HUZUNI WENGI WAZIMIA WAKIMUAGA AKWILINA LEO


HUZUNI, Vilio na Simanzi hali iliyopelekea  baadhi ya wanafunzi  wa Chuo cha Usafirishaji,(NIT), kupoteza fahamu wakati wakimuaga mwanafunzi mwenzao, Akwilina Akwilini aliyefariki baada ya kupigwa risasi ya kichwa na polisi akiwa kwenye daladala wakati polisi hao wakitawanya maandamano ya Chadema ijumaa iliyopita.


 baadhi ya matukio ya huzuni yanayojitokeza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), baada ya kuwasili mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho, Akwilina Akwiline.
Mwili wa mwanafunzi huyo unaagwa leo, Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho.
Wanafunzi zaidi ya wanne aliokuwa akisoma nao Akwilina chuoni hapo ni kama hawaamini baada ya kushuhudia jeneza lenye mwili wake, huku wengine wakipoteza fahamu na kupewa huduma ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Viongozi waliofika mpaka sasa katika viwanja vya NIT ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi; Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako; Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni; Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika.
Tayari ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo imeanza.

0 Comments:

Post a Comment