ASKOFU AMANI APIGA STOP WENYE MIMBA KUVAA SHELA

Askofu MKUU wa Kanisa Katoliki jimbo kuu la Arusha,Isaac Amani Massawe amepiga marufuku maharusi wa kike wenye ujauzito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kanisani

Aidha Askofu huyo pia amezuia kufanyika kwa sherehe za ubarikio ,ubatizo na komunio kwenye  kumbi za starehe.

Askofu Amani ametoa utaratibu huo mpya jumapili April 29, mwaka huu wakati wa misa takatifu ya shukrani aliyoitoa kwa waumini wa kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa katoliki la mt,Thereza jijjni Arusha.


0 Comments:

Post a Comment