![]() |
| Moja ya nyumba iliyoathirika na Mvua |
Katika Mkoa wa Arusha Habari Tanzania tunaripoti Tukio la January 2 katika wilaya ya Meru ambapo kaya nne ziliathirika na mvua hizo kwa kuvunjiwa nyumba zao na uharibifu Mkubwa wa vyakula.
Kaya zilizoathirika na mvua hizo zipo kwenye kitongoji cha Nkoamangashi katika Kata ya Kikatiti. Familia hizo ni kama ifuatavyo Famila Charles Litoi mbise, Familia ya Bw. Frank Charles, familia ya Emanuel Wariaeli, na Familia ya Ndugu Afraeli Emanuel.
Kufauatia athari hizo Viongozi wa maeneo hayo Kitongoji hadi kata wakawa karibu zaidi kuzinusuru familia hizo kutokana na janga hilo.
Diwani wa kata ya Kikatiti Mh. Elias Mungure akawataka wasamaria wema kuungana na wanakitongoji hao ili kufidhia hasara zilizotokea na kuzinusuru kaya hizo dhidi ya njaa baada ya vyakula kuharibiwa.
![]() |
| Diwani wa Kata ya Kikatiti Mh Elias Mungure akitoa maelekezo wakati akiwapa pole wahanga wa Tukio hilo. |
![]() |
| Mifuko 8 ya Saruji na Chakula kwa familia zilizoathirika na mvua iliyonyesha hapo Jana. |
Awali Mwenyemiti wa kitongoji hicho Jacob Emanuel alieleza tukio hilo lilivyotokea na kuwa wa kwanza kutoa msaada wa haraka pamoja na kutoa taarifa kwa viongozi wengine kwa ajili ya msaada zaidi.
Wakati mvua hizo zikinyesha na tukio hilo kutokea majira saa tisa za alasiri mmoja wa mwana kaya alieleza ilivyokuwa huku kwa bahati nzuri Hakukua na mtu aliyejeruhiwa.
Mashuhuda wanasema mvua kubwa iliyoambatana na Upepo mkali , mawe ya barafu iliezua mabati ya nyumba na pelekea kuta za nyumba kuvunjika bibaya , Ripoti hii pia ilishuhudia hali ya nyumba hizo pamoja na Miti mikubwa ya maeneo hayo ilivyovunjwa vunjwa ovyo.



0 Comments:
Post a Comment