LISSU AWASILI UBELGIJI

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amewasili Nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi kufuatia majeraha ya shambulio la risasi mjini Dodoma miezi kadhaa iliyopita.

Lisu alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi kabla ya kwenda Ubelgiji taarifa za awali zimedai Lissu amefika Salama Ubelgiji nakupokelewa katika Hospitali ambayo jina halikutajwa.

Siku moja kabla ya kuondoka Mwanasiasa Huyo wa upinzani Hapa Tanzania aliongea na Vyombo vya Habari kueleza mwenyewe hali ya Afya yake baada ya matibabu ya karibu miezi mitatu Nairobi.

VOA TV News itakuletea updates Mara zitakapofika mezani kwetu.

0 Comments:

Post a Comment