Siku moja baada ya Taasisi ya Kuzuia kupambana na Rushwa TAKUKURU kutangaza kutupilia mbali Ushahidi wa Video uliowasilishwa kwa Taasisi hiyo na Mbunge Joshua Nasari Leo Lema Kafunguka ya Moyoni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema Leo ofisini kwake Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amesema kitendo cha TAKUKURU kutupilia mbali Ushahidi wao ni kinyume cha Taratibu za kisheria za Taasisi hiyo muhimu.
Lema Amesema amesikitishwa sana Maamuzi yaliyofikiwa na TAKUKURU ya kutupilia mbali Ushahidi huo huku sababu ikiwa kwamba Ushahidi huo uliambatana na Siasa.
Aidha Iwapo kama Chama hicho kitachukua hatua gani Lema amesema TAKUKURU ilikuwa mahala pekee Pa suala kupata Ufumbuzi suala la Rushwa.
Katika hatua nyingine Lema Ameaisitiza kuwa huenda suala Hilo limepelekwa kwa mashinikizo. " Mkurugenzi wa TAKUKURU hayuko kazini kwa sababu ya Saluti .. Yupo kazini kwa sababu ya interest ya Taifa hili....." Alisema Lema

0 Comments:
Post a Comment