Kada Maarufu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tambwe Hizza, amefariki leo alfajiri.
Mmoja wa watu wa karibu na marehemu amesema," Twambwe alikua ameamka saa kumi anajisikia vibaya akasema aende hospitali Kizuiani kufika geti gari likaanza kuyumba akafanikiwa kusimamisha,".
Anadai watu alienda kuangalia wakamkuta ametulia kwenye gari lake ambapo alikuwa peke yake.
Meya wa Ubunge, Boniface Jacob, amenukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha taarifa za kifo cha Tambwe.
Inadaiwa Marehemu Tambwe alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa pumu na amefariki akiwa ni mmoja wa waratibu wa kampeni za chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) katika jimbo la Kinondoni.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Temeke.

0 Comments:
Post a Comment