Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale-Mwiru, 87, amefariki dunia.
Mzee Kingunge amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa wa Nyumbani kwake.
Alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) hadi alipojiuzulu kutoka kwenye chama hicho mwaka 2015.
Kingunge amefariki ikiwa ni siku chache baada ya mke wake,Peras kufariki January 4, mwaka huu na kuzikwa Januari 11, mwaka huu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini DAR es Salaam.
Source BBC




0 Comments:
Post a Comment