MAMLAKA ya Mapato nchini, (TRA), imebaini Askofu Zakary Kakobe hana akaunti binafsi kwenye benki yoyote nchini huku akaunti ya kanisani lake la Full Gospel Fellowship likiwa na zaidi ya sh 8.1 bilioni benki.
Aidha imebaini kuwa kanisa hilo linaweka kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na majaba huku wakiwa hawafuati taratibu za kupeleka na kurejesha fedha benki.
Pia imedaiwa kanisa hilo haliandai taarifa ya mapato na matumizi huku fedha za kanisa zikitumika kugharamia ujenzi wa nyumba binafsi ya mke wa Askofu Kakobe na kugharamia Safari binafsi za familia nje ya nchi.



0 Comments:
Post a Comment