![]() |
| Mh. Melance Kinabo akisaini Mkataba wa mkopo huo. |
Diwani wa kata ya Themi jijini Arusha Mh. Melance Kinabo Leo amesaini mkataba wa mkopo wa shilingi za Tanzania Millioni kumi na Tano (Mill. 15) unaotolewa na Halmashauri ya jiji la Arusha kwa ajili ya vikundi vitatu kutoka kwenye kata hiyo.
Akisaini mkataba huo Diwani Kinabo amesema Jukumu lake ni kuwaelimisha Wananchi juu ya aslimia kumi ya fedha za serikali zinazotolewa kwa ajili ya wanawake na vijana.
Vikundi vitatu ambavyo Mzabibu, Kambarage Vicoba na Kikundi cha Jiongeze Kijana Vicoba Group Vimechukua mkopo huo ambapo kila kikundi kitatakiwa mupatiwa shilingi za Tanzania Millioni tano (Tsh Mill. 05).
Aidha Kinabo akawahimiza vijana kuchangamkia Fursa mbalimbali ikiwemo hilo la kuchukua mkopo kutoka Halmashauri ya Jiji ili kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla.

0 Comments:
Post a Comment