FATMA KARUME ALIVYOTWAA URAIS TLS




HATIMAYE Fatma Karume ameibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha urais wa chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) baada ya kumbwaga mshindani wake wa karibu Godwin Simba Ngwilimi.

Karume amechaguliwa kushika wadhifa huo kwenye uchaguzi wao uliofanyika jana jijini Arusha wakati ambapo alipata kura 820
akifuatiwa kwa Ngwilimi ambaye ni Makamu wa Rais anayemaliza muda wake aliyepata kura 364 huku wagombea wengine  Godwin  Mwapongo akiambulia kura 12 na Godfrey Mwasonga akishika mkia kwa kuambulia kura 6.

 Karume anabeba  mikoba ya mtangulizi wake  Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji anakoendelea na matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana septemba mwaka jana mjini Dodoma.

Matokeo hayo yaliyopekewa kwa shangwe na mawakili hao yalitangazwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Oguto Omumwana ambaye pia alitangaza matokeo ya viongozi wa matawi 13 ya TLS.

Viongozi hao waliapishwa na wakili mkongwe Colman Ngalo kushika nyadhifa hizo kama katiba na kanuni za uchaguzi za taasisi hiyo zinavyoagiza.


Awali kampeni za uchaguzi huo zilipamba moto kwenye mitandao ya kijamii ambapo kulikuwa na makundi mbalimbali ya wanaharakati na wanasheria walikuwa wakiwaombea kura wagombea hasa wa nafasi ya Urais.

Aidha kwa siku ya ijumaa ulipoanza mkutano mkuu wa TLS kwenye hoteli ya Mount Meru walionekana baadhi ya wanasheria wakiwa wamevaa tisheti za kumuombea kura Karume

Aidha, wanasheria hao walichanga kiasi cha shilingi 607,000 na dola Marekani 712 kwa ajili ya kuchangia gharama  za aliyekuwa Rais wa TLS,  Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

SALAMU ZA LISSU 

Lissu ashukuru kwa ushirikiano na msaada waliompatia katika wakati wote hata pale aliposhambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akihudhuria vikao vya bunge Mjini Dodoma.

Aliwashukuru kwa michango ya damu, fedha za kugharamia matibabu pamoja na kumtembelea kwa kipindi cha miaka minne aliyokuwa akipatiwa matibabu Nairobi Kenya.

Ambapo alisema anastaafu kwa sasa nafasi ya Urais lakini wataendelea kukutana kwenye harakati ambapo baada ya salamu hizo wajumbe wa mkutano huo walisimama kwa ishara ya kupokea salamu hizo.


0 Comments:

Post a Comment