DANIEL AWAKI Ashinda kwa Kishindo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa


Chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha nimefanya uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa kutoka Wilaya za Mkoa huo, Mjumbe wa  Halmashauri kuu ya Taifa Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa Mkoa wa chama hicho.

Katika uchaguzi huo Amechaguliwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Ambapo ameshinda Mh. Loota Sanar ambaye amemgaragaza mpinzani wake ndugu Lekule Laizer

Hata hivyo Kwa upande wa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa akiiwakilisha chama hicho kwa Mkoa wa Arusha ameahinda Mh. Daniel Awaki ushindi wa Awaki umehesabiwa kama ushindi wa kishindo kiwango cha alipotajwa ukumbi huo ulishabikia kwa bashasha zakutosha.

Chama hicho kimesema zoezi lililobaki ni kuhakikisha kinashiriki kwenye uchaguzi Mdogo wa maruduo nakushinda nafasi zote kwa kishindo. Uchaguzi wa Marudio umeitishwa kwenye Majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini, Longido na kwenye kata ya Kimandolu jijini Arusha.

0 Comments:

Post a Comment