MBOWE LEO KUUNGURUMA KAMPENI ZA KINONDONI




MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA), Freeman Mbowe, Leo anatarajia kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Salum Mwalim, anayeungwa mkono na UKAWA.

Afisa habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, (KUB)' anatarajiwa  kumuombea kura Mwalimu kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni utakaofanyika leo Jumatatu, saa 8 mchana katika Viwanja vya Mtambani, Kata ya Mzimuni, maeneo ya Magomeni Mikumi.

0 Comments:

Post a Comment