MASHAHIDI kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wamedai kuwa mbunge huyo alifanya makosa kueleza ndoto yake hadharani kwani iliibua hisia mbaya kwa wananchi huku wakishindwa kutaja kifungu cha sheria kikichovunjwa wala tukio lolote lililotokea mpaka sasa kutokana na kauli hizo anazodaiwa kuzitoa oktoba 22, 2016.
Aidha walidai Lema alikosea kuwaeleza wananchi kuwa hawezi kuvaa sketi juu ya suruale baada ya kudai nchi inaandaliwa kuingia kwenye udikteta na mwanaume atakuwa mmoja tu Rais John Magufuli.
Mashahidi hao wa nne na watano WA upande WA Jamhuri ambao ni polisi wameyasema hayo leo mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Arusha, Devota Msofe wakati walipokuwa wakiongozwa kutoa ushahidi wao na wakili wa Serikali, Agnes Hiyera na kuhojiwa na mawakili wa utetezi, John Mallya na Sheki Mfinanga.
Shahidi wa nne, H 2261, Mongo,(25), ambaye ndiyo alipiga picha za video za mkutano ulifanyika Kambi ya Fisi kwenye kata ya Ngarenaro aliieleza mahakama hiyo kuwa anayoyaongea ni yale aliyoyasikia uwanjani kwani baada ya mkutano kumalizika alikabidhi kaseti ya video kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, (RCO), na hakuwahi kuiona tena.
Hata hivyo shahidi huyo alidai kuwa Mkuu wa Upelelezi wa wilaya ya Arusha, (OC CID), Damas Massawe hakuwa kwenye mkutano huo na kuwa yeye ndiye alimfuata ofisini kwake na kumweleza mambo yaliyotokea kwenye mkutano jambo linalowafanya watofautiane na Massawe ambaye ni shahidi wa kwanza kwenye shauri hilo kwani aliieleza mahakama hiyo kuwa siku ya tukio alikuwa kwenye mkutano huo.
Akihojiwa na wakili wa Lema, Mfinanga, Mongo alikiri kila mtu ni lazima atakufa na kifo hakiwezi kusababisha vurugu huku akisema hakumsikia Lema akisema atamuua Rais wala Mungu atamchukua Rais.
Hata hivyo shahidi huyo aliieleza mahakama si kosa kwa Lema kutoa taadhari kuwa endapo Rais akiendelea kuminya demokrasia itatokea umwagaji damu na nchi inaandaliwa kuingia kwenye udikteta na mwanaume atabaki mmoja ambaye ni Rais (Magufuli) hivyo hayuko tayari kuvaa sketi juu ya suruale.
Shahidi huyo alinukuu maneno aliyodai kuwa yalitolewa na Lema kwenye mkutano huo kuwa " nchi inaandaliwa kuingia kwenye udikteta na mwanaume atakuwa mmoja. Rais Magufuli.Lema amesema hawezi kuvaa sketi ndani ya suruale na aliwataka wananchi kujiandaa kudai yao kwa njia yoyote,".
Kwa upande wake shahidi wa tano, Lubia ambaye ni Mkaguzi ni mkaguzi wa operesheni za polisi jijini Arusha aliieleza mahakama kuwa siku hiyo NB ya Mkutano Lema alisema kuwa Meya na madiwani wameshazungumzia miradi ya maendeleo hivyo atakachofanya ni kumzungumzia Rais Magufuli pamoja na wateule wake Mkuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya wanavyominya demokrasia.
"Kama mheshimiwa Rais na Serikali yake wataendelea kuminya demokrasia na kudharau viongozi wa upinzani iko siku nchi itaingia kwenye machafuko na umwagaji damu na kwamba Jeshi la polisi na majeshi mengine hawataweza kuzuia uhalifu utakaotangazwa," shahidi huyo wa Jamhuri aliieleza mahakama akidai mneno hayo yalisemwa na Lema kwenye mkutano huo.
Shahidi huyo alidai kuwa maneno ya Lema yaliwapa wananchi hisia za kwenda kuvunja sheria akiwemo yeye ambapo Wakili Mallya aipomtaka endapo kuanzia kauli hiyo ya Lema ilipotolewa oktoba 2016 mpaka sasa kama imesababisha tukio lolote la uvunjifu WA Sheria shahidi huyo alidai hana jibu mahsusi.
Shauri hili linalovuta hisia za wengi linaendelea kesho.

0 Comments:
Post a Comment