika mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosto, 2011.

Endelea kuperuzi ukurasa huu nitawahabarisha zaidi

0 Comments:

Post a Comment