Mbunge Joshua Nassari leo akitoka mahakamani.
Wakili wa Serikali Fortunate Mhalila alisomewa shitaka hilo leo mbele ya Hakimu Jasmine Abdul, ambapo Nassari anadaiwa kitenda kosa hilo maeneo ya Malina wilayani Arumeru.
Alidaii kuwa Nassari alimshambulia Ngudu kwa kumpiga mateke katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia maumivu makali.
Wakili wa Serikali Mhalila aliomba shauri hilo lipangiwe siku nyingine kwani upalelezi bado haujakamilika.
Nassari anayetetetewa na wakili Sheki Mfinanga likanaka makosa hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na diwani Gabriel Mwanda sanjari na kusaini bondi ya shilingi milioni 5.
Hakimu Jasmine ameahirisha shauri hilo mpaka Machi 6, mwaka huu litakaporudi mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa


0 Comments:
Post a Comment