LOWASSA AKIFARIJI WAFIWA KWA KINGUNGE

Waziri mkuu wa zamani na  mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefika nyumbani kwa Kingunge Ngombale Mwiru aliyefariki alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa  Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.


Lowassa ameungana na waziri mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim, Spika mstaafu  Pius Msekwa na mke wake Mama Anna Abdallah, Kamanda Mstaafu wa Polisi  mkoa wa Dar es salaam, Suleiman Kova na viongozi wengine katika kuwafariji ndugu jamaa na marafiki waliojiyokeza Nyumbani hapo.

Lowassa alikuwa rafiki  wa siku nyingi wa marehemu Kingunge ambapo urafiki huo ulidhihirika wazi pale muasisi huyo wa CCM alipojivua uanachama wa Chama hicho na kuzunguka maeneo mbalimbali nchini akimuombea kura za Urais Lowassa aliyekuwa akigombea Kwa tiketi ya CHADEMA akiwakilisha vyama vinavyounda umoja wa katiba, UKAWA.

0 Comments:

Post a Comment