ZITO AISHUKIA SERIKALI MAUAJI YA RAIA

KIONGOZI Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo,Zitto Kabwe,ameeleza kusikitishwa kwake na matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali hapa nchini na kuitaka Serikali kuunda tume huru kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha matukio hayo na taarifa ziwekwe wazi ili jamii ijue.
Amesema kuwa matukio hayo kwa sasa yamekuwa yakishika kasi na yameonekana kuwa ni matukio ya kawaida tu ili hali damu za Watanzania wasio na hatia imekuwa ikimwagika kila kukicha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kabwe ambaye pia ni mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT-Wazalendo aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,alipokuwa katika ziara yake na kutembelea Kata zinazoongozwa na Madiwani kupitia chama hicho.
Akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,pamoja na viongozi wengine ngazi ya Taifa na mikoa atakayotembembelea alisema kuwa lengo la ziara yake hiyo ni kuwashukuru wananchi wa Kata hizo kwa kuwapa dhamana ya kuongoza kata hizo katika uchaguzi mkuu wa oktoba 2015.
“Pia tutashiriki kazi za maendeleo,kushawishi utekelezaji wa maono ya azimio la Tabora kwenye miradi ya maendeleo,kutafuta majawabu ya changamoto zinazowakabili,kusikiliza kero zao na kuzifikisha katika mamlaka husika,kukagua utendaji wa madiwani,ikiwa ni pamoja na kusisitiza uwazi,uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote yahusuyo Kata zao”alisema Zitto.
Kadhalika alizungumzia hatua ya wao kukamatwa na polisi walipokuwa katika ziara yao ya mkoani Morogoro wakitokea Mkoa wa Pwani kuwa walishishwa kuendelea na zira yao katika Mkoa huo baada ya kukamatwa na polisi na kulazimika kulala ndani kabla ya kuachiwa kwa dhamana jana ambapo leo wataendelea na zira yao katika kata ya Sale Wilayani Ngorongoro Mkoani hapa ambapo wana madiwani wawili.
Akizungumzia hatua yao ya kukamatwa na polisi alisema kuwa ni baada ya wao kuamua kutembea kwa miguu kwa mwendo  mrefu kuelekea Kata ya Luela kutokana na kukosekana kwa barabara ya kuingia na kutoka katika kata hiyo na ndipo walipokamatwa na polisi kwa maelezo kuwa wametumwa na wakubwa wao wa kazi kwa madai kuwa nimefanya mkutano bila kibali ilihali hakuna mkutano wowote tulioufanya.

0 Comments:

Post a Comment