Mkuu wa Wilaya ya Arusha DC Gabriel Daqqaro pamoja na Naibu Waziri Wa TAMISEMI George Joseph Kagunda
Naibu waziri wa Tamisemi George Kagunda,amehitimisha ziara yake huko Mkoani Arusha kwakupongeza jitihada zanazofanywa na Halmashauri za mkoa huo.
Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Arusha,Kagunda amesema ametembelea wilaya za Ngorongoro,Meru,Monduli na Arusha na kujiridhisha na miradi ya serikali inayoendelea katika Halmashauri hizo.
Kagunda ameendelea kusema Serikali ilitoa fedha kiasi cha billioni ishirini na mbili nukta tano(Billioni 22.5) kwa lengo la kutekeleza kazi mbalimbali ndani ya jiji hilo,zikiwemo za mfuko wa barabara billioni mbili nukta moja (billioni 2.1) ambazo zimetumika katika barabara za amjini kwa kiwango cha lami,barabara za changarawe,mitaro na barabara korofi.
Aidha Kagunda amelisemea tatizo la uhaba maji na maji yenye madini ya Floride katika baadhi ya maeneo nchini , suala ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa jamii inayotumia maji hayo hususani katika maeneo ya mkoa wa Arusha , manyara , Singida na Simiyu.
Kagunda amezisemea changamoto hizo kwakuwataka wananchi wote wenye visima vya maji,kupeleka maji hayo maabara ili kuidhinishwa kwa matumizi ya binadamu.

0 Comments:
Post a Comment