MBOWE AISHUKIA SERIKALI, ANENA MAZITO MUSTAKABALI WA UPINZANI

 Naomba kukiri kama mwenyekiti wa chadema kuwa mwaka 2017 ulikuwa mwaka mgumu sana kisiasa kwetu sisi baada ya uhuru wa Demokrasia kupata majaribu mengi sana. Freeman Mbowe

- Rais amekuwa mbabe na amewaruhusu wasaidizi wake nao wawe wababe, wananchi wanateswa na wanashindwa kuongea na hakuna mtetezi wao. Freeman Mbowe

- Vyombo vya dola kuanzia TRA, Polisi Usalama wa Taifa na wasimamizi wa uchaguzi wamegeuza wapinzani kuwa maadui wa taifa. Freeman Mbowe

- Kama serikali na CCM wanaamini upinzani ni hasara kwa nchi wana wingi wa kutosha katika bunge na wapitishe sheria wavifute

kinachouawa sio Chadema wala vyama vya upinzani bali kinachouawa ni taifa,

Vyombo vya dola vinatumia nguvu nyingi kuturudisha kwenye mfumo ambao tulishatoka zamani na dunia ilishatoka zamani

Haiwezekani mtu mmoja akawa ana mawazo ya kusifiwa kuliko mtu yoyote,

Wasaidizi wa rais nao wameanza kumuiga bwana mkubwa, mtu yoyote
akiikosoa serikali wanatokea wapambe kutoka vyama vya siasa, wanatokea wapambe kutoka polisi, uhamiaji, na TRA wanaanza kumshambulia aliyetoa mawazo yake



- Tunaitaka Serikali iharakishe uchunguzi wa makosa kwa wale ambao wameshikiriwa ili wapate haki yao ya kuhukumiwa ama kuachiwa huru kama watakutwa hawana hatia. Freeman Mbowe

- Vita ya ufisadi ingefanikiwa sana kama kusingekuwa na uonevu, ingepiganiwa kwa kufuata sheria na sio matamko ya Viongozi, Vita hii imeonea watu na kuwabagua watu. Freeman Mbowe

Viongozi wa dini wana uhuru wa kutoa mawazo yao, wana wajibu wa kusema, ni watu wanaoelea taifa hili kiroho

Hawa ndio rais anawaambia wamuombee, iweje akiambiwa atubu wanamshambulia mtu aanayetakiwa amuombee?

Maaskofu wasikate tamaa, Kakobe, Shao, Shoo, maaskofu wengine pamoja na mashehe na maimaMu waendelee, taifa linawahitaji

Sisi upinzani watukosoe pia wakiona tunafanya makosa, hatuwezi kuwa na chuki kutokana na mtu kutoa mawazo tofauti

- Huwezi kumshambulia kakobe mwenye wafuasi kama mtoto mdogo kisa tu amekwambia utubu kwa makosa uliyoyafanya. Freeman Mbow

- Toka 2010 Mimi kama mwenyekiti wa Chadema sijafanya siasa wala kuhudhuria mkutano wa hadhara nje ya Kampeni, hii sio haki. Freeman Mbowe

- Fomu za maadili tulisharudi kabla hata ya Rais Magufuli pamoja na wabunge wetu. Freeman Mbowe

- Neno uchochezi limekuwa kichaka cha kuficha maovu ya viongozi na tumeona waliokuwa wakiikosoa Serikali wanatishwa na hata kupotezwa kabisa lakini 2018 CHADEMA tutazidi kusema. Freeman Mbowe

- Nawaomba viongozi wote wa Dini wasikate tamaa kwa kutishwa au kunyanyaswa na wateule wa Rais pale wanapotoa Mawazo yao. Freeman Mbowe

Waandishi hampo salama pia, sio tu vyombo vyenu kufungiwa, sasa hivi unashughulikiwa wewe kama mwanadishi, ndio kilichomkuta Azory

Tunajua serikali ina mpango wa kupeleka muswada wa marekebisho wa sheria ya vyama vya siasa, ili haya tunayolalamikia ni kinyume cha sheria yawe sheria kabisa


- Leo umebaki muda mchache kuumaliza Mwaka 2017 na tutaanza Mwaka 2018 lakini tumepoteza Ndugu zetu, Jamaa na kuona wengine wakipigwa risasi lakini Serikali imekaa kimya. Freeman Mbowe

- Utendaji wa Chadema hivi sasa hauwezi kulinganisha na siasa za wakati wa Kikwete na wakati huu. Leo siwezi kuitisha mkutano wa hadhara Dar ambapo ni makao makuu ya chama changu. Freeman Mbowe

- Mpaka sasa gharama za matibabu mheshimiwaTundu Lissu ni Dola za Marekani 300,000. Hadi sasa Serikali, Bunge hawajatoa chochote japo waliahidi kufanya hivyo. Freeman Mbowe

- Ili mti ukue lazima majani yapukutike muda mwingine, karibia wote tumefuatwa lakini waliofika bei mapema wameondoka, na najua wataondoka wengi. Freeman Mbowe

- Serikali hii ni sugu kufanya matumizi nje ya bajeti ingawa tuna sheria ya bajeti ambayo inakataza matumizi ya fedha nje ya bajeti. Freeman 
Source JF

0 Comments:

Post a Comment