SPIKA WA EALA ALIVYOPATIKANA KWA MBINDE

HATIMAYE mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Rwanda, Martin Ngoga  ameapishwa kuwa Spika wa bunge la nne baada ya kuibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi hiyo ya juu kwenye chombo hicho cha uwakilishi.

 Ngoga ambaye alikuwa mgombea pekee aliyekuwa ukumbini wakati wa zoezi la upigaji kura lilipofanyika alipata kura  35, akifuatiwa mbunge kutoka Burundi, Leontine Nzeyimani aliyepata Kura moja huku mgombea kutoka Tanzania,  Adam Kimbisa akiambulia sifuri.

Hata hivyo zoezi hilo la kijinadi, kuomba na upigaji kura  lilifanyika wakati wabunge wa Tanzania na
Burundi wakiwa hawapo kwenye ukumbi wa bunge kwani wamesusia zoezi hilo.

Hivyo kura hizo zilipigwa na wabunge wa Kenya, Uganda, Rwanda na Sudani ya Kusini.

HALI ILIVYOKUWA KABLA YA ZOEZI LA UPIGAJI KURA

Mabishano makali ya kisheria yameibuka kwenye bunge la Afrika Mashariki,(EALA) baina ya wabunge wawili wa Tanzania walioingia bungeni na wabunge kutoka Kenya, Uganda,Rwanda na Sudani ya Kusini.

Mabishano hayo yalitokana na hoja iliyotolewa na mbunge wa Tanzania Ngwaru Maghembe na Makame waliotaka bunge liahirishwe kwani akidi haijatimia kutokana na wabunge wote wa Rwanda kutohudhuria huku kwa upande wa Tanzania wakiwa wao wawili ambao ni chini ya idadi inayotakiwa ya walau wawe wabunge watatu kutoka kila nchi.

Mbunge kutoka Uganda Mbidde alipinga hoja hiyo akidai kanuni zinasema wabunge wateule  watachagua spika mara baada ya kuapishwa na haizungumzii suala la Akidi hivyo akamtaka Katibu wa bunge,

Burundi walieleza hawaridhishwi na namna uchaguzi wa spika unavyoendeshwa hivyo wakaamua kupunguza mchakato huo hivyo nadhani si vizuri kuendelea ni vema tukasikia kutoka kwa wabunge hawa wanahitaji kupewa ufafanuzi zaidi ili tuweze kwenda pamoja

USHAURI  WA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAWAZIRI  WA EAC WATUPWA


Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, Alhaji Kirunda Kivenjinja alishauri kikao hicho kiahirishwe mpaka wakuu wa nchi zinazounda jumuiya hiyo wakutane kupatia ufumbuzi utata wa nchi gani inapaswa kushika nafasi ya spika.

Alidai njia hiyo ndiyo itawezesha jambo hilo kupatiwa ufumbuzi baada ya wabunge hao kufikia maridhiano.

Amesema usiku kucha alifanya mawasiliano na mawaziri wenzake waliopo bungeni pamoja na mwenyekiti wa wakuu wa nchi, Museveni ambaye alimshauri suala hilo lijadiliwe na kufikiwa maridhiano ya pamoja na wabunge lakini kwa kuwa imeshindikana basi ni vema suala hilo likajadiliwa na wakuu hao wa nchi.


Alisema Awali Burundi walipeleka  pertition kwa mwenyekiti wa wakuu wa nchi wakitaka zoezi la kupata nchi ya kupata spika lizingatie alfabeti japo wakati huo hawakujua kama Tanzania watagombea.

Rais Museveni alimwambia mkataba wa kuanzishwa EAC uko wazi hivyo wabunge  wajadiliane  yafikiwe maridhiano ya pamoja ambapo alidai baada ya kuona yameshindwa kufikiwa hivyo ni vema suala hilo likarudishwa kwa wakuu wa nchi.

“Kwa kuwa bunge halisongi mbele suala hili lipelekwe kwa wakuu wa nchi wakalipatie ufafanuzi hivyo akaomba spika ahairishe bunge hilo mpaka wakati mwingine,” Kivenjinja.


Hata hivyo wabunge walipinga uamuzi huo kwa madai kuwa bunge ni chombo huru na hawako tayari kufanyiwa maamuzi na bunge.

Mbunge kutoka Uganda, Mbidde alinukuu vipengele mbalimbali vya mkataba wa kuanzishwa kwa EAC na kanuni za uendeshaji wa bunge hasa kikao cha kwanza ambavyo havizingumzii kuwa ni lazima akidi itimie wakati wa kupiga kura ya kupata spika.

Alisema kanuni hizo zinasema baada ya wabunge wateule watakaopenda watapiga kura ya kuchagua spika jambo alilodai kuwa hivyo hao wabunge waliosusia kuingia kupiga kura hawawezi kuzuia zoezi la kupiga kura.

Mbunge Kutoka Uganda, Nakauki alipinga hoja ya Mwenyekiti wa baraza la mawaziri kwa kile alichoeleza kuwa bunge ni chombo huru kinachojitegemea kwani tofauti na mawaziri ambao wameteuliwa wabunge wamepigiwa kura kuingia kwenye chombo hicho cha uwakilishi.

Alienda mbali akidai kuwa hawawezi kuchaguliwa kiongozi wa kuwaongoza na wakuu wa nchi hivyo akatoka uchaguzi ufanyike.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa nchi zote isipokuwa wabunge wawili wa Tanzania, Maghembe na Makame ambao walisisitiza zoezi la kupiga kura haliwezi kufanyika mpaka akidi itimie.

Katibu wa bunge Madette alitaka wabunge wafikie uamuzi kwa kupiga kura huku akiwataka wanaounga mkono hoja ya Mbidde kunyoosha mikono na wabunge wote wakanyoosha jambo lililowafanya wabunge wawili wa Tanzania waliokuwa ukumbini kutoka nje kuonyesha hawaungi mkono maamuzi hayo.


0 Comments:

Post a Comment