Kitu Kaongea Mungure Sakata la Maafisa wa CHADEMA Wanaokihama chama hicho

Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh. Elias Mungure amesema chama hicho hakitatetereka kufuatia wimbi la wanaokiahama chama hicho kuongezeka hivi katibuni ..

"Viongozi wenzangu wa Chama, Viongozi wa serikali wanaotokana  na CHADEMA, Makamanda wetu wapambanaji na wanachama wetu wote.

  Tuwapuuzie na kuwadharau wasaliti wanaojiuzulu kwa lengo la faida zao na kudhoofisha Chama.

   Tusiwajadili kabisa ila tuwapuuze na tujadili namna ya kujenga na kuhimarisha Chama na kuheshimu maamuzi ya vikao Vya Chama.

  Hakuna aliye maarifu sana kuliko CHAMA.Bora hawa waondoke mapema ili 2020 tuende wapambanaji safi tuikombowe Tanzania kutoka kwenye Uhuru wa Bendera kwenda kwenye Uhuru wa utu.

Wasaliti wote muda si mrefu watajuta sana baada ya kujua wamedanganywa.

   Tanzania ni yetu sote.Tuongeze mapambano.Freedom is coming soon."  Mungure

0 Comments:

Post a Comment